Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Mamlaka nchini Afrika Kusini zimeripoti kuwepo kwa aina mpya ya Virusi vya Corona, B.1.1.529, ambavyo ni tofauti na aina zingine za virusi vinavyofahamika.
Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mlipuko nchini Afrika Kusini, Prof. Tulio de Oliveira amesema kuwa kirusi hicho kipya kina zaidi ya mabadiliko (mutation) 50 kwa ujumla na mabadiliko mengine 30 katika muundo wa protini ambayo ndio shabaha kuu ya chanjo na njia ya virusi hivyo kuingia katika seli zetu za mwili.
Baadhi ya mataifa duniani yamekwishaanza kuchukua tahadhari dhidi ya Kirusi hiki kipya, ikiwamo Uingereza ambayo imetangaza kuweka zuio la muda la kusafiri kwa mataifa sita ya Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe, Botswana, Lesotho na Eswatini, huku wasafiri wanaofika wakilazimika kukaa karantini.
Waziri wa Afya wa Uingereza, Sajid Javid amesema kuwa wasiwasi wa kirusi hiki unatokana na idadi kubwa ya mabadiliko (mutation), ikitajwa kuwa mara mbili ya kirusi cha Delta pamoja na uwezekano wa chanjo kushindwa kuhimili kirusi hiki, huku akionya kuwa uwezekano wa kutokea kwa maambukizi ni mkubwa kuliko aina zingine za virusi vya corona.
Mpaka sasa kuna jumla ya maambukizi 77 yaliyoripotiwa katika Jimbo la Gauteng pekee nchini Afrika Kusini, maambukizi 4 nchini Botswana na moja nchini Hong Kong, ambayo ni ya msafiri aliyetoka nchini Afrika Kusini.
Kuna wasiwasi kuwa kirusi hicho kinaweza kuwa kimesambaa zaidi, huku ikikadiriwa kuwa maambukizi yote yanayoripotiwa katika jimbo la Gauteng yanaweza kuwa ya aina hii mpya ya Kirusi, huku maambukizi yakikadiriwa kuwa yamesambaa katika majimbo mengine.
UPDATE: MATAIFA YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA AINA MPYA YA KIRUSI
Baada ya Afrika Kusini kuripoti aina mpya ya Kirusi cha Corona, Mataifa kadhaa yakiwemo Singapore, Ufaransa, Kenya na Japan yametangaza kuchukua hatua kukabiliana nacho
Ufaransa, Uholanzi na Japan zimetangaza kuzuia safari za ndege kutoka Afrika Kusini na Nchi jirani. Israel, Singapore na Italia zimeiweka Afrika Kusini, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lesotho na Eswatini kwenye orodha ya Nchi hatari
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema itachukua wiki kadhaa kuelewa madhara ya Kirusi hicho ambacho kwa sasa kinafahamika kama B.1.1.529