Aina ya silaha walizonazo Houthi zinaogopesha na majaribio ya kuzitumia inatoa picha ya azimio lao la vita

Aina ya silaha walizonazo Houthi zinaogopesha na majaribio ya kuzitumia inatoa picha ya azimio lao la vita

Baada ya jaribio la wiki iliyopita kuteka meli na kuipeleka kwenye maeneo yao kushindwa na kusababisha vifo vya askari 10 wa Houth kumewakasirisha sana wanamgambo hao na serikali ya Iran.

Iran imeamua kuingiza meli yake ya kivita katikati ya meli nyengine za kivita zinazojidai kuilinda bahari nyekundu kama kwamba wameamua kuziambia nchi hizo za muungano kwenye bahari iliyo karibu na Yemen na Iran kuwa fanyeni mnachotaka basi.

Houth nao wametoa uwanjani silaha yao ya aina yake ambayo mfano wake kwa mara ya mwanzo imetumiwa na Ukraine katika vita vyake na jeshi la Urusi.silaha hiyo si nyengine bali ni droni ya baharini ambayo ni boti inayojazwa miripuko na kuongozwa ama chini ya bahari au juu yake bila kuwemo na mtu hata mmoja.

Droni ya bahari huwa inakwenda kwa kasi kuelekea kwenye lengo lake na kujibamiza na kuleta mripuko kwa meli za adui

Baada ya kukasirika sana Houth wametoa droni ya baharini hapo jana ambayo kwa bahati mbaya iliripuka kabla ya kufikia meli zinazofungaman na Israel zilizokuwa zikipita maeneo hayo..Hata hivyo jaribio la matumizi la droni hiyo kumetoa picha ya nia ya kuendeleza mashambulizi yao kwa meli zinazopingana na onyo la Houth.
sijaelewa...
 
Allah amefunguwa chuo wapi?
Elilmu yote ni yake.Hana haja ya kufungua chuo.Yesu (Issa a.s) na mitume wote hawakuhitimu chuo chochote lakini elimu zao ni miujiza mitupu sio kama wewe mbumbumbu
 
Back
Top Bottom