Kubali ukweli tu kwamba Kenya hamfanyi utafiti wa kina kabla ya kuchukua uamuzi ndiyo sababu mnapata matatizo ya kiuchumi, mfano mzuri ni kuanguka na kufilisika kwa KQ, bila kufanya utafiti na kudhani biashara itakua nzuri kama unavyofikiria wewe, Kenya Airways ilinunua na kukodi ndege nyingi kwa wakati mmoja, kinachotokea sasa wanapata hasara na ndege wanauza na kukodisha, kwa sasa hivi biashara dunia nzima imeshuka sana, shipping companies nyingi zimesimamisha meli zao na wanauza baadhi ya meli kama inavyofanya KQ, katika hali kama hiyo, sio kipindi sahihi kujenga bandari, ni bora kuboresha na kupanua iliyopo kama mlivyofanya ya Mombasa, mngesubiri kuona kama biashara itaboreka ndani ya kipindi cha miaka 5 hadi 10, kama ikiboreka ndiyo mjenge.
Tanzania baada ya kuona kwamba hali ya biashara sio nzuri, tumeamua kuboresha hizi bandari zetu 3 tulizonazo, kama biashara sio nzuri, sio busara kupanua biashara, endelea kuboresha na kuhakikisha uliyonayo haitetereki, kilichotokea kwa KQ, lazima kitatokea kwa Lamu port. Kwanini unasisitiza Ethiopia wakati nimekuambia wameshajenga reli wanatumia bandari ya Djibouti, acha kuchanganya kati ya Djibouti na Eritria, hizi ni nchi mbili tofauti, Addis na Djibouti ni karibu kuliko Lamu, ni Kama Kampala na Mombasa ilivyokaribu kuliko Kampala na Dar, kamwe haitowezekana Ethiopia kuacha kutumia reli yao ya umeme waliojenga kwa pesa yao, eti watumia usafiri wa barabara hadi Lamu, msipokua makini mtaendelea kupata hasara kama inavyotokea kwa KQ