Airtel inazidi kutanua soko la Unlimited internet, Vodacom na Tigo wakiendelea kushupaza shingo watastuka soko lishamezwa

Airtel inazidi kutanua soko la Unlimited internet, Vodacom na Tigo wakiendelea kushupaza shingo watastuka soko lishamezwa

mkuu ni wifi au fiber? kama ni fiber huku nakoishi natmia ya tigo ya speed 20 mbs kwa 55000 sasa nitahama nahamia mapinga hakuna fiber kabisa nilidhani ni router nije niichukue.

Yes ni unlimited fiber internet ya Halotel, ina router ya Halotel ZTE na fiber yake ina wire zile nyembamba za fiber wametandaza, so wakikuunga unapata wifi ya kutumia, ndio maana ina speed sana
 
Zinanunuliwa na wachache sana. Na hao wanaonunua zinawashinda wanarudi tena kwenye mabando ya siku na wiki.

Tatizo mnafikiri Tanzania ni hapo M/City na maduka makubwa zinazouzwa hizo router

Watanzania wengi kwanza hawajui hata router ni nini.

Hili taifa bado lina umasikini mkubwa sana wa kipato cha mtu mmoja mmoja

Kweli Mtanzania wa kawaida atoe 250k au 110k kwa ajili ya intaneti? Tembeeni vijana mjionee uhalisi wa maisha ya Mtanzania
Mkuu nipo dodoma nao na hicho ninachokwambia nimekishuhudia huku. Anyway mambo yasiwe mengi...
 
Yes ni unlimited fiber internet ya Halotel, ina router ya Halotel ZTE na fiber yake ina wire zile nyembamba za fiber wametandaza, so wakikuunga unapata wifi ya kutumia, ndio maana ina speed sana
hii ni same kama nilyofunga hapa sema ya tigo. wanakupa router ambayo imeungwa kwenye waya wa fiber kwenye nguzo zao walizosambaza, hiyo router ina port moja ya ethernet, na inatoa wifi ya 2.4g na 5.g kwa pamoja, wewe mtumiaji ndiye utachagua wajiunga ipi.
Ila naona halotel hapo kwako ina ping nzuri kinoma
 
sasa unaniuliza hili swali unadhani nimefanya research naweza kukupa exact number? Ila mimi kila lodge ninayoenda hapa dar katika harakati za uzinifu nakuta wifi tena ni zile za 25000-35000, napoishi, nikienda sokoni kwenye saluni za kike na kiume kuna wifi, tena waameweka hadi vile vispka. Tunatoa huduma ya kunyoa nywele na mteja atapata free wifi.... Rafk zangu ninaozunguka nao wanatumia hizi router, mimi mwenyewe nimefnga fiber ila nahama soon nitanunua router maana nakohamia hakuna fiber.
Nakubaliana na wewe kuwa si watanzania wengi, ila vinanunulika sana na watu wanavitumia.
Kama DSTV ina wateja 180k na bado ina survive, basi bila shaka wakiwa na wateja 200k nao watasurvive. Kabla ya kufunga wifi, nilienda chukua router pale kibo complex, wakaniambia mzigo umeisha nisubiri.
Kila lodge unayoenda acha kutupanga woye tunaishi Dar lodge zenye hiyo huduma ni chache mno.
 
Kila lodge unayoenda acha kutupanga woye tunaishi Dar lodge zenye hiyo huduma ni chache mno.
Kwani mimi na wewe tunaendaga lodge moja mkuu? Mimi lodge zote ninazoenda zina wifi, unawapa device yako wanakuingizia password.
Pia na sehemu kibao zinazotoa huduma za Airbnb zina wifi.
 
Nenda kwenye duka la halotel watakusajilia maana laini ya kawaida haikubali. Hata namba zake ni tofauti kabisa, zinaanza na 300 na siyo 062 kama hizi za kawaida...
Lakini ukiweka ifanane na ya sasa ya kawaida kwenye hiyo ya 300 itakubali
 
Lakini ukiweka ifanane na ya sasa ya kawaida kwenye hiyo ya 300 itakubali
Haikubali, na jinsi inavyosajiliwa inasajiliwa kwenye laini yako ya halotel, inakuwa kama ni laini msaidizi wa laini yako kuu ya halotel, sijui umenielewa hapo mkuu...?😀
 
Hakuna kitu kama hicho, tembea Tanzania ujionee jinsi kauli yako ni uongo mtupu. Kati ya Watanzania 10 ni wangapi wana router?
Yaani we unataka kusemaje, watu wasiuze routers kwa kuwa kuna kundi la watu masikini..!?

