Airtel wanayajua mahitaji muhimu kwa binadamu kwa watu wa waliokumbwa na Maafa Hanang?


Hiyo pesa wangewanunulia vyakula na malazi
 
Wanajua kuna wale wachukua matukio wasio rasmi watarushiana video hivyo kwa wale ambao hawapo eneo la tukio wanajua ni kwa kiasi gani watu wameathirika. Misaada inakuja baada ya kuona hali halisi.
 
Acha hizo,,,wao wametoa moja ya mahitaji muhimu,,,”MAWASILIANO”..Wewe umetoa nini??!!
 
Kwa mnao jua naomba kueleweshwa internet itasaidiaje Kwa wahanga wa janga hili pale katesh manyara?

Kwanini wasitoe misaada kama chakula,vifaa vya matibabu,dawa na magodoro.kwanza pale watumiaji wengi ni hallotel na hiyo Airtel.Sasa pia sina hakika kama wote Wana smart phone (simu janja) ni wachache sana wenye smart.
 
Mimi ningewapongeza kama wangepeleka hata tani1 tu ya mahindi au maharage
Ningewaona wa maana kweli kweli
 
Internet siyo urgent need kwa sasa kwa watu wa Hanang!
Wewe ni mmoja wa vilaza na liability kwa Taifa kwa sasa!
Unavyowaza wewe ni kama Mimi hapa watu hawana umeme kule ushaharibika hata kuchaji simu ni shida wewe una amka tu unasema internet Bure Ili asilimia kubwa ya watu hata simu hawana. Safari Bado sana asee
 
Huwezi kujipangia Msaada!
Ni sawa hapa tunatoa maoni yetu kuwa wangeangalia vitu vya mhimu vinavyo hitajika Kwa Sasa hata kama wangetoa tani Moja ya unga wa ngano hakika wangefanya vyema sana.

Pia fikria umeme haupo pale Kwa Sasa miundombunu imeharibika sana hata kuchaji simu ni Kwa mbinde hata wenye Sola nao zimeharibiwa vilevile!

Kabula hujasema kitu fikiria Kwa undani zaidi Kuna chalii yangu hapo nangwa kaniambia hata mawasiliano Kwa Sasa ni shida!
 
Acha kubishana na mazombie
 
Internet siyo urgent need kwa sasa kwa watu wa Hanang!
Wewe ni mmoja wa vilaza na liability kwa Taifa kwa sasa!
Misaada yote inatakiwa, kila kampuni au mwenye uwezo atoe kwa field yake,

Mwalimu anaweza jitolea kufundisha bure watoto kwa sasa muda huu mambo yapo shaghala baghala, nesi atasaidia hospital,
Ma engeneer watajitolea ujenzi,
Wapish watapika
Watu wa electronics watatoa mawasiliano bure, watu wanahitaji kuongea na ndugu zao mbali, kuwathibitishia wapo salama ,


And btw, huo msaada wa haraka na muhimu idai serikali yako sio Airtel
 
Mkuu hapa Kila mtu anatoa maoni yake tu Wala sio ubabe Wala nini ulichokizungumza ni sawa hata Mimi sipingi! Umewasiliana na watu wa huko lkn? Maana hata kuchaji simu zao wanaenda sehemu nyingine Tena mara Moja Moja! Kipi Cha mhimu Hadi hapo? Mb unazo za kutosha dk za kutosha ila simu Haina chaji Ina umuhimu gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…