Aisee michezo ya kubahatisha (kubeti) kama huna afya nzuri unaweza ukafa huku unajiona

Aisee michezo ya kubahatisha (kubeti) kama huna afya nzuri unaweza ukafa huku unajiona

Elon J

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2022
Posts
635
Reaction score
1,907
Aise hii michezo ni hatari sana, sio kiuchumi tu zaid kiafya, hii kitu imenikuta jana.

Sasa Jana katika kujaribu zari nikawa nimebeti, nikazipa kama timu nane hivi nikatia stake yangu kiasi, mkeka ukawa unasoma 6m na some thing, nikaendelea na mambo yangu.

Sasa nakuja kucheki mida ya mbili hivi usiku sijaamini, naona kabaki Barcelona tu mkeka utiki, daaa! Nikasema hii ndo siku yangu nikamsikilzia Barcelona mida yake ifike nikajua kabsa baca atashinda kulingana na timu aliyokuwa anacheza nayo.

Bwana weee! Hapa ndo nikaamini michezo ya KUBAHATISHA kama huna AFYA zuri unaweza kujikuta upo hospital.

Dakika ya kwanza tu nashangaa baca kala goli aise nikaona tumbo limejaa ghafla, haja kubwa na ndogo ikanibhana gafla😂 nikajaribu ku cash out inasoma kama 2m na something hapo ni kama dkk ya 15 hivi, moyo ukaniambia acha utoto hebu kuwa na subira, nikaendelea kusikilzia aise dkk ya 24 hvi kama cjakosea wakala chuma ya pili, aise tumbo la kuhara lilinishika gafla nikajiona kabsa kama mtu niliechanganyikiwa, kwenda chooni haja haitoki Yani nikajikuta nazunguka zunguka tu kama kichaa😂

Nikajaribu ku cash out tena inasoma kama laki tisa na something, daaa! Moyo haujaamini Yaani kutoka 6m mpka 900k hapana Bado nikaendelea kujipa matumaini.

Kwa kufupisha Uzi aise ilifika muda jasho likawa linatiririka mpka nikiwa nahisi kizunguzungu,,baada ya kuona kabisa 6m ikiondoka huku naona.

Imefika dkk ya kama 70 Ngoma bado 2-1 nikaona kabsa hapa kitumbua kimeshaingia mchanga, nikajaribu cash out Ngoma inasoma laki nne na kitu nikaona usinitanie Nika cash out ikakubali.

Imefika dkk ya 87s baca kasawazisha ooh aise nikahisi Dunia inanizomea mixer matusi. Yaani hamu ya kula ikakata, usingizi siupati niliona kila aina ya tabu, aise kubet hapana.
 
Hii michezo ya kubahatisha imeanzia Ulaya na kwenye nchi zilizoendelea, wao wanafanya kama hobby tu baada ya kazi za kutwa nzima, yaani kama sisi tunavyofikiria kwenda coco beach ziku za sikukuu.

Sasa nchi za kiafrica kama hapa kwetu TZ imegeuka kuwa kazi rasmi hasa kwa vijana. Ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa.
 
Hii michezo ya kubahatisha imeanzia ulaya na kwenye nchi zilizoendelea, wao wanafanya kama hobby tu baada ya kazi za kutwa nzima, yaani kama sisi tunavyofikiria kwenda coco beach ziku za sikukuu.

Sasa nchi za kiafrica kama hapa kwetu TZ imegeuka kuwa kazi rasmi hasa kwa vijana. Ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa.
Exactly,,hii michezo unaweza kuhisi kama cjui kitu gan Yan, unaweza kwel kuingia for leisure tu, but muda unavozid ndivo unavendelea kuwa Teja wa hii michezo, sikufichi me mwenyew naona ishaingia kwenye damu Yani hata nikiwa kazin lazm nitenge mda ni bet but naomba mungu niache maana naona si salama Kwa afya
 
Back
Top Bottom