Habari zenu wakuu,nimerudi tena kuuliza swala ambalo limekua likinipa shida sana mwezi huu nadhani akili imewaka mpaka sasa sijui mwisho ila sijakata tamaa.
Nilifungua huu uzi hapa chini nikiomba msaada kwa mwenye msaada anisaidie kunipa nyumba yake nichukulie mkopo, Bank nilizoenda zote walikataa nyumba ya mtu ambae ni mwana familia.
Habari zenu wana jamiii, ni matumaini yangu mu wazima wa afya tele. Nina Shida ya Pesa ya dharura nimejaribu kukopa kwa watu binafsi hawana, katika taasisi nao wanahitaji dhamana (hasa nyumba). Nimefika Bank CRDB nimewambia hitaji langu,wakaniambia mahitaji kwa mfanyabiashara kama mimi, Vyote...
www.jamiiforums.com
Baada ya kugonga mwamba niliwashukru walioweza jitoa muhanga kuniamini eneo hilo mpaka mtu anaridhia kukupa hati yake ya nyumba sio masihara ndugu zangu Jamii Forum ina watu na Malaika hakika.
Basi baada ya kukaa kutafakari nimerudi tena kwenu kuuliza wajuzi...
Bank wanahitaji Mtu uwe na kiwanja ulichokiendeleza, nikawaza haraka haraka Je nikiamua kuinua nyumba ya kawaida kabisa kwa bajeti ya 3m-5m nitoe room ya vyumba vitatu tu. au chumba na sebule
Hapa naongelea nyumba ya kawaida kabisa kabisa isiyo na chembe ya mbwembwe aina yoyote ile very local house lakini perfect one ambayo mtu anaweza kuishi vizuri tu.
Je,kwa nyumba ya
Chumba na Sebule na Choo au
Chumba,Sebule,Sebule , kisha Baada ya kumaliza hiyo nyumba nirudi bank tena sasa kukopa.
Hii nyumba itakubalika au watataka nyumba kubwa kabiisaa hii yangu wataiona kibanda? na Je nikishaijenga nilazima niingie nianze kuishi hapo au nikiinua tu nikaimaliza inatosha?
Labda sijaeleweka swali, nauliza kwa nyumba hyo mkopo nitapewa? Maana bank wanaweza nipa up to 30m kwasasa kulingana na mzunguko wangu wa biashara.
Je hizi 30m wakija kuangalia nyumba wakikuta ni Local,hawatoninyima? naomba msaada wa mawazo wakuu.
maana malengo yangu nitoe mtaji wangu ofisini kama 3m-5m nijenge room chumba na sebule,then niende bank wanipe 30m nikitoa 5m nikirudsha kwenye mtaji nabaki na 25m ambazo zinantosha sana.
Mawazo yenu ndugu zangu,nina hesabu ambazo sielewi nauliza ili nipate uhakika nisije choma mtaji biashara ikafa nikaishia kubaki na nyumba ambayo hata si ya ndoto au hata mawazo yangu.
asanteni kwa mtakaoshiriki kunishauri