Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Asingetapeliwa ungejifunza wapi?😂

Kila pale unapojiona mjanja ujue kuna mtu alivalishwa mzigo ndio wengine wakasanuka . Bila shaka hata wewe umewahi kuibiwa /kutapeliwa
Nimewahi mkuu ila kitambo kidocho🤣🤣🤣.
Nilitaja mpaka namba za siri za airtelmoney 🤣🤣.
 
Siku moja nipo kwenye mizunguko yangu ya hapa na pale maeneo ya Ubungo nikakutana na jamaa mmoja baada ya kuzungumza nae kwa muda akaniambia nimelogwa na kuanza kuniambia mambo ya nyumbani kwetu, akaniambia kama huamini tafuna hili karatasi nikatafuna nikatema nywele Daah si nikaanza kumuamini aisee

Akaniambia nimkabidhi pesa zangu nilikuwa na Sh elfu 30 na simu akaniambia chukua hii dawa nenda mpaka pale kituo cha mwendokasi usigeuke nyuma wala kuongea na MTU ukifika itupe pale.

Ile nafika kituo cha mwendokasi akili inarudi kwamba huyu jamaa nimemuamini VP kumuachia simu yangu na pesa, nikageuka nyuma kumcheki simuoni nikaamua kurudi pale kilichofuata ni majonzi na kilio nimetapeliwa

Sitaisahau simu yangu ya Tecno spark 4 asee, niliumia sana siku hiyo
Mtakuja muombwe macho na mtoe.🤣🤣🤣🍑
 
Yule tapeli nilimkubali ana mbinu, kikubwa usijadiliane naye. Mimi nijiona namumudu, akanipiga dk za jioooni
Anakuwa na bahasha mbili,moja INA simu halisi nyingine INA sabuni.Anakupa simu halisi unaishka ,unaitest iko pa,atahakikisha mnashindwana bei ili umrudishie ile simu.Ukishampa bahasha yenye simu anajifanya kukubali offer ya ko.Unampa pesa anakukabidhi bahasha yenye sabuni.Kwakuwa ameishakupanga kwamba ni ya wizi anakuambia uondoke haraka sana pale na kwakuwa unaamini umenunua kwa pesa ndogo unaondoka faster,ukija check unakuta umemnunua Sopu kwa million mia.Ukirudi ulipomuacha humkuti.Imeisha hiyoooo
 
Mimi juzi juzi tu nimepigwa 50k nilikuwa nimekaa pale mwanyamala kwa kopa karibu Na kituo kidogo cha polisi nikitekeleza majukumu yangu...wakaja madogo watatu wamevaa tisheti za tigo,wakaniambia kaka tuna huduma ya kubadirisha laini yako iwe 5g nikawaambia sihitaji wakaniambia ni bure nikawaambia poa wakaniomba laini ya tigo (nalifanya makosa makubwa kuwapa laini yangu Na namba yangu ya muda) walikuwa Na Ile mashine ya kusajilia kumbe wale wapumbavu wakiisha download apps ya whatsup kwenye Ile mashine Na muda huohuo Wana namba yako ya nida inakuwa rahisi kupata namba ya Siri..... Muda kidogo naona meseji za miamala zinatembea kwenye simu yangu kumbe jamaa wanahamisha tu kupitia Ile mashine..
 
Wewe na mleta mada wote wasukuma. Inasemekana ni rahisi zaidi kumtapeli msukuma. Ya kweli haya mkuu?
 
Miamba wa dizaini hii wapo toka kitambo sana hapo Dsm, ni kwamba hukuwahi kuwajua tu pigo zao.
 
Back
Top Bottom