Aina gani ya Nyumba inayofaa Kuchukulia Mkopo Bank?

Aina gani ya Nyumba inayofaa Kuchukulia Mkopo Bank?

maana malengo yangu nitoe mtaji wangu ofisini kama 3m-5m nijenge room chumba na sebule,then niende bank wanipe 30m nikitoa 5m nikirudsha kwenye mtaji nabaki na 25m ambazo zinantosha sana.[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Kwa mtaji huo the most utapata 5 mpaka 10


Sent using Jamii Forums mobile app
5m ninayotoa ofisini sio kwamba ni Fixed Capital mkuu, hiyo ni balance ambayo ipo kuipa backup original Capital incase imeyumba ndio mana naweza chomoa 5m na biashara ikaendelea.

Ila kama watanipa 5m to 10m watakuwa wamenipunja sitokuwa na haja ya ku risk this much kwa pesa ambayo siko na uhakika itakuja au lah.
 
Bank statement yako inazungusha kiasi gani kwa mwezi
Una mtaji wa bei gani?
Una miliki kitu gani kingine?
Kwa kuanzia huwezi pewa hiyo pesa wakikupa nyingi sana ni 10M tena kwa madhumuni ya kuendeleza biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Bank Statement kwa mwezi 100m-150m

2. Mtaji 60m

3. Namiliki kiwanja Tu (Mali isiyohamishika) Zinazohamishika ni Biashara ya Piki Piki (Boda Boda) zipo 11..

Kunipa hela chini ya 20m bora niukose huo mkopo.
 
ila hizi bank ifike mahali waanze kutuangalia tusio na nyumba na viwanja vyenye hati
Benki sio shirika la kujitolea wala msaada. Wewe kwenye biashara yako huwa unakopesha mdada jobless asiye na makazi maalum ambaye muda wowote anabebwa na mhuni akafanye sogea tuishi?
Hiyo ni biashara na ina misingi, sio huruma
 
Habari zenu wakuu,nimerudi tena kuuliza swala ambalo limekua likinipa shida sana mwezi huu nadhani akili imewaka mpaka sasa sijui mwisho ila sijakata tamaa.

Nilifungua huu uzi hapa chini nikiomba msaada kwa mwenye msaada anisaidie kunipa nyumba yake nichukulie mkopo, Bank nilizoenda zote walikataa nyumba ya mtu ambae ni mwana familia.


Baada ya kugonga mwamba niliwashukru walioweza jitoa muhanga kuniamini eneo hilo mpaka mtu anaridhia kukupa hati yake ya nyumba sio masihara ndugu zangu Jamii Forum ina watu na Malaika hakika.

Basi baada ya kukaa kutafakari nimerudi tena kwenu kuuliza wajuzi...

Bank wanahitaji Mtu uwe na kiwanja ulichokiendeleza, nikawaza haraka haraka Je nikiamua kuinua nyumba ya kawaida kabisa kwa bajeti ya 3m-5m nitoe room ya vyumba vitatu tu. au chumba na sebule

Hapa naongelea nyumba ya kawaida kabisa kabisa isiyo na chembe ya mbwembwe aina yoyote ile very local house lakini perfect one ambayo mtu anaweza kuishi vizuri tu.

Je,kwa nyumba ya Chumba na Sebule na Choo au Chumba,Sebule,Sebule , kisha Baada ya kumaliza hiyo nyumba nirudi bank tena sasa kukopa.

Hii nyumba itakubalika au watataka nyumba kubwa kabiisaa hii yangu wataiona kibanda? na Je nikishaijenga nilazima niingie nianze kuishi hapo au nikiinua tu nikaimaliza inatosha?

Labda sijaeleweka swali, nauliza kwa nyumba hyo mkopo nitapewa? Maana bank wanaweza nipa up to 30m kwasasa kulingana na mzunguko wangu wa biashara.

Je hizi 30m wakija kuangalia nyumba wakikuta ni Local,hawatoninyima? naomba msaada wa mawazo wakuu.

maana malengo yangu nitoe mtaji wangu ofisini kama 3m-5m nijenge room chumba na sebule,then niende bank wanipe 30m nikitoa 5m nikirudsha kwenye mtaji nabaki na 25m ambazo zinantosha sana.

Mawazo yenu ndugu zangu,nina hesabu ambazo sielewi nauliza ili nipate uhakika nisije choma mtaji biashara ikafa nikaishia kubaki na nyumba ambayo hata si ya ndoto au hata mawazo yangu.

asanteni kwa mtakaoshiriki kunishauri
Kanisa linalipa kwani watakao kuja kusali na kuombewa ndio watakaolipa deni.
 
Benki sio shirika la kujitolea wala msaada. Wewe kwenye biashara yako huwa unakopesha mdada jobless asiye na makazi maalum ambaye muda wowote anabebwa na mhuni akafanye sogea tuishi?
Hiyo ni biashara na ina misingi, sio huruma
Maana yangu ni waangalie masharti tu mkuu, mbona kwenye simu online siku hizi kuna vimikopo na app zipo kibao unaanza kopa anzia kiasi kidogo hivyo hivyo hadi unapanda kwa kujidhamini mwenyewe tu, kwanini bank wao wanashindwa?
 
ila hizi bank ifike mahali waanze kutuangalia tusio na nyumba na viwanja vyenye hati
Siyo lazima uwe na nyumba, kama umewekeza pesa pia kwenye dhamana za Serikali (Government bonds) unatumia ile hati kuombea mkopo benki nyingine.
 
5m ninayotoa ofisini sio kwamba ni Fixed Capital mkuu, hiyo ni balance ambayo ipo kuipa backup original Capital incase imeyumba ndio mana naweza chomoa 5m na biashara ikaendelea.

ila kama watanipa 5m to 10m watakua wamenipunja sitokua na haja ya ku risk this much kwa pesa ambayo siko na uhakika itakuja au lah.
Ok sawa nimekupata vema lakini wanakuwa na ma QS wao wa kutathmini thamani halisi ya nyumba
Vilevile wanaangalia mtaji
Kisha mapato yako kwa mwezi
Na mwisho mzunguko wako wa cash kwa mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo lazima uwe na nyumba,kama umewekeza pesa pia kwenye dhamana za serikali (Government bonds) unatumia ile hati kuombea mkopo benki nyingine.
Government Bonds hata sizijui mkuu, hebu nifungue macho eneo hilo nijipatie chakujiongezea point labda huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom