Air Tanzania (ATCL) yasitisha safari za Ndege kwenda Mumbai India

Air Tanzania (ATCL) yasitisha safari za Ndege kwenda Mumbai India

Tuchukue tahadhari, usalama wa maisha yako huanza na wewe. Tusijisahau sana. Nawaza, hivi chanjo inayopigiwa chapuo na kuwa imeshaanza kutumika imetoa matokeo chanya? Au bado CORONA imedinda tu? Watuletee matokeo ya chanjo km vile ASTRAZENECA, SPUTNIK V, NOVAVAX etc etc.
Tumuulize Slow Slow, alituambia kwamba ameiambia Corona ikae nasi kwa adabu.
 
Dar es Salaam. Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kusitisha safari zake kwenda nchini India ambako vifo na maambukizo ya corona yanazidi kuongezeka.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji na ofisa mtendaji mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi inasema safari hizo zimesitishwa kuanzia leo, Mei 4.

“ATCL itaondoa faini zote kutokana namabadiliko haya, itatoa tiketi nyingine au kuwarudishia nauli zao abiria waliokuwa wamekata tiketi,” amesema Matindi.

Ili kupata ufafanuzi zaidi, Matindi amewataka abiria waliokata tiketi kupiga namba O800110045 bure.

Taarifa nchini India zinasema leo pekee, maambukizo mapya 357,229 na kufanya jumla kuwa zaidi ya milioni mbili. Kwa idadi hiyo, India inakuwa miongoni mwa mataifa yenye maambukizo mengi zaidi duniani.

Mpaka sasa ni Marekani pekee yenye idadi kubwa, zaidi ya maambukizo milioni tatu yaliyotokea kabla ya kuanza kutolewa kwa chanjo na Brazil inashika nafasi ya tatu ikiwa na zaidi ya maambukizo milioni 1.5 yaliyothibitika.

Mpaka sasa, Serikali ya India imeshatoa chanjo kwa zaidi ya watu milioni 16.69 bure huku dozi milioni 7.5 zikiwa zinaendelea kutolewa. Taifa hilo lenye watu bilioni 1.4 ni la pili kwa idadi kubwa duniani likiwa nyuma ya China.

20210504_225731.jpg
 
Nahisi tumeshachelewa.....kwa nini kulikuwa na kigugumizi ?......very sad indeed.
Correct. These imbecile have all along been going to fetch the COVID 19 new/deadly variant from India! So sad!
 
Hii ni hatua njema hata hivyo haitoshi.

Pole pole tutafika.

Usafiri wote wa anga India na sisi unapaswa kusimama.

Waliopita India siku za karibuni tunapaswa kuwakodolea macho zaidi.
 
Nchi hii bwana kila mtu mjuaji.

Tuliamishwa na wapiga kelele humu jf eti ndege zetu kubwa zote zimepaki tu JKIA kwa sababu eti hazikuwa na pa kwenda jambo ambalo halikuwa kweli.

Sasa ajabu ya karne walewale tena waliotoa madai hayo ndiwo haohao wanaoshinikiza Air Tanzania isitishe safari zake huko India 😂!

Nchi hii aliyeturoga huenda ni bibi yangu.
 
Vijana wa CCM na CHADEMA mimi siwawezi kwa kweli. Bora nibaki bila kuwa mwanasiasa hivi hivi.
 
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kusitisha safari zake kwenda nchini India ambako vifo na maambukizo ya corona yanazidi kuongezeka.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji na ofisa mtendaji mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi inasema safari hizo zimesitishwa kuanzia jana, Mei 4.

“ATCL itaondoa faini zote kutokana namabadiliko haya, itatoa tiketi nyingine au kuwarudishia nauli zao abiria waliokuwa wamekata tiketi,” Matindi.

WhatsApp-Image-2021-05-04-at-20.55.03.jpeg


Credits: millardayo.com
 
Back
Top Bottom