Aisee! Mastaa hawa 10 walishikwa mkono wakajibeba kabisa...

Hili Pepo la wasanii kuwakimbia maproduzer na wengine kuanzisha productions zao wenyewe linahamia taratibu Kwa music video directors..mambo yanaanza kwenda mrama mdogomdogo,soon mambo yatakuwa mabaya sn Kwa bahadhi ya directors
Nandy alianzisha video production yake akatengeneza video ya jay melody ilikuwa 😂😂😂
 
Ule niliupenda sana. Sema jamaa yuko down to earth
 
Belle 9 alichomoka mwenyewe na hit song "sumu ya penzi" nadhani 2009 and since then akawa anapandishia hit after hit, hiyo dear gambe ilikuja baadae sana
 
Hili Pepo la wasanii kuwakimbia maproduzer na wengine kuanzisha productions zao wenyewe linahamia taratibu Kwa music video directors..mambo yanaanza kwenda mrama mdogomdogo,soon mambo yatakuwa mabaya sn Kwa bahadhi ya directors
Tatizo ni kwamba monopoly ya Muziki imeruhusu kundi dogo la watu kukua kuliko wengine na kibaya zaidi wasanii wengine nao wameingia mtegoni.

Kila msanii akifanya interview anamzunguzia Diamobd, Alikiba au Harmonize. Maana yake hapo anamfanyia endorsement huku akidogosha brand yake.

Ndio maana wasanii wengine hata kama hawajatoa ngoma wanasikika tu.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wasanii kumiliki pesa na hivyo kuwa na nguvu ya kumiliki mpaka kampuni za video productions.

Msanii akishakuwa na studio, video production tayari wewe kama producer au video director unaishiwa nguvu ya maamuzi.

Na sasa hivi msanii kana Diamond amekuwa na media, hata media personalities na wasanii wenyewe wameshakosa nguvu ya kumchallenge kwa mategemeo kuwa labda watakuja kupata kazi hapo.
 
Hili Pepo la wasanii kuwakimbia maproduzer na wengine kuanzisha productions zao wenyewe linahamia taratibu Kwa music video directors..mambo yanaanza kwenda mrama mdogomdogo,soon mambo yatakuwa mabaya sn Kwa bahadhi ya directors
Kuna watu wataanza kurekod Kwenye vipaimara ha haa ...tatizo jingine technolojia ya camera inakimbia Sana aisee , camera ya million 2 ina 4k , Kideo kinaonekana swaaafi kabisa, ukipitisha kwenye editing program kitu kinatoka mswano Sana .... Kwa nini uende Kwa mtu akupige sjui video million 10 ......
 
Hivi Alisema na Kabwela ipi ilitangulia?

Kuhusu Vee money...mwanzoni baada ya ngoma yake na dimpoz niliona kama kabahatisha, sikuwahi kkutegemea kama angekuwa talented kiasi kile alivyokuja kuni prove wrong.
 
Ahahah Kaka kuna video sasa hivi haziitaji tena makamera ya bei mbaya..kitakachkfanya wasanii wqkimbilie kwako si kamera Kali Bali ni creativity ya director husika
Kwa hiyo sasa hivi director atapiga pesa Kwa ubunifu na ukali wa video zake Tu

Wimbo wa John legend-good night ulishutiwa na camera ya simu ya Google..imagine bro!!
 
Very true mkuu
 
Yes, hata ngoma ya I'm sorry feat Kane Brown ni kamera ya iPhone.

Walishoot wakati wa lockdown na ni ngoma kali.
 
Yes, hata ngoma ya I'm sorry feat Kane Brown ni kamera ya iPhone.

Walishoot wakati wa lockdown na ni ngoma kali.
Hanscana asipoangalia atapotea,sasa hivi kushuti kwenye majengo mazuri kisha unaedit video alafu unategemea ulipwe mamilioni itakuwa ngumu sn Kwa wasanii kufanya hivyo

Aongeze ubunifu..jamaa wa South America ni wakali sn wale watu,wanachoimba sikielewi lkn video zina ubunifu mkubwa sn.Bongo tukijaribu Kuwaiga japo kidogo Tu mambo yatakuwa poa
 
Kiukweli Hanscana hana ubunifu wowote. Silaha yake kubwa anayotegemea ni ubora wa Camera
 
Mimi naliangalia hili suala la monopoly kwa jicho lingine kidogo, lile la wasanii kutamani uhuru ama kuondoka kwenye maisha ya kuwa tegemezi kwa producer, director hata media house fulani, hivyo kufanya juhudi ya kuweza kujifanyia hivyo wao wenyewe. Hakika wameona pia kwamba kuna pesa inaweza kutengenezeka kwa kutumia wasanii wengine wasio na uwezo wao kwa sasa.

Hili liko kila mahali na limesaidia wengi ingawa kama ilivyo kawaida katika maisha, kuna wataofanikiwa zaidi ya wenzao kiasi cha kutengeneza monopoly. Nilisoma mahali kuwa JayZ aliamua kusambaza muziki wake mwenyewe aepuke kulizwa na distributors, na baadae akaenda DefJam. Tekno pamoja na kuimba pia ni bonge la producer ambae asilimia kubwa ya nyimbo zake anajitengenezea mwenyewe. Hili linampa uhuru na uwezo wa kusaidia wengine pia ('If' ya Davido nasikia ni kazi ya Tekno mwanzo mwisho).

Katika vitu ninavyofurahia kama mpenzi wa muziki wa bongo ni kuona Diamond, Harmonize, AliKiba na hata Rayvanny walivyokua kutoka kuwa wasanii wadogo, mpaka wa kawaida, hadi kumiliki (japo sehemu ya) label zao wenyewe na hata vituo. Hii inamaana wanajipunguzia utegemezi kwa kina Radio One, Clouds na wengineo kupata promo, ambayo nayo inawapa nafasi wasanii wadogo kusikika katika media hizo.

Diamond mwenyewe alitoboa baada ya kuamua kufanya muziki wake uwe kimataifa zaidi na kupata 'international appeal' iliyowasaidia kina Rayvanny, Harmonize na wengine nao kupaa zaidi. Naamini angetegemea kina Clouds asingefika hapo. Hata suala la nchi kuwa na Fiesta na Wasafi Festival, (Kina Harmonize sijui yao kama ipo inaitwaje)na mengineo ni bonge la ushindi kwa sanaa na taifa. Mbeleni nategemea kuona wasanii wengi zaidi wakifanikiwa kufanya hivyo.

Ningependa hali hii iendelee na nione matajiri wasanii wakiongezeka zaidi na zaidi maana hii itaongeza ushindani na kuongeza pesa mtaani. 'Windfall' yake kwa jamii ni kubwa.
 
Nimeangalia shikorobo ya sheta aisee godfather ni mbwa 😀😀 af goma la 2014 huko ....Ila majonjo mle ya director ni nouma Sana .....Sisi madirector hatuna ,
 
Nimeangalia shikorobo ya sheta aisee godfather ni mbwa [emoji3][emoji3] af goma la 2014 huko ....Ila majonjo mle ya director ni nouma Sana .....Sisi madirector hatuna ,
Ahahah "sisi madirector hatuna"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…