Air Tanzania (ATCL) yasitisha safari za Ndege kwenda Mumbai India

Air Tanzania (ATCL) yasitisha safari za Ndege kwenda Mumbai India

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesitisha Safari zake kwenda Mumbai nchini India kuanzia leo Mei 4 kutokana na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Corona.

Abiria wote walioathiriwa na uamuzi huu watarudishiwa gharama zao za Safari.

INDIA: VISA VYAFIKIA MILIONI 20, UPATIKANAJI OXYGEN BADO CHANGAMOTO.

Hospitali zaomba misaada huku Jeshi likitakiwa kusaidia kukabiliana na mlipuko.

Wataalamu waonya idadi halisi za visa na vifo inaweza kuwa kubwa kuliko inavyoripotiwa.

Soma India: Maambukizi ya Corona yafikia Milioni 20

IMG_20210504_202809_684.jpg

66131FF5-0263-47D5-86EA-53853C9882A8.jpeg
 
Tuchukue tahadhari, usalama wa maisha yako huanza na wewe. Tusijisahau sana. Nawaza, hivi chanjo inayopigiwa chapuo na kuwa imeshaanza kutumika imetoa matokeo chanya? Au bado CORONA imedinda tu? Watuletee matokeo ya chanjo km vile ASTRAZENECA, SPUTNIK V, NOVAVAX etc etc.
 
Hivi wale wapigania lagacy wako wapi?

Siku hizi wamepungua kasi kabisa.
 
Tuchukue tahadhari, usalama wa maisha yako huanza na wewe. Tusijisahau sana. Nawaza, hivi chanjo inayopigiwa chapuo na kuwa imeshaanza kutumika imetoa matokeo chanya? Au bado CORONA imedinda tu? Watuletee matokeo ya chanjo km vile ASTRAZENECA, SPUTNIK V, NOVAVAX etc etc.
Chanjo ya PFIZER imepunguza sana mzigo wa UVIKO Uingereza.

Utafiti uliohusisha watu 170,000 baada ya kupata chanjo umeonyesha idadi ya wagonjwa kupungua kwa asilimia 75 kwa watu wenye umri kati ya miaka 80 hadi 83 ndani ya siku 35 hadi 41 baada ya kupata dozi ya kwanza.
Kasi ya maambukizi imepungua kwa asilimia 70. Idadi ya waathirika imeshuka kutoka asilimia 15.3 hadi 4.6 kwa watu 100,000 waliopimwa.

CHANZO
telegraph.co.uk April 14 2021
11:27 PM
 
Back
Top Bottom