Airtel wanayajua mahitaji muhimu kwa binadamu kwa watu wa waliokumbwa na Maafa Hanang?

Nyinyi ngumbaru ni lini mliona Airtel inalima magimbi kwamba ibebe magunia iwapelekee waathirika? Mnataka Airtel ipeleke nyama ya sungura kwani hiyo ni kampuni ya ufugaji?

Airtel imetoa ilichonacho, na nyinyi wenye lawama peleka lawama kule tuone zitasaidia kitu gani. Na bado Airtel imetoa fedha ili zikasaidie kununua mahitaji, mna akili za bata kudhani Airtel itatoka kukusanya magunia ya maharage kupelekea wananchi.

Kampeni ya #TupoPamojaNanyi kupitia TTCL, Airtel, Vodacom, Halotel na Tigo imechangia fedha za kutoa hayo magunia mnayotaka.

Kwanza sio lazima kulazimisha msaada wa kampuni binafsi.
Pili, jifunzeni kupokea misaada kama haina madhara na mzingatie anayetoa msaada hali yake, huwezi taka mfugaji akikuchangia mfugo wake usilazimishe akuletee furniture kutoka kwa seremala na seremala vilevile usilazimishe akuletee mfugo. Huo ni upumbavu.
Tatu, muache ushamba mawasiliano ni suala muhimu kwenye ulimwengu huu. Kuna watu wanataka kujua hali ya familia zao, kuna watu wamepotea taarifa zinazidi kutolewa, kuna misaada inaletwa watu wapewe taarifa. Hayo yote yatasaidiwa na mawasiliano iwe simu ama redio stations za kule. Nyinyi akili zimekalia kwenye nyanya na ugali.
 
Nimesoma mahali kwamba Airtel inasambaza bure Internet kule eneo la maafa, hiki ni kichekesho kikubwa sana.

kwanza nani asie jua speed ya Internet ya Airtel? Pili je hizo ni moja ya Needs za watu walio kumbwa na maafa pale? Watu wanahitaji Mahema, Maji, madawa, nguo. Airtel wao wanaona Internet ndii basic needs pale?

Hii ni Marketing strategies ya kijinga sana, kama hawawezi toa Basic needs pale kama Chakula, madawa, mahema, na nguo waache ujinga.

Hawa airtel wana akili sawa na watawala, yaani wote wanafanana akili na jinsi ya kuwaza si bure hata mtandani wao umekaaa kima gumashi gumashi sana.

Umetumia sana hisia kuliko akili...Airtel imeamua kusaidia kutokana na huduma inayotoa...Chakula watoe wengine kina Azam kama vipi.
 
Kwa hiyoo wameona huo ndo msaada katika kipindi kigumu kama hichii labda waongeze na msaada wa vitu vingine ila sio uu uhunii
 
Nyinyi ngumbaru ni lini mliona Airtel inalima magimbi kwamba ibebe magunia iwapelekee waathirika? Mnataka Airtel ipeleke nyama ya sungura kwani hiyo ni kampuni ya ufugaji?

Airtel imetoa ilichonacho, na nyinyi wenye lawama peleka lawama kule tuone zitasaidia kitu gani. Na bado Airtel imetoa fedha ili zikasaidie kununua mahitaji, mna akili za bata kudhani Airtel itatoka kukusanya magunia ya maharage kupelekea wananchi.

Kampeni ya #TupoPamojaNanyi kupitia TTCL, Airtel, Vodacom, Halotel na Tigo imechangia fedha za kutoa hayo magunia mnayotaka.

Kwanza sio lazima kulazimisha msaada wa kampuni binafsi.
Pili, jifunzeni kupokea misaada kama haina madhara na mzingatie anayetoa msaada hali yake, huwezi taka mfugaji akikuchangia mfugo wake usilazimishe akuletee furniture kutoka kwa seremala na seremala vilevile usilazimishe akuletee mfugo. Huo ni upumbavu.
Tatu, muache ushamba mawasiliano ni suala muhimu kwenye ulimwengu huu. Kuna watu wanataka kujua hali ya familia zao, kuna watu wamepotea taarifa zinazidi kutolewa, kuna misaada inaletwa watu wapewe taarifa. Hayo yote yatasaidiwa na mawasiliano iwe simu ama redio stations za kule. Nyinyi akili zimekalia kwenye nyanya na ugali.
Nani ana huo mda wa kutumia hizo dakika na mb kwa wale walio athirika kijana??? nyumba imebomoka airtel wakikupa mb za bure na dakika inakusaidia nini??? airtel ni shirika kubwa waache janja janjaa watoe msaada unaoelewekaaa sio hii promotion ya ovyoo wanayotoa wanataka watu wakatafute line za airtel kipindi hiki cha matatizo au wameambiwa hanang kila mtu ana line ya airtel???
 
Nimesoma mahali kwamba Airtel inasambaza bure Internet kule eneo la maafa, hiki ni kichekesho kikubwa sana.

kwanza nani asie jua speed ya Internet ya Airtel? Pili je hizo ni moja ya Needs za watu walio kumbwa na maafa pale? Watu wanahitaji Mahema, Maji, madawa, nguo. Airtel wao wanaona Internet ndii basic needs pale?

Hii ni Marketing strategies ya kijinga sana, kama hawawezi toa Basic needs pale kama Chakula, madawa, mahema, na nguo waache ujinga.

