Aina za Pikipiki: Ipi "taste" yako kwa Matumizi Binafsi?

Aina za Pikipiki: Ipi "taste" yako kwa Matumizi Binafsi?

Wakuu.

Kwa wapenzi wa pikipiki kwa matumizi binafsi, unapendelea aina ipi? Au umewahi kumiliki aina ipi? Yepi mazuri na mabaya ya iyo aina? Ulinunua wapi na bei vipi?

Baadhi ya aina ambazo mimi nimekutana nazo na kua na experience nazo kidogo ni hizi chache:

Sport Bikes
Nazipenda muonekano wako, very aggressive na unavyoendesha unalala. Nilikua nayo CBR600RR ni nzuri lakini sishauri kwa mtu anaetaka first bike.

View attachment 3022494
Chagua yenye cc ndogo mfano Yamaha R15 (usimix na R1), KTM RC390

View attachment 3022495View attachment 3022497
Ukiweka na Akaprovic exhaust lazima mtaani wakuwekee kikao.

Ubaya wake ukiangusha mara moja tu ayo maplastic (fairings) yanapasuka, hapo kuyapata msala inabidi uagize or ndio uanze kuyaunga unga kama simtank lililotoboka.

Sport bikes nyingi tunauziana used hapa, kuna wahindi town wanaagiza nje na pia kama unaweza kufuata Zanzibar jambo jema.

Bei ni kuanzia Mil 3.5 used hadi 20+ kutegemeana na brand, engine size, mwaka nk.

View attachment 3022530
View attachment 3022531
Mfano hii nimeikuta inauzwa Mil 10. Sio mbaya ila pia ni bei ghali kama hauna mapenzi na pikipiki.

TVS hawa hawa wanaotengeneza izi pikipiki wana chuma kizuri sana kinaitea Apache RR-310, sema wanakibania kutuletea Tanzania.

View attachment 3022524
Nadhani kwa bei zao elekezi, tungefanikiwa kuendesha Sport bikes kwa chini ya Mil 6 mpyaa.

Naked Bikes
Hizi ni pacha wa sport bikes, ila zimekua zimeondolewa ayo maplastic ya pembeni.

Mfano, KTM RC390 naked wake ni KTM Duke 390.

View attachment 3022500
Honda yeye ana CB150R ni tamu sana hii chuma.
View attachment 3022501
Yamaha anakuaga na MT series nk.

Hizi tofauti na Sports bike, zenyewe unaendesha ukiwa wima kabisa. So, maumivu ya mgongo kwa safari ndefu hauwezi yasikia sana.

Hizi unaweza kununua Mpya, mfano TVS RTR 160 na 180 4V zilikua zinauzwa Mil 3.5 hapa hapa Tanzania, kama zinepanda sahivi zitakua Mil 4.5 hivi.

View attachment 3022527

Kwa muonekano sio haba, na ni nzuri pia ukichukulia zinatoka kwa reputable brand.

King Lion nae hayupo nyuma, ana vyuma vyake unaweza pata uka enjoy kipyaaa kabisa au used, kwa chini ya Mil 3.5 hivi.

View attachment 3022537View attachment 3022538

Sema ujinga wa baadhi ya brands mfano iyo juu, unakuta ni kaunga unga kanunua kutoka China yeye kaziita King Lion, ukiitani spare ndio utazijua rangi zote.

Dirt Bikes
Hivi vinakuaga na cc ndogo na ni kwaajili ya off-road na michezo ya ajabu ajabu.

View attachment 3022507
KTM kateka sana soko hapa kwa Enduro, SX na SX-F series. Hizi wengi wanazitumia kama second bike kwaajili ya off-road na kucheza na matope.

Yamaha na Honda pia wana dirty zao, imara na nzuri sana

View attachment 3022510

Hizi sio common kununua kwaajili ya trip ya mjini au kazini utaonekana wa ajabu labda mishe zako ziwe pori kwa pori. Pia sio common kipiga trip ndefu.

Used ni chini ya Mil 5 kwa brand za KTM na Yamaha ila kuna brand za kichina izo sina uzoefu.

Scooters
Hizi Scoter ni ndogo na slow, ni kwa misele ya mjini na siku hizi wakina mama wapambanaji wanazipigania sana.

View attachment 3022511
Kama mishe zako Kariakoo au mji uliojazana sana unaweza pambania haka. Mali safi sana.

Kwa wenyeji wa Zanzibar mashahidi kule ni moja ya usafiri maarufu sana unaotumiwa na wanaume kwa wanamama.

Nazo zipo za bei ndogo kuanzia Mil 2 na kwenda juu hadi 8 na zaidi.

