Aisha alipigwa, kuvuliwa nguo zote na Kurekodiwa, Na kwamba akisema kwamba alitekwa Picha zake zitavujishwa Mitandaoni na kumuua

ABDUL NOMA
 
Wanatekana wenyewe hao kuleta fitna, pattern inaonesha wanaotekwa chadema ni Waislam tu. Kwanza Mohamed, sasa Aisha.

Kuna fitna kubwa inapikwa hapa.


Kama ni fitna kwanini Polisi wasichunguze wawashike hao watekaji. Kama ni Chadema wanateka watekaji washikwe tatizo sio chama ni wahalifu washikwe bila kujali chama.
Kama Chadema wana jeshi la kuteka mtu kutoka kwenye basi mchana na kwenda kumuua na Raisi kasema apewe ripoti ambayo kama kaipata kafanya siri!
Huyu Mama wenzake wamteke kwa kuchoma kanga za Samia! Dada yangu kajipime kidogo mapenzi yako na Mama sasa . Yaani uchawa wako umefikia sehemu ya ku suppport haya. Jiulize wadini ni Chadema au wewe!
 
Ukitaka kuishi tanzania kwa amani fake ya ccm, usiwakosoe. Kuchoma kitenge ni jambo dogo sana kwa nchi zenye ukomavu wa demokrasia. Watu uchoma bendera za nchi iwe kitenge chenye picha ya samia. Je ccm inataka rais wawe misukule wake.
 
Pole yake ila Hawa Jamaa ndio wale walikuwa wanaimba SSH muuaji na wakachoma vitenge alivyovitoa?

Haya mambo Huwa wanaoyataka wenyewe Kwa Kushindwa kutumia akilalamika na busara
 
Hiyo ni jinai na ni kazi ya jamhuri hiyo haihitaji ridhaa ya mtu. Kama kweli hajafanyiwa ubaya huo basi jamhuri imfungulie mashtaka ya kudanganya umma. Aisha ameeleza yaliyomkuta na ameonesha majeraha aliyopata. Je inawezekana mtu mzima mwenye akili timamu apange njama ya kukubali kudhuriwa na wenzake kwa sababu za kisiasa? Ili apate nini hasa? Au una maana gani? Yeye kukataa kutoa ushirikiano kwa polisi hakuhalalishi kwa aliyofanyiwa.

Aisha ameona gari yenye namba ya polisi ikihusika kwenye tukio la yeye kutekwa na kupigwa halafu unataka aende polisi kutoa ushirikiano, huo ni ujuha.

Lissu alipopigwa risasi uliwahi kusikia jamhuri imefungua jalada la uchunguzi na kumhoji Lissu? Mtu hadi anapewa ulemavu watu wanakalia kimya kama hakuna lililotokea unaona ni sahihi? Ingekuwa ni kiongozi wa ccm amefanyiwa hayo wangekaa kimya?Ukandamizaji wa haki dhidi ya upinzani sio suala jipya na ni moja ya sababu ya ccm kuchukiwa na watu waliokuwa neutral kwenye siasa.
 
Duh

Kumrekodi mama wa Kiislam akiwa mtupu ni Dhambi mbaya Mno mbele ya maulana 🐼
Mkuu; Usiwatweze wengine. Kwa Binadamu yoyote yule; Ni dhambi kubwa au mbaya mno (ni kosa) kumrekodi mtu yeyote akiwa mtupu - huo ni Udhalilishaji wa kiwango cha juu na uliovuka mipaka. Hairuhusiwi na Haikubaliki kabisa.
 
Samia ni mwenyekiti wa ccm pia. Kama wanawake wa CDM walichoma kanga za Samia kama mwenyekiti wa chama kuna tatizo gani wakati ni sehemu ya siasa ya vyama. Inashangaza kwamba siasa zinawagawa watanzania kwa sababu tu watu fulani wananufaika na madaraka.

Tukio kama hilo hutosikia ccm wala viongozi wa dini wakikemea vikali ila wakisikia kuna maandamano ya amani ya kupinga uovu huo wanajitokeza na kuhubiri amani na kukemea watu wasiandamane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…