Halafu ambacho hukijui (au unakijua ila unajipa uchizi usiokuwa nao) pamoja na uwepo wa routers hizo bando za buku buku zenu bado zipo... router sio ya kila mtu, sasa wewe mtu huna kazi ya kukuhitajia mtandao, huna hata account ya netlix ili tuseme japo unahitaji router kwa ajili ya movies...router ya kazi gani.

Ila kuna watu wanapongeza saana huu uradi wa unlimited unawafaa kwenye kazi zao, wewe wa buku buku endelea na buku buku zako hakuna atakaekuzuia kutumia buku yako.
 
Does it mean inakuwa fixed kwa mwezi au ni unlimited
Kwa jinsi walivyoniambia ni kwa mwezi, ila kama ikitokea ukanunua GB 210 ila ukatumia labda tuseme GB 80, ukinunua bado jipya kabla ya muda wa kifurushi kuisha kufika zile data zilizosalia (GB 130) utahama nazo kwenda mwezi unaofuata. Siyo unlimited...
 
KUna vitu muwe mnashirikisha akili.

Hivi ni Watanzania wangapi wanaweza kuafford hizo huduma?

Buku buku ndio uwezo wa Watanzania 99.9%
Unapata buku unaunga Sasa hivi. Baada ya muda labda jioni unapata buku unaunga Tena. Aliyeshiba haezi elewa....

Ndio maana mtu anamwambia mwezie nunua Michele uweke ndani, kwa mama ntilie unapoteza hela....Sasa ukiangalia huwezi pata cash ya kununua kilo 10 kwa mara Moja ila kila siku unaeza pata buku ya kula wali maharage kwa mama ntilie....... So........
 
Kwa jinsi walivyoniambia ni kwa mwezi, ila kama ikitokea ukanunua GB 210 ila ukatumia labda tuseme GB 80, ukinunua bado jipya kabla ya muda wa kifurushi kuisha kufika zile data zilizosalia (GB 130) utahama nazo kwenda mwezi unaofuata. Siyo unlimited...
Router wanakupa bure ama unainunua mkuu..


Halafu wana limited ya data ambazo ukizivula speed inapungua?
 
Router wanakupa bure ama unainunua mkuu..


Halafu wana limited ya data ambazo ukizivula speed inapungua?
Device unanunua, wana MiFi za 50k na 150k. But wakati mimi naenda kununua nilienda na 50k kwa ajili ya device ila nikakuta device za 50k zimeisha so nikaacha kununua device, nikachukua tu laini now nimeweka hiyo laini kwenye simu.

Kuhusu kupunguza speed kwa uzoefu wangu sijakutana na hiyo hali. Na nafikiri kwa kuwa wanakuuzia data ambayo ni limited mfano 210GB, sidhani kama watakuwa wanahitaji kulimit speed. Tangu nimeenza kutumia naona iko sawa tu. Kwa mfano wa sasa nimetest speed ni 16mbps. Siyo kubwa ila kwa matumizi ya kawaida kustreem iko poa tu.
 
Halotel Fiber Home Wifi is the best internet, router bure na vifurushi vyao inaanzia 70k kwa mwezi na speed 20mb/s hicho ndio kifurushi cha chini na 95k kwa speed ya 40mb/s kwa mwezi na hicho kinatosha sana unlimited, Halotel wamekamata Dar sio mchezo
Hio halotel fibre nzuri sana
 
Hizo fiber kwa sisi wa nyumba za kupanga bado haziko feasible kwetu, leo tupo kesho hatupo.

Siku wakianza kuwezesha na line zao ziwe na access na hizo unlimited watatukamata wengi sana..
Ndio hata mimi nimeona hilo likiwezeshwa kwa line itakuwa magoli sana. Imagine unashinda kazini umelipia internet atumie beki 3 tu labda. Ilitakiwa wawezeshe na line ya simu iweze kutumia unlimited iliolipiwa nyumbani at the same speed
 
Back
Top Bottom