Airtel wanayajua mahitaji muhimu kwa binadamu kwa watu wa waliokumbwa na Maafa Hanang?

Airtel wanayajua mahitaji muhimu kwa binadamu kwa watu wa waliokumbwa na Maafa Hanang?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Nimesoma mahali kwamba Airtel inasambaza bure Internet kule eneo la maafa, hiki ni kichekesho kikubwa sana.

kwanza nani asie jua speed ya Internet ya Airtel? Pili je hizo ni moja ya Needs za watu walio kumbwa na maafa pale? Watu wanahitaji Mahema, Maji, madawa, nguo. Airtel wao wanaona Internet ndii basic needs pale?

Hii ni Marketing strategies ya kijinga sana, kama hawawezi toa Basic needs pale kama Chakula, madawa, mahema, na nguo waache ujinga.

Hawa airtel wana akili sawa na watawala, yaani wote wanafanana akili na jinsi ya kuwaza si bure hata mtandani wao umekaaa kima gumashi gumashi sana.

FB_IMG_1701750182016.jpg
 
Airtel imetoa GB 2 na Dk. 100, kwa waathirika Hanang kwa siku 3 mfululizo.

Maana yake kwa mtu mmoja wametoa Tsh. 9000, idadi ya watu Ni 300,000+, hii ina maana;

300,000x 9000= 270,000,000/-

Kwanini hii pesa wasingeipeleka kwa wahusika?

Hii haiingii akilini kabisa!
 
Airtel imetoa GB 2 NA DK 100, KWA WAATHIRIKA HANANG Kwa siku 3 mfululizo.

Mwana yake kwa mtu mmoja wametoa tshs 9000,

Idadi ya watu Ni 300,000 plus

300,000x 9000= 270,000,000

Kwanini hii pesa wasingeipeleka kwa wahusika!

Hii ,haiingii akilini kabisa
sasa wakiwapa wahusika kila mhusika akipata 9,000 watakuwa wametoa nini.
 
Airtel imetoa GB 2 na Dk. 100, kwa waathirika Hanang kwa siku 3 mfululizo.

Maana yake kwa mtu mmoja wametoa Tsh. 9000, idadi ya watu Ni 300,000+, hii ina maana;

300,000x 9000= 270,000,000/-

Kwanini hii pesa wasingeipeleka kwa wahusika?

Hii haiingii akilini kabisa!


Hujui Biashara wewe, hiyo ni service siyo cash. And nikueleze tu hata wasingetoa, pengine hiyo wasingeipata.

Ni sawa na useme, haya maji yanayomwagika kwenye leakage ya idara ya Maji, si nikachukue cash? Ile sio cash.
 
Back
Top Bottom