Aina gani ya Nyumba inayofaa Kuchukulia Mkopo Bank?

1.Bank Statement kwa mwezi 100m-150m

2.Mtaji 60m

3.Namiliki kiwanja Tu (Mali isiyohamishika) Zinazohamishika ni Biashara ya Piki Piki (Boda Boda) zipo 11..

Kunipa hela chini ya 20m bora niukose huo mkopo.
Hapo unaweza kupata kati ya 30 mpaka 40.. Lakini pia kama ukiweza achana na mikopo kwasasa huwa ina gundu fulani hasa kama biashara zako zinafanya vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok sawa nimekupata vema lakini wanakuwa na ma QS wao wa kutathmini thamani halisi ya nyumba
Vilevile wanaangalia mtaji
Kisha mapato yako kwa mwezi
Na mwisho mzunguko wako wa cash kwa mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka hela uipate BANK kazi sio ndogo, wanasema mwanzoni huwa pagumu sana.

Ila kuna watu bank inawamwagia tu mihela, dhamana zinatucost sana.
 
Mpka hela uipate BANK kazi sio ndogo,wanasema mwanzoni huwa pagumu sana.

Ila kuna watu bank inawamwagia tu mihela,dhamana zinatucost sana.
Wana formalities nyingi sana na vigezo vya kutosha
Lazima watembelee biashara na kujiridhisha ni ya kwako kweli
Lazima wakupige picha ukiwa ndani na nje ya biashara yako
Lazima uwe na TIN na leseni ya biashara
Lazima uwe na mkabata wa upangaji usiopungua miezi 6
Lazima wakague hesabu za mauzo yako daily, weekly na monthly
Lazima watembelee unapoishi na kama umepanga waone mkataba
Lazima uwapelekee nyaraka za serikali y a mtaa
Kama umeoa lazima uoneshe cheti cha ndoa na mkeo ajue unakopa
Lazima uoneshe bank statement ya walau miezi 3 hivi

Kwenye dhamana
Kama nyumba ni yako utawakabidhi hati ama leseni ya makazi
Lazima waitembelee na kama huishi hapo kuna QS wao ataitathmini
Lazima wafike ardhi kujiridhisha nknk

Hivi vigezo baadhi vina gharama na mlipaji ni wewe
Nyumba ya dhamana lazima uikatie bima kulingana na thamani iliyoandikwa
Mkopo nao lazima uukatie bima
Na kuna processing fee ya mkopo.. Ukiomba 10M unaweza kuondoka na 9.3


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh hili nalo neno
 
Na kuna processing fee ya mkopo.. Ukiomba 10M unaweza kuondoka na 9.3
Processing fee ni uonevu tu kwakweli yaani bank wao hawataki ingia cost popote pale yaani wao wanajiweka safe side, kwako ni loose loose tu usiporudsha pesa yao.

Ila nawaelewa sana maswala ya pesa nawaelewa sana wako sahihi na ni haki yao.
 
Una utani sana na hao jamaa, hao jamaa ni smart na mpaka wakakubali dhamana ya hiyo nyumba basi ina thamani zaidi ya pesa watakayokupa, hao wajanja zaidi ya unavyojua.

Kama wakipiga hesabu nyumba ni million 5, utapata mkopo wa mil 1 na haiwezi kuzidi 2.5mil na siku ukishindwa kulipa, utaelewa kama kazi zao hawabahatishi.
 
Hapo unaweza kupata kati ya 30 mpaka 40.. Lakini pia kama ukiweza achana na mikopo kwasasa huwa ina gundu fulani hasa kama biashara zako zinafanya vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
"Mikopo huwa ina gundu fulani"

Nilisoma mahali eti kujenga ghorofa kwa hela yako mfukoni haifai inatakiwa ujengee mkopo. How do you say on that?
 
"Mikopo huwa ina gundu fulani"

Nilisoma mahali eti kujenga gorofa kwa hela yako mfukoni haifai inatakiwa ujengee mkopo. How do you say on that?
Huo ni mkopo direct wa ujenzi na kiwanja ndio dhamana na marejesho yake ni ya muda mrefu.. Hapa mara nyingi unaingia ubia na bank na marejesho huanza baada ya jengo kukamilika na kuanza biashara
Kwa kifupi pesa yote inakuwa controlled na bank, kwakuwa ujenzi kama huo hupewa mkandarasi aliyesajiliwa na kuidhinishwa na bodi ya wakandarasi.

