Aina gani ya Nyumba inayofaa Kuchukulia Mkopo Bank?

Mil.30 nimeitolea bank, sikuwa najua naweza pewa hicho kiasi wao ndio waliniambia kutokana na mzunguko wangu wa biashara kupitia account yangu wanaweza nipa up to 30m.

Wakaniambia tu nahitajika dhamana, ila si kwamba mimi niliwambia nataka 30m ni wao baada ya kuwaeleza nia yangu wakaniambia wanahitaji kuangalia mzunguko wa pesa kwa account yangu ndio wakanipa majibu hayo.

Flat Plot Hamna BANK wanapokea hata kama kina HATI ilikuwa ni zamani sasa hivi kiwanja lazima uwe umekiendeleza kwa kukifanyia chochote kile. Otherwise hiyo Plot unayotaka chukulia mkopo iwe Center kweli kweli (napo sina hakika kama watakubali kulingana na policy za mabank za sasa) labda unyooshe mkono.

Na maswala ya kugawa hela kwa maafisa, hela yenyewe nakopa halafu naanza igawa tena naonaga mikosi inaanziaga humo.
 
Hio 30M unahitaji ndani ya muda gani?maana hio process unayopitia naona ni ndefu
30m in 6 month ndani ya miezi 6 nina uhakika itakuwa imenizalishia faida ya kutosha na kunitunishia Mtaji wangu.

Nitawarudishia pesa yao nitabaki na biashara yangu iliyo stable tena kama mwanzo.
 
ID ya Mshana imevamiwa anatoa madini huu uzi. Tofauti na mada za kufikirika anazopenda
 
Ukiwa mtafutaji anza na kukopa kwenye vikundi vidogo vya kuweka na kukopa. Kule mnakutana watu like minded mnaojuana na wenye vyanzo vya mapato. Huko gharama za kukopa ni ndogo na mlolongo ni mfupi na riba sio kubwa. Na mikopo hii ina faida kubwa kuliko ya mabenki. Kisha ukizoea kulipa hiyo, biashara yako ikakuwa na ukawa na vyanzo vingi na assets nyingi ndio ukope benki mkopo mkubwa kidogo.

Mambo ya kuanza na benki waachie waajiriwa wa serikali
 
Mkuu bank hawana RIBA kubwa, wenye riba kubwa ni hizi microfinace zingine zingine ila amini nakwambia BANK wana riba nafuu mno tofauti na hela wanayoitoa, shida tu ni hela zao hazipatikani kirahisi.
 
Bila hati Hatua pati pesa huu ni unyanyasaji
Kaka Vitus, unataka kusema kuwa unaweza kumpatia mpita njia pesa zako bila kufikiria atazirudishaje? Huo ni utaratibu tu wa Bank na Financial Bodies zenye kusaidia WAJASI.

Nawashukuru kwa kupata uzoefu wa kupata mkopo kupitia bank. Ngoja kwanza niendelee na vicoba hadi pale nitakapopata nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya. Subira yavuta heri.
 
Mikopo inahitaji nidhamu sana, kuna jirani yangu amechukua mkopo ameweka dhamana nyumba ila sasa kakimbilia kula bata Tangaaaa!!!!
 
maaana yangu ni waangalie madharti tu mkuu,mbona kwenye simu online siku hiz kuna vimikopo na app zipo kibao unaanza kopa anzia kias kidogo hvyo hvyo hadi unapanda kwa kujidhamini mwenyewe tu,kwann bank wao wanashindwa?
Hiyo mikopo ya sijuwi M PESA na nduguze nayo wana ku test na viela kidooogo. Usipolipa wanakeketa kwenye salio na maokoto yoyote yatakayoingia kwenye App. Hata hivyo, wanavyo vigezo lukuki kuidhinisha mtonyo kukufikia na siyo kirahisi kama unavyofikiri. Wanafuatilia mazoea yako na line unayoitumia, intensity ya transaction unazofanya mara kwa mara n.k.

Ndugu yangu,
Kwa turn over ya mil 150; nakusihi uushinde moyo wako na endelea tu na biashara huku ukiomba heri. Anza kuweka milioni moja kila mwezi na ndani ya mwaka utakuwa umefikia malengo yako.
 
😄😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…