Kama unapenda au una miliki pikipiki za matairi mawili au manne unaweza share experience.

Edit 1:

Standard Bikes


Hizi ni kundi la pikipiki za kawaida ambazo uwa tunapishana nazo kila siku, na zinatumiwa sana na maafisa usafirishaji (bodaboda).
View attachment 3023633

Unaweza kuzichanganya na naked bikes au na cáfe racer ila izi nyingi zinakua na cc ndogo 150 kushuka.

View attachment 3023634

Unavoendesha unakua umekaa wima, tofauti na sports ambazo unalala, na wengi wanashauri ziwe beginner bike.

View attachment 3023635
Mfano kwa Tanzania, Boxer BM-150, TVS, Kibao cha Mbuzi, Haojue, San LG nk.

Hizi pikipiki zilivyoshoot bei hakuna anaelewa. Zamani zilikua 1.6 hadi 1.8 millions, ila sahivi mpya nyingi ni Mil 2.5 hadi Mil 3.

Used zipo za kuanzia Laki 7 kuendelea, ila lazima zitakua na changamoto.

Touring/ Sport Touring Bikes.
Kama jina linavyosema, haya ni mapikipiki kwaajili ya masafa, na wote wawili wewe na abiria wako mkikaa mnakua comfortable tofauti na pikipiki zingine, kwahiyo mnaweza ata kusafiri distance kubwa.

View attachment 3023639

Nyingi zinakuaga na cc kubwa, fairings, tank kubwa za mafuta, vioo kwa mbele kupunguza madhara ya upepo na uzito wake unafika hadi kg 250 kuendelea.

View attachment 3023640
Bila kuona picha ya SanLG Uzi huu hauna manufaa yoyote kwangu
 
Kuna hizi ATV za Zforce zimeanza kujaa mjini,, hivi bei inakwendaje na ubora wake maana naona ni za China half ni automatic drive
 
Kuna hizi ATV za Zforce zimeanza kujaa mjini,, hivi bei inakwendaje na ubora wake maana naona ni za China half ni automatic drive
Kusema kweli ATV sijawahi zielewa. Naona zimekaa ki-sport jui like siwezi enda nayo baadhi ya sehemu.

Naona ni nzuri mtu anakua na means nyingine ya usafiri hafu ATV for fun.
 
Kama hizo sport bike ila zinakuwa na tyres nene kidogo kuliko kawaida, zinaendaje mkuu?
 
Mzunguko ktk engine huw una rotation zake sasa kwa upande wa 4 stroke ina maana kuna piston 4 zinazojitegemea ili kutoa power stroke iliyokamili.
Hapana mkui inaweza ikawa na single piston na inaenda 4 stroke kwa maana ya mizunguko miine . 1. Kuingiza hewa na mafuta {intake)
2. Compession kuya bana ule mchanganyiko wa hewa na mafu
3. Power sroke hapa yakishwa banwa heat na energy inaongezeka sparkplaga inatoa cheche mlipuko unagokea na unasukuma piston na kitu kinasepa
4. Exhaust ule uchafu unatolewa sasa kupitia exhaust
 
MC0052_960b0e.jpg

Mjini unatamba na chuma ya namna hii. Toleo la miaka ya 90 ila hadi leo lina heshima kubwa.

Shida yake ni kwamba lina kelele sana hili dubwana.
 
But I prefer 2-stroke kutokana na POWER yake.. ukigusa kdg tu tyr ishanyanyuka. Kama ni mtu wa michezo inafaa sana.

Hakuna tope, mlima, mchanga wala taka taka yoyote itakayokuzuia.

Na kama mtaalam wa Wheelie ile inakubal vzr sana power wheelie (hugusi clutch at all) ni wese jingi tyre unaliona linaelea..
Hizo ukiendesha unanuka moshi hatari
 
Sorry tupe experience Yako ni safari gani ndefu ulisafiri kwa pkpk gan na km ngap kwa mda gan
Sorry nilichelewa kuona hii.

Mimi nilikua na Honda CBR 650R ya 2014 (hii ni cc 650), hii nimezunguka nayo kiasi.

Ingawa sio mtu wa maspeed, tulijiunga na wadau (Wadau wa Hot Bikes in Dar WA Group) kwenda Lushoto.

Mimi huyo tukakutana Mlimani, tunapitia Bagamoyo then Tanga to Lushoto.

Ubaya wa CBR ni Sport bike, unavoendesha unalala. Kwa safari fupi it was funny ila safari ndefu ni mateso.

Niliishia Msata, nikarudi Chalinze safari ikaisha iyo.
 
Back
Top Bottom