denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Mimi ninachoamini, hata mtu kuwa katikati ya mfumo mbaya, lakini anaweza kusimama mwenyewe kwa misingi yake akajitenga na huo mfumo mbovu akafanya mambo yake na jamii ya watanzania anayoiongoza ikamuelewa.
Chukulia mfano wa Magufuli, ulizuka mtindo wa kuita serikali ya Magufuli na CCM ya Magufuli, hii ilikuwa na maana kwamba, CCM na serikali vyote vilikuwa vinaendeshwa kwa mtazamo na maono ya Magufuli, hapa ndipo unapoita udhaifu wa sheria na Katiba kwenye andiko lako.
Utaona wazi kwamba, kumbe huo udhaifu wa sheria na Katiba unaweza kutumia na kiongozi aliyepo madarakani either positively au negatively, zile sheria ziko pale kwenye maandishi lakini mtekelezaji ndie anaebeba huo mzigo wa udhaifu wake, hasa ukizingatia anaweza kuugeuza huo udhaifu ukaonekana na manufaa kwa jamii anayoiongoza.
Sasa turudi kwa Samia, naona umeamua kutupia lawama zako zote kwa wasaidizi wake, kwamba wao ndio chanzo cha makosa anayofanya Samia.
Na makosa hayo ni mengi, kuanzia zile teuzi zake, anateua leo anatengua kesho ambapo hiyo tabia imekuwa ikijirudia mara kwa mara toka alipoapishwa. Sasa kwa hali ya kawaida alitakiwa aone kama hawa wasaidizi wangu wananipotosha nakosea kila wakati, ni bora nifanye mambo yangu kwa mtazamo na maamuzi yangu.
Nchi yetu na Katiba tuliyonayo inampa hayo mamlaka na nguvu za kufanya hivyo kama tulivyoona kwa mtangulizi wake (Magufuli). Tujiulize kwa nini asifanye hivyo?
Hapo utapata jibu moja kwamba Samia either ni mvivu asietaka kufuatilia mambo kwa karibu, au anapuuzwa na wasaidizi wake.
Kuhusu kupuuzwa na wasaidizi wake, kuna zile tetesi zilizoenea wakati wa kifo cha Magufuli, kwamba alikuwa akifichwa taarifa za msingi za kifo cha Magufuli na kuna mambo yaliyokuwa yakiendelea chini chini ili kumuondoa kwenye nafasi yake ya VP awekwe mwingine.
Hapa utapata picha kwamba, kama hawa waliokuwa wakimficha hizo taarifa bado wamemzunguka mpaka leo, basi tutegemee mabaya zaidi mbeleni, angetakiwa kuwaondoa hawa wote mapema alipoapishwa aweke watu wake afanye nao kazi.
Hilo la uvivu naliacha kila mmoja afikirie kwa namna yake, hasa akizingatia kule Samia alipotokea, tabia za watu wa kule, na mengineyo.