Hawa airtel wana akili sawa na watawala, yaani wote wanafanana akili na jinsi ya kuwaza si bure hata mtandani wao umekaaa kima gumashi gumashi sana.

Another one from Airtel. Hapo kimsingi wameonyesha kiwango chao cha ujinga
 
Povu la nini? Yoyote anaweza kutoa anachoweza. Mawasiliano nayo ni muhimu sana... itasaidia hats wahanga kuwasiliana kirahisi na ndugu na jamaa wengine...
Atleast ingekuwa dakika za kupiga na sms sio internet pekee maana hapo amewatenga wanaomiliki viswaswadu
 
Kuna clip Moja niliona Bahati mbaya siku-download ...

Jamaa alikuwa na iphone na pizza akaenda Kwa jamaa (jobless) alikuwa amekaa sehemu kama wale ombaomba wetu.
Yule jamaa akaambiwa chukua kimoja hapa. Chapu akachukua pizza [emoji487] katika kumuuliza maswali akajibu nitachukuaje simu Ili Hali Nina njaa? Ukweli Nina njaa lakni chakula ndo nahitaji sana Kwa Sasa!

Kuna funzo kubwa sana hapa
 
Mkuu hapa Kila mtu anatoa maoni yake tu Wala sio ubabe Wala nini ulichokizungumza ni sawa hata Mimi sipingi! Umewasiliana na watu wa huko lkn? Maana hata kuchaji simu zao wanaenda sehemu nyingine Tena mara Moja Moja! Kipi Cha mhimu Hadi hapo? Mb unazo za kutosha dk za kutosha ila simu Haina chaji Ina umuhimu gani
Airtel ndio wakajenge miundombinu ya umeme? Ndio wakasimike nguzo zilizoanguka?
Ukweli kwamba hii Nchi inawatu wengi sana wasio jielewa! Mtu anakwambia FAO ndo walete chakula! Inahuzunisha sana. Kwan Airtel atapata dhambi Gani kuleta hata magodoro pale watu wanalala ovyo? Au hata mahema tu!
Je wakileta magodoro na mahena mahitaji yote yatakamilika 100%? Sivyo.
Sasa kama hayatokamilika ikakosekana hitaji lolote utalalamikia tena Airtel? Uko hata na hisa 1 pale mpaka kudictate watoe mahema na magodoro? Na hizo fedha walizotoa haziwezi nunua hayo mahema na magodoro?

Kama magodoro hamna, serikali inayokusanya kodi na ambayo ina wajibu direct kwa mwananchi inafanya nini muda wote huu. Ni lini ulisikia Airtel wana kitengo cha dharula kutenga bajeti ya mahitaji yote ya wahanga wa majanga nchi hii?

Na je, Airtel ndio wana wajibu wa kujua kipi kinahitajika na kipi kimepatikana? Unaweza kusema hapa yanahitajika magodoro mangapi na mahema mangapi? Airtel hizo data wanazikusanya kutoka wapi wakati ziko serikalini?

Makampuni ya wawekezaji hayafanyi maamuzi kimatakomatako kama mnavyodhani mkishakunywa wanzuki. Hapo zimekusanywa fedha, data zipo serikali na taasisi zake husika na mashirika husika yanajua nini kinatakiwa. Kampuni nyinginezo ambazo sio experts kwenye hili suala zinaweza toa hela ikanunua kinachohitajika. Wewe kama unaona wanahitaji mapera wapelekee ila Airtel haiwezi fanya hivyo.
 
Nani ana huo mda wa kutumia hizo dakika na mb kwa wale walio athirika kijana??? nyumba imebomoka airtel wakikupa mb za bure na dakika inakusaidia nini??? airtel ni shirika kubwa waache janja janjaa watoe msaada unaoelewekaaa sio hii promotion ya ovyoo wanayotoa wanataka watu wakatafute line za airtel kipindi hiki cha matatizo au wameambiwa hanang kila mtu ana line ya airtel???
Ina maana hela waliyotoa hujaona? Ulitaka watoe nini hasa. Wametoa hela kwanza kabla ya kutoa hizo huduma za mawasiliano.
Ukiwa na msiba mfugaji akachangia pesa then akatoa mbuzi wa kuchinja utakasirika kwanini ametoa mnyama. Ulitaka mfugaji alete pombe.

Kwenye CSR wapi uliona kampuni inatoa msaada kimbumbumbu bila kutoa na huduma zake.
 
Kwa hiyoo wameona huo ndo msaada katika kipindi kigumu kama hichii labda waongeze na msaada wa vitu vingine ila sio uu uhunii
Wameshatoa msaada kabla ya huu. Ila kwa sababu hii ni third world country kila kitu ni lawama.
 
Ina maana hela waliyotoa hujaona? Ulitaka watoe nini hasa. Wametoa hela kwanza kabla ya kutoa hizo huduma za mawasiliano.
Ukiwa na msiba mfugaji akachangia pesa then akatoa mbuzi wa kuchinja utakasirika kwanini ametoa mnyama. Ulitaka mfugaji alete pombe.

Kwenye CSR wapi uliona kampuni inatoa msaada kimbumbumbu bila kutoa na huduma zake.
Kama wametoka Hela Sina neno nao
 
Back
Top Bottom