Hela inayopotea ni yetu sote. Siyo hela ya Magufuli au CCM.
Rais Magufuli, arudi nyuma mpaka mambo yalipoharibikia. Aliunganishe Taifa. Katika umoja na maelewano ya kitaifa, hata mkulima anaweza kushaurika, anaweza kutupatia nafuu ya deni, na anaweza kukubali kulipwa kidogo kidogo. Na ndege zikaendelea kuruka bila wasiwasi wowote. Hiyo inaweza kufanyika pia kwa wadai wengine.
Bila hivyo, Rais Magufuli atapambana sana lakini hatafanikiwa hata kimoja. Kila siku atazidi kudidimia katika mipango yake. Kwa sasa kuna mambo kibao hayaendi (hata kabla ya Covid 19):
1) ukuuaji wa uralii umeshuka kutoka 15% mpaka 3.6%
2) Ukuaji wa uwekezaji umeahuka toka 28% mpaka 4%
3) Thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo yameshuka kwa 50%
4) Makusanyo ya kodi hayaongezeki pamoja na kuchukua vyanzo vote vya mapato vya halmashauri, miji na majiji
5) Misaada kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa imeshuka kwa zaidi ya 60%
Wakati huo huo kuna sauti nyingi toka jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali.
1) Mahusiano ya kimataifa yamezorota kiasi cha kunyoshewa vidole na taasisi mbalimbali kutokana na kutozingatia haki za binadamu, uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, utawala wa sheria, chaguzi za kidemokrasia, misingi ya demokrasia ya vyama vingi, sheria mbovu zinazodidimiza misingi ya uwazi na utawala bora. Haya yote yameifanya Serikali ya sasa kuonekana ni ya ajabu kwa vile inalipeleka taifa gizani badala ya kulipeleka kwenye mwanga.
2) Mauaji, upotezaji na mashambulio ya watu wenye mawazo pinzani dhidi ya serikali au Rais. Vitendo hivi vya hovyo vimeifanya Serikali kuwa unpopular kwa kila genuine person, bila ya kujali mtu huyo ana mlengo gani wa kisiasa.
3) Uanzishaji wa kundi la kijambazi la 'watu wasiojulikana' kwa nia ya kudhibiti wasiokuwa tayari kuisifia serikali, n.k. Kundi hili limeharibu kabisa image ya serikali na Rais.
Nadhani Rais anajua wazi kuwa njia zilizofikiriwa kuwa zingeisaidia Serikali yake kupata mafanikio, hazifanyi kazi. Hivyo ni vema kurudi nyuma na kutafakari, na kisha kutafuta mbinu mpya kwa kutumia mawazo mapya kutoka kwa watu wapya. Bila hivyo, atakuja kutoka Ikulu akiwa ameinamisha kichwa kwa sababu ya kukosa cha kujivunia kama alama nzuri aliyoiacha.
Sent using
Jamii Forums mobile app