Hivyo vitu hucheza na fikra na hofu juu ya wajinga wanoamini amini uchawi una nguvu kuliko Mungu Muumba wa viumbe vyote.
Ukiwa na hofu ktk jatibu/changamoto yoyote ile na ukakosa uvumilivu ni lazima uangukie ktk mitego ya shetani.
Kikubwa hasa ni kutohusisha fikra zako kabisa na habari za kishirikina hata urogwe vipi we amini tu huko kurogwa kwako kutakuwa na mwisho wake na aliyekupatia pumzi ndiye mwenye mamlaka ya kuruhusu uondokwe na uhai lakini vinginevyo utadhoofika kipindi cha majaribu tu na utarudi ktk hali ya kawaida kiafya, kiakili, kimwili na kiroho/kiimani.
NB: HAKUNA KISICHOWEZEKANA KWA MUNGU LAKINI JARIBU HUWA CHACHU KWETU BINADAMU KUTUWEKA IMARA KIIMANI.