Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

Eeh hii sindio
bongo mzeebaba, unaweza ukauziwa dumu la Toyota oil ya kupima😂😂😂
Kumbe bei yake halisi ni 120,000?
Kwahiyo nitakua nimeuziwa diluted ama? Ngoja leo naenda kuonana na fundi wangu, nitam-bana kwelikweli!

Nitaleta mrejesho jioni hapahapa.
 
Hukupaswa kufanya kwa pamoja hivyo vyote, si lazima
 
Sema gearbox ukichakachua vimiminika majibu yanakuja fasta sana gear box hainaga hii toyota sijui hii audi huwa fasta tu inadanja
Kwahiyo mkuu nitakua nimeua gearbox ya babywoka yangu?
 
MREJESHO:

Jana nilienda kwa fundi wangu kunyoosha Oil Sample niligonga jiwe ikabonyea. Nimegundua ni kweli siku ile ya kwanza nilipigwa kipigo cha mbwa koko.


2. Oil Seal wamelamba 10K inauzwa
25K
Ulisema kweli aisee. Jana tumenunua Oil Seal nyingine kwa 25,000. Wala sijataka kumuuliza fundi kwa nini siku ile tulinunua 35,000.

3.Engine oil lazima wamekuwekea 20W 50 maana ndio cheap ni 35K wamelamba 10K

Nimeamini maneno yako bro. Baada ya kunyoosha Oil Sample ikabidi tuongeze Oil kama litre mbili hivi @5000 per litre. Nimekuta washaweka oil, nilienda kula. Nimepiga picha ya dumu. Fundi nimemuuliza anasema hii Oil inafaa kwa gari zote za diesel na petrol. Ni kweli?


Mwisho tulinunua Bearing moja (inayozungusha fan belt) ilikua imeisha halafu inapiga kelele. Nimetoa 25,000 sijui na penyewe nimepigwa maana ndio mara ya kwanza.
 
Hahahah umeamini sasa bwana mdogo. Hio bearing sijawahi badili ila yangu pia imeshaanza kelele baada ya mamvua mvua inabidi nikaibadilishe ila umenipa mwangaza walau nitajua jinsi ya kuwaingia mafundi. Naimani haitazidi 20K
 
Mwamba vipi oil ya injini ya diesel hyo au gari yako ya diesel
 
Awali ya yote nikupe pole kwa kupigwa...ila ndiyo maisha na ndiyo kujifunza...

Hiyo oil usiweke kwenye gari lako....Ni nzito sana na isitoshe ni recommended kwa diesel engine

Nunua 5w30 ya Total lita 4 ni kati ya 50k mpka 55k. Ni miongoni mwa oil nzuri ambazo bei yake ni ya wastani, siyo ghali wala siyo rahisi..

Ukiweka kama hii ninayotumia mimi ni nzuri zaidi...Total quartz..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi 10W 30 total wanayo
 
Mkuu hapo kwenye Riber charge ndio nini?[emoji1787]
Garage za chini ya muembe hizo. Halafu hiyo gari ulishatumia sana mpk ma mounting hayo unabadili basi ushapiga nayo mzigo sana.
Break BARD ndio sijaielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…