Aina za wanawake wanaodumu kwenye ndoa Tanzania

Aina za wanawake wanaodumu kwenye ndoa Tanzania

Mi mmasai bana nikujivunia umasai ni fahari yangu.
Ni kabila ile ingine imeshashindwa kudumisha mila
 
Binafsi ninakubali utafiti huu. Mana katika kutafuta wife material kutokana na social background priority Yangu ilikuwa ni mkurya,mmasai na Msukuma. Nilidate na Msukuma nikaangukia kwa mkurya. Hayo wengine ni kuwasifia tu na kuwatafuna na kusepa ila ukweli naujua mwenyewe.
Kuna jamii chache zinazojua mana ya ndoa tukubaliane nalo.na pia kipimo kizuri ukitaka kujua kama kabla hilo ni zuri angalia kama wanaume Wa hilo kabila wanaoa wadada wao I.e mfano je muha anapenda kumuoa muha mwenzako ama anakimbilia jamii zingine. Hapo utawajua kama wazuri mana kwanza wao kwa wao wanajuana tabia zao kuliko wewe Wa kuja.

Binafsi huwa nashauri makabila haya yanafaa kutafuta wife material mmasai,mkurya,msukuma , muha ,haya makabila huwezi achwa ama kudharauliwa kisa umefulia. Wanakomaa ama wanavumilia halo zote za majira ya mwaka.
 
Kwa kuwa makabila yapo zaidi ya 120 Tanzania, basi yalojitoteza hapo yote ni bora bila kujali ukubwa wa asilimia ambazo kimsingi haziakisi kabila jingine bali lilelile.

Anyway, tuliopo kwenye ndoa tunajua mengi na kwamba takwimu hizo mbali na elimu ilotolewa na mtoa mada, hazina uhalisia wowote. Mi nilioa mwanamke niliyemtoa bikira nikiamini nimepata chagua sahihi kwa mujibu wa imani ya jamii kuwahusu wenye bikira, bado najuta why I got married to her. Ndoa za sasa ni kizungumkuti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi nisiye na kabila
Utafiti feki huu wala usiwe na wasiwasi. Nina wasiwasi hata sampling, Tanzania ina makabila zaidi ya 120. Je utafiti uliyahusisha yote na idadi sawa ya couples kutoka kila kabila? Na hakuna waliokufa ndani ya muda wa utafiti?
 
Kwa kuwa makabila yapo zaidi ya 120 Tanzania, basi yalojitoteza hapo yote ni bora bila kujali ukubwa wa asilimia ambazo kimsingi haziakisi kabila jingine bali lilelile.

Anyway, tuliopo kwenye ndoa tunajua mengi na kwamba takwimu hizo mbali na elimu ilotolewa na mtoa mada, hazina uhalisia wowote. Mi nilioa mwanamke niliyemtoa bikira nikiamini nimepata chagua sahihi kwa mujibu wa imani ya jamii kuwahusu wenye bikira, bado najuta why I got married to her. Ndoa za sasa ni kizungumkuti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya uliyoyasema ndiyo ukweli wenyewe ambao inabidi kila tafiti inayohusu ndoa iutumie kama concluding remarks. Siyo mbwembwe kama hizi za eti wanawake wa kabila, au aina fulani wanadumu kwenye ndoa, uongo mtu. Watu wa NGOs nyingi na baadhi ya academicians kama kitila mkumbo wa wizara ya maji ndiyo njia zao za kujipatia fedha au kupanda vyeo vya kitaaluma kwa kufanya utafiti feki na kuandika machapisho feki yasiyokuwa ya uhalisia na hayana maana yoyote kwenye jamii.
 
Ndoa ya wazee wangu haikuwa ya kijijini,
Haikuwa ya kimila,
Kabila langu hapo halipo ila wazee wangu huu Ni mwaka wa 40, mpaka wanaanza kufanana, ndoa ukiipatia Raha Sana asikwambie mtu, ila ukiikosea utajuta kuzaliwa,

Rudia tena utafiti wako.
 
Hasara za kula makande usiku, mnaanza tafiti nyepesi nyepesi tu kisa kuna mdada kabila fulani kakuzingua unaamua kabila lake ulitoe.
 
Tz kuna makabila120+ ,sasa hiyo sample size yako naona kama siyo representative
 
Mama mkwe wangu anasema wazazi wake walimuita jioni kuwa kuna kijana anataka kukuoa, kesho saa nne asubuhi mtakutana nae kanisani kama umempenda mtaandikisha ndoa.
Kesho yake asubuhi shangazi yake na mama yake walimsaidia kujiremba, alitolewa nguo na viatu. Wakamsindikiza mpaka kanisani.

Baada ya kuandikisha ndoa alionana na mchumba siku ya harusi. Ndoa ina miaka 50+
 
Mama mkwe wangu anasema wazazi wake walimuita jioni kuwa kuna kijana anataka kunioa, kesho saa nne asubuhi mtakutana nae kanisani kama umempenda mtaandikisha ndoa.
Kesho yake asubuhi shangazi yake na mama yake walimsaidia kujiremba, alitokewa nguo na viatu. Wakamsindikiza mpaka kanisani.

Baada ya kuandikisha ndoa alionana na mchumba siku ya harusi. Ndoa ina miaka 50+
Hawajaliwa mtoto wa kike Sky...

Maana anakaexperience kidogo kuliko kukutana na ambaye baba alilala na mama hata hakumbuki kama alilala nae.
 
Back
Top Bottom