Aina hii ya maisha mpaka lini kuchelewa kulala na kuwahi kuamka

Aina hii ya maisha mpaka lini kuchelewa kulala na kuwahi kuamka

Mbinguni tutafika tukiwa hoi wakuu sio mchezo fikiria tu lifestyle ya kuchelewa kulala na kuwahi kuamka mwili haupati fursa ya kupumzika ipasavyo unalala saa 7 usiku afu saa 10 alfajiri unapaswa uwe tayari umeamka.

AIna hii ya maisha lazima upate changomoto ya afya ya akili ukiongeza na ugumu wa maisha yaani ukitoboa miaka 50 plus basi mungu ni mwema.
Mara nyingi kazi hiyo inatakiwa uifanye ukiwa na uhakika wa pesa ya ziada kutoka katika mtirirko wake,kama vile incentive,kuiba kidogo sababu naamini ni meneja wa mradi wa Lodge,Camp au Mgodi,sasa kama hivyo ndivyo na wewe wekeza sehemu uwashike watu masikio pia. Au ongesa elimu ya masafa.Otherwise baadae utapata taabu
 
Aahahahahaa mimi siku zote niko majimatitu ama mbagala charambe, utanikuta hapo na dera langu napiga domo kwa wauza mihogo, vidagaa na vitumbua.

Namshukuru Maulana nimestaafu nafunyiiza pensheni yangu inifikishe kileleni.

Mjini sikuhizi naenda kwa koneksheni tuu.

Huko uliko mmesalimika?
Nimesalimika thanks God !

Mmmh wastaafu watoke Mikocheni wajenge Charambe ?!!

Labda Mbweni....mabwepande alike... wastaafu kutoka Mikocheni hawaziwezi kelele na vurugu za uswazi....

Hapo kwako una heka ngapi ?!! Ha ha ha

Ubarikiwe sana ,amen!
 
Hakika !
Si wengi wanajeuri ya kuacha kazi.

Mfumo wa maisha unawafanya wanajikuta watumwa kwenye nyumba zao na kuendelea kufanya kazi ili kumudu gharama za usafiri kwendq na kurudi kazini.

Wachache wanafanikiwa kupata mitaji na kujiajiri karibu na wanakoishi au kuajiriwa karibu na wanakoishi.

Maisha ni kupanga, kupanga ni kuchagua.

Aluta Kontinua.
Hakika !
 
Nimesalimika thanks God !

Mmmh wastaafu watoke Mikocheni wajenge Charambe ?!!

Labda Mbweni....mabwepande alike... wastaafu kutoka Mikocheni hawaziwezi kelele na vurugu za uswazi....

Hapo kwako una heka ngapi ?!! Ha ha ha

Ubarikiwe sana ,amen!


Hata huku mbagala kuna kilinge, karibu Kilingeni Mbagala cc: Mshana Jr

Huku sio habari ya hekari ni kujichanganya tuu na wakulungwa. Kuishi na kadamnasikuna raha yake, siku wakinipa karaha napanda zangu boti huyooo Zanzibar nikipoa na upepo narudi zangu charambe.

Aluta Kontinua.

Kuna dada mmoja nilimuacha kazini hapo nilipostaafu. Siku moja alikiwa na mishe zake akanikuta niko mtaani nasubiria mihogo, akaniita Mama Kasinde...!!! Ni wewe.... ananifahamu fika... (niliamua kukata mawasiliano na watu niliofanyanao kazi baada ya kustaafu nijenge jamii mpya).

Akanifata akaninong'oneza.... si bure, wewe unaendelea na kazi yako namba mbili, kwani na huku kuna wanaotafutwa.... niliishia kucheka tuu.
 
Mbinguni tutafika tukiwa hoi wakuu sio mchezo fikiria tu lifestyle ya kuchelewa kulala na kuwahi kuamka mwili haupati fursa ya kupumzika ipasavyo unalala saa 7 usiku afu saa 10 alfajiri unapaswa uwe tayari umeamka.

