Aiseee maisha haya; Nimelima ekari 2, nimevuna gunia 6 tu

Aiseee maisha haya; Nimelima ekari 2, nimevuna gunia 6 tu

Aache ubunge na uwaziri akalime
Atuoneshe mfano

Ova
Thubutuuu..
Alivyokuwa "Kigong'ota" aliwahi sema anataka kuwa mkulima mkubwa.

Alivyomuona baba yake akiwa meya wa Dom kajiuzia gari kwa elfu 22, akaona kumbe siasa inalipa.
 
Nilikuwa nimelima mahindi ekari 2, Jana nimeenda kuvuna haya mahindi nimempata gunia 6.

Nimeagiza Bajaji/ Toyo la mizigo kuja kubeba haya magunia 6 ya mahindi ambayo bado sijayapukuchua toka kwenye magunzi.

Cha ajabu kwangu ni ajabu bajaji/ Toyo limefika kijijini kuna zuio la mtendaji wa kijiji anaomba ushuru wa Mazao yangu ambayo ni chakula cha nyumbani kwangu
Hongera mkuu, kuna wengine hawajapata kabisa. Kulingana na mwaka husika. Kwa mwaka huu mvua zilizindi sanaa. Mwakani nayo ni siku lima tenaaa.
 
Huwa siwa sikilizagi wale wanakwambia heka 1 ukilima sawa na faida ya milioni 10. Changamoto za kila unachofanya ni wewe
 
Kwako faida unaipataje? Maana mbolea lazima ununue kwa money, vibarua n.k
vizuri sana:-
  1. cha kwanza kubali kwamba unajifunza kilimo na uone gharama unazotoa ndio fees yaani kuwalipa vibarua na gharama zingine.
  2. kingine kama ardhi ni yako kubali kuwa unalima kwaajili ya kuwa na ardhi ikufae siku zijazo.
  3. ili kilimo kilete tija lazima ikiwezekana kichanganywe na mifugo na ndipo hapa tunapokuja kwa issue ya money one to three ukiweza.
    1. unachukua mazao unaipa mifugo mifugo inatoa mbolea kisha unauza mifugo ndo unapata hela hapa kitakulipa
    2. au unalima mazao yanayoweza kutumika kwa chakula cha mifugo na biashara mfano unalima mabonga kwa ajili ya kupata mbegu za maboga kwa kuwa ni bidhaa muhimu kwa sasa kwa ajili ya bundle la familia na kisha maboga unawapa nguruwe kisha unauza nguruwe na unapatafedha.
  4. kilimo ni zaidi ya fedha kila anayelima anamalengo tofauti mwingine analima ili kukimbia sumu zinazopatikana kwenye mazao yanalimwa kibiashara. mfano kwangu mimi unga wa dona wa kununua dukani sio salama tena kwa kuwa mkulima kama kavuna magunia 100 anatenga gunia 20 kwa ajili ya chakula kisha yanayobaki anapiga dawa ambayo inaweza kuwa na madhara siku zijazo. hivyo kwa mkulima kama kapata chakula kwa hekari mbili zinamtosha sana.
 
magunia 6 ya mahindi ambayo bado sijayapukuchua toka kwenye magunzi.
Hayo ukipukuchua utapata labda junia moja na robo..

Anakuomba ushuru kiasi gani?

Kwani walifuta ile decree ya Magu ya kuzuia tozo kwa mazao yasiyozidi tani 1,5?
 
Back
Top Bottom