Tatizo ni kwamba monopoly ya Muziki imeruhusu kundi dogo la watu kukua kuliko wengine na kibaya zaidi wasanii wengine nao wameingia mtegoni.
Kila msanii akifanya interview anamzunguzia Diamobd, Alikiba au Harmonize. Maana yake hapo anamfanyia endorsement huku akidogosha brand yake.
Ndio maana wasanii wengine hata kama hawajatoa ngoma wanasikika tu.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya wasanii kumiliki pesa na hivyo kuwa na nguvu ya kumiliki mpaka kampuni za video productions.
Msanii akishakuwa na studio, video production tayari wewe kama producer au video director unaishiwa nguvu ya maamuzi.
Na sasa hivi msanii kana Diamond amekuwa na media, hata media personalities na wasanii wenyewe wameshakosa nguvu ya kumchallenge kwa mategemeo kuwa labda watakuja kupata kazi hapo.
Mimi naliangalia hili suala la monopoly kwa jicho lingine kidogo, lile la wasanii kutamani uhuru ama kuondoka kwenye maisha ya kuwa tegemezi kwa producer, director hata media house fulani, hivyo kufanya juhudi ya kuweza kujifanyia hivyo wao wenyewe. Hakika wameona pia kwamba kuna pesa inaweza kutengenezeka kwa kutumia wasanii wengine wasio na uwezo wao kwa sasa.
Hili liko kila mahali na limesaidia wengi ingawa kama ilivyo kawaida katika maisha, kuna wataofanikiwa zaidi ya wenzao kiasi cha kutengeneza monopoly. Nilisoma mahali kuwa JayZ aliamua kusambaza muziki wake mwenyewe aepuke kulizwa na distributors, na baadae akaenda DefJam. Tekno pamoja na kuimba pia ni bonge la producer ambae asilimia kubwa ya nyimbo zake anajitengenezea mwenyewe. Hili linampa uhuru na uwezo wa kusaidia wengine pia ('If' ya Davido nasikia ni kazi ya Tekno mwanzo mwisho).
Katika vitu ninavyofurahia kama mpenzi wa muziki wa bongo ni kuona Diamond, Harmonize, AliKiba na hata Rayvanny walivyokua kutoka kuwa wasanii wadogo, mpaka wa kawaida, hadi kumiliki (japo sehemu ya) label zao wenyewe na hata vituo. Hii inamaana wanajipunguzia utegemezi kwa kina Radio One, Clouds na wengineo kupata promo, ambayo nayo inawapa nafasi wasanii wadogo kusikika katika media hizo.
Diamond mwenyewe alitoboa baada ya kuamua kufanya muziki wake uwe kimataifa zaidi na kupata 'international appeal' iliyowasaidia kina Rayvanny, Harmonize na wengine nao kupaa zaidi. Naamini angetegemea kina Clouds asingefika hapo. Hata suala la nchi kuwa na Fiesta na Wasafi Festival, (Kina Harmonize sijui yao kama ipo inaitwaje)na mengineo ni bonge la ushindi kwa sanaa na taifa. Mbeleni nategemea kuona wasanii wengi zaidi wakifanikiwa kufanya hivyo.
Ningependa hali hii iendelee na nione matajiri wasanii wakiongezeka zaidi na zaidi maana hii itaongeza ushindani na kuongeza pesa mtaani. 'Windfall' yake kwa jamii ni kubwa.