AIna hii ya maisha lazima upate changomoto ya afya ya akili ukiongeza na ugumu wa maisha yaani ukitoboa miaka 50 plus basi mungu ni mwema.
Ndio hapo suala la malengo ya kimaisha yanapohusika. Unaishi maisha hayo katika hatua ya kujitafuta, kujiimarisha kiuzoefu wa kazi, kiuchumi, ukiwa na lengo la muda fulani tu, na baada ya huo muda , uwe tayari kwenda hatua ya juu ambayo itakupa ahueni ya hiyo kadhia ya kukosa muda wa kulala. Usipokuwa na malengo thabiti juu ya maisha yako, utajikuta maisha yako yote uko hapo hapo.
 
Hata huku mbagala kuna kilinge, karibu Kilingeni Mbagala cc: Mshana Jr

Huku sio habari ya hekari ni kujichanganya tuu na wakulungwa. Kuishi na kadamnasikuna raha yake, siku wakinipa karaha napanda zangu boti huyooo Zanzibar nikipoa na upepo narudi zangu charambe.

Aluta Kontinua.

Kuna dada mmoja nilimuacha kazini hapo nilipostaafu. Siku moja alikiwa na mishe zake akanikuta niko mtaani nasubiria mihogo, akaniita Mama Kasinde...!!! Ni wewe.... ananifahamu fika... (niliamua kukata mawasiliano na watu niliofanyanao kazi baada ya kustaafu nijenge jamii mpya).

Akanifata akaninong'oneza.... si bure, wewe unaendelea na kazi yako namba mbili, kwani na huku kuna wanaotafutwa.... niliishia kucheka tuu.
Ha ha ha ha kumbe uko huko Charambe kimkakati .......
 
Badili mtazamo wako,adui wako mkuu ni mawazo yako badili unavyofikiri ubadili Maisha yako.
Ingia kwenye madarasa ya utambuzi na ukuaji kiroho uyaone maisha kwenye mwanga bora.
Nje ya Hapo utaishia kuilaumu ccm huku ukiwa mtaji wa wanasiasa upinzani kugombea shamba la mahindi
 
Kuna misemo hii ya maisha...

Life is a game, play it well.
Don't work hard, work smart.

Kibongobongo au daslaaam, wengi tunajitafuta kwa kuajiriwa au kujiajiri. Na moja ya maendeleo ya kujitafuta ni kuwa na P.O. BOX yako, na mjini kumewahiwa ama laah uwe na pesa ndefu hata kariakoo ukitaka kiwanja unapata.

Wengi wetu tumepata pioboksi Mapinga, Vikindu, Gezaulole, Madale, Marambamawili halafu tunajitia moyo naishi kwa nafasi, kuna hewa safi, nafuga, nabustani ya mchicha and the like....

Ila kazi au ujasiriamali ni kariakoo au posta au mwenge au sinza. Kutoka kwenye hivyo vitongoji na uwahi kuamsha goli lako au kusaini saa mbili asubuhi lazima uamke saa kumi alfajiri. Na safari ya kurudi nyumbani jioni na mafoleni ukiwahi umefika saa tano usiku au sita. Ukijitahidi una kausafiri kako unafika saa 4 usiku.

Ukofika kwako hulali puu kama gunia la mahindi, kwanza ukague yaliyotokea kwako siku nzima, ule, uoge, uandae nguo za kesho, kama una mifugo (hata mbwa) uichungulie bandani kuja kulala saa saba usiku eehehehehe.

Afya ya akili lazima ijizime data kadri umri unavyoenda. Suluhisho ni nini?

Saa ingine haya maisha ni konyo tuu.
Wala sio uongo kwanza kipande cha mbagala mpaka kongowe sijui pale uiii kule wakae tu
 
Back
Top Bottom