Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Wizi wa kizamani ndio unatapeliwa nao leo?
 
Siku moja nipo kwenye mizunguko yangu ya hapa na pale maeneo ya Ubungo nikakutana na jamaa mmoja baada ya kuzungumza nae kwa muda akaniambia nimelogwa na kuanza kuniambia mambo ya nyumbani kwetu, akaniambia kama huamini tafuna hili karatasi nikatafuna nikatema nywele Daah si nikaanza kumuamini aisee

Akaniambia nimkabidhi pesa zangu nilikuwa na Sh elfu 30 na simu akaniambia chukua hii dawa nenda mpaka pale kituo cha mwendokasi usigeuke nyuma wala kuongea na MTU ukifika itupe pale.

Ile nafika kituo cha mwendokasi akili inarudi kwamba huyu jamaa nimemuamini VP kumuachia simu yangu na pesa, nikageuka nyuma kumcheki simuoni nikaamua kurudi pale kilichofuata ni majonzi na kilio nimetapeliwa

Sitaisahau simu yangu ya Tecno spark 4 asee, niliumia sana siku hiyo
Hahahahahaha daaah wewe jamaa ni fala au???
 
Uzuri wa daslam mafala wanaingia kila siku toka mikoani,kwahyo utapeli hautakaa uishe,na siku hizi mbinu zimebadilika kuendana na wakati .
 
Back
Top Bottom