Huo ni mkopo direct wa ujenzi na kiwanja ndio dhamana na marejesho yake ni ya muda mrefu.. Hapa mara nyingi unaingia ubia na bank na marejesho huanza baada ya jengo kukamilika na kuanza biashara
Kwa kifupi pesa yote inakuwa controlled na bank, kwakuwa ujenzi kama huo hupewa mkandarasi aliyesajiliwa na kuidhinishwa na bodi ya wakandarasi
Wewe kazi yako ni kusaini tu ili jamaa alipwe na bank.. Na ukianza biashara pesa inapitia kwenye account ya bank husika
Mikopo ninayozungumzia yenye gundu ni pale biashara zinaenda vema, na una maokoto ya kutosha tu halafu unataka kupanua biashara zako bila hasa kuwa specific utautumiaje huo mkopo.. Hizo pesa huitwa mlango wazi kwakuwa ukishaitia mkononi huibuka dili ya faida ya haraka nawe bila kuwaza unajitumbukiza humo
Unakumbuka ile simulizi hapa JF ya jamaa aliyekopa 4B na sasa ni kapuku?
Sent using
Jamii Forums mobile app