Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Sitasahau nilipouziwa kipande cha UDONGO kwa tsh 60000/= kariakoo badala ya Nokia N70...ilikuwa mwaka 2010 😂😂😂
Ama pale Karume walikua na mtindo wanakuonesha jeans ingine kesha wanakufungia ingine ilokua nusu yani imekatwa.
Ukifika home uitoe unakuta suruali kaptura.
 
Kuibiwa na kutapeliwa vina uhusiano ? Elimu kidogo hapo tafadhari niko njia panda
Sio kila kuibiwa ni kutapeliwa ila kutapeliwa ni sehemu ya kuibiwa.
Tapeli ni mwizi anayeiba kwa ulaghai pasi na utumizi wa nguvu.
Conmen are thieves.
 
Unatapeliwa huku unaona kawaida ila baadae majuto na kujilaumu kuhusu haka kakitu KUAMINI
Hiyo ni kawaida unapopoteza kitu ndipo utajua kuwa limepotezea kijinga, hapo hapo akili inarudi na kuona njia zote ambazo zingeweza kuzuia hilo tukio.
 
Daresalaam mtu akikusalimia mtu yeyote usiyemjua awe mtoto mdogo, mwanamke mrembo kijana shababi au mzee au mbibi kitu cha kwanza mchukulie kama tapeli.

Kitu cha pili hulazimiki kumwitikia salamu yake na unaweza kuendelea na safari au kazi yako.

Kiungwana ukimwitikia usiongee chochote kwake.
Akikikuongezea manane kama hayakuhusu mwambie mimi sijui, na endelea na mambo yako.

Ukimsikiliza akikuhusisha tu na mambo yake au ya kwako tambua kuwa huyo ni tapeli

Mfano anakuuliza "naenda Kekoko mwonyeshe daladala za huko zilipo.
Ukisikia "nisindikize" huyo ni tapeli.

Kuna visichana vinakuongelesha kana kwamba vimepotea hivi, vielekeze kituo cha polisi cha karibu ili aende au viende vyenyewe hasa sehemu ambayo huwajui watu

Kama kuna watu unawajua washirikishe kwenye tatizo lake.

Daresalaam usifanye chochote wala kumpa ushirikiano yeyote usiye mjua.
Unaweza kutoa dakika moja tu umsikiliza mtu usiye mjua na isizidi hapo.
Ukijifanya mwema Dar, umetapeliwa.
Daresalaam usiye mjua yeyotechukulie kama tapeli.

Nawasilisha.
 
Umenikumbusha mamaangu alirudi home analia.
Twamuuliza nini!? Akadai kipindi anatembea toka soko kuu la Kariakoo kwenda Karume apande gari za Kigamboni alikutana na wadada wawili,mmoja alidai mgonjwa mwingine akaomba asaidiwe wampeleke sehemu tulivu,sasa yule mwingine akasema lete nikushikie pochi kipindi unamnyanyua kumkokota umuweke sehem tulivu,mama akamkabidhi bhana.
Ile anamweka alipokusudiwa anageuka nyuma hamuoni yule mdada kaenda na pochi.
Yani mkuu hii Dar ukitaka uwe salama kuwa mbinafsi tu I repeat kuwa mbinafsi.
Ukitembea kausha.
 
Simu na pesa haitoshi, watu wajinga kama wewe mlitakiwa muibiwe hadi nguo, muachwe uchi kabisa, hahaha
 
Kama wewe ndio tapeli kwangu huchomoki kabisaa sijui utapitia angle ipi ? Labda uhack simu
Tena wewe kama ID yako umekaa kifursa fursa..kuwapiga easy sana...na mkipigwa huwa hamsemi kwa aibu😂😂
 
Tena wewe kama ID yako umekaa kifursa fursa..kuwapiga easy sana...na mkipigwa huwa hamsemi kwa aibu😂😂
Sioni kwangu lamaana utafaidika kwanza hela sina sijui kingine labda sms za simu🤭🤭🤭
 
Kutapeliwa sijawahi, ila kuna siku nilipigwa ngeta roba ya mbao kizembe tu.
Aisee sitasahau
Jamaa waliondoka na maokoto km M2+ pesa ile hata kwanini nilitembea nayo sijui.
Ilikua asubuhi sa 11 hapo migo kanisani kona ya makanya
 
Back
Top Bottom