Wewe kazi yako ni kusaini tu ili jamaa alipwe na bank.. Na ukianza biashara pesa inapitia kwenye account ya bank husika

Mikopo ninayozungumzia yenye gundu ni pale biashara zinaenda vema, na una maokoto ya kutosha tu halafu unataka kupanua biashara zako bila hasa kuwa specific utautumiaje huo mkopo.. Hizo pesa huitwa mlango wazi kwakuwa ukishaitia mkononi huibuka dili ya faida ya haraka nawe bila kuwaza unajitumbukiza humo

Unakumbuka ile simulizi hapa JF ya jamaa aliyekopa 4B na sasa ni kapuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kama una shida serious ya hela, labda 30m, una nyumba / eneo lenye thaman ya 50m.

Ushauri wa bure:
  • Uza property yako.
  • Maliza shida yako.
  • Nunua eneo simple.
  • Panga nyumba....
Hizo hela za marejesho lipa kodi na jipange upya, kubali kuanza upya ila kwa amani.

Nikuhakikishie:

Asilimia 99% ya wachukua mkopo hushindwa kulipa, kupoteza property au, kuishi maisha ya msongo wa mawazo muda mrefu, na hata kufa.
 

Hio 30M unahitaji ndani ya muda gani? Maana hio process unayopitia naona ni ndefu
 
1.Bank Statement kwa mwezi 100m-150m

2.Mtaji 60m

3.Namiliki kiwanja Tu (Mali isiyohamishika) Zinazohamishika ni Biashara ya Piki Piki (Boda Boda) zipo 11..

Kunipa hela chini ya 20m bora niukose huo mkopo.

Hujapata tu connection ya sehemu za kukopa ila unakopesheka nje ya bank ungekuwa saccos hio pesa 30M unaipata bila bank statement, na kelele nyingi mimi nimechukua 25M saccos kwa hati ya kiwanja tu ofcourse wadhamini wangu pia wamechangia.

Endelea kufatilia utapata option tu lazima.
 

Nautafuta huo uzi niliusoma lakini siku subscribe
Ila 4B ni parefu dah kwa sisi ambao hatujawahi kufika huko tunaona maluweluwe
 
"Mikopo huwa ina gundu fulani"

Nilisoma mahali eti kujenga gorofa kwa hela yako mfukoni haifai inatakiwa ujengee mkopo. How do you say on that?

Hakuna gundu lolote, mkopo utumike kwenye biashara ambayo tayari ina run tena biashara iwe tayari ina miezi 18 na zaidi na uelekeo umeshaonekana, tatizo wengi tuna haraka unachukua mkopo na biashara ndio inaanza utateseka sana.

Au chukua mkopo ka inject sehemu isiyozalisha na huna backup ya biashara angalau mbili utaita maji mma
Unaweza kukopa na kurejesha bila stress ila lazima akili itulie.
 
Hiyo milioni 30 umeitoa wapi wakati hawajaja kukufanyia tathimini?.Haupewi mkopo kwa kiasi unavyotaka wewe.Maafisa mikopo wanakuja kwako wanatathimini mali unayoiweka kama dhamana na uwezo wa marejesho kupitia biashara mara muda wakurejesha mkopo na riba yake ndo wanakufanyia tathimini ya kiasi utakachoweza kupata.Sio lazima nyumba iliyokamilika kwasababu ata kiwanja chenye hati kuna bank zinapokea.
 
Ni kweli mkuu,kuna dada mmoja niliongea nae akaniambia hata kikoba chao wanaweza kopesha mtu kwa kiasi hicho ila sikua mwanachama kwahyo shida ikaanzia hapo.

Mpaka sasa sielewi akili inazidi kuegamia kwenye ujenzi tu wa hicho kijumba nione bank wakija kuthaminisha wataniambiaje..

nishajaribu sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…