Aisha alipigwa, kuvuliwa nguo zote na Kurekodiwa, Na kwamba akisema kwamba alitekwa Picha zake zitavujishwa Mitandaoni na kumuua

Aisha alipigwa, kuvuliwa nguo zote na Kurekodiwa, Na kwamba akisema kwamba alitekwa Picha zake zitavujishwa Mitandaoni na kumuua


View: https://m.youtube.com/watch?v=UWMD2TZIRiA
Kiongozi wa BAWACHA - Gari jeupe Land Cruiser watu sita namba plate inaanzia na PT ...., mtambuzi mwanamke alinifuatilia toka stendi ya basi tukapanda wote nilidhani ni abiria wa kawaida ...

Wamenidhalilisha walinivua nguo na kunipiga picha nikiwa uchi .... wamenitishia nikiita press conference watavujisha picha hizo za kunidhalilisha ...

Nimepata kipigo kikali mwili wote umevilia damu nawaonesheni sehemu za mikono na miguu muone jinsi maungo yakivyovilia ila siwezi kuwaonesha sehemu nyeti za mgongoni, tumboni ...l

Lakini hospitali ya Mwananyamala nilipopelekwa madaktari na manesi walinikakuga mwili wote kuona kipigo nikichopata ili waweze kunipa huduma sahihi na kunipeleka chumba cha X-Ray kuona majeraha ya ndani ya mwili ...

ABDUL NOMA
 
Wanatekana wenyewe hao kuleta fitna, pattern inaonesha wanaotekwa chadema ni Waislam tu. Kwanza Mohamed, sasa Aisha.

Kuna fitna kubwa inapikwa hapa.


Kama ni fitna kwanini Polisi wasichunguze wawashike hao watekaji. Kama ni Chadema wanateka watekaji washikwe tatizo sio chama ni wahalifu washikwe bila kujali chama.
Kama Chadema wana jeshi la kuteka mtu kutoka kwenye basi mchana na kwenda kumuua na Raisi kasema apewe ripoti ambayo kama kaipata kafanya siri!
Huyu Mama wenzake wamteke kwa kuchoma kanga za Samia! Dada yangu kajipime kidogo mapenzi yako na Mama sasa . Yaani uchawa wako umefikia sehemu ya ku suppport haya. Jiulize wadini ni Chadema au wewe!
 
Ukitaka kuishi tanzania kwa amani fake ya ccm, usiwakosoe. Kuchoma kitenge ni jambo dogo sana kwa nchi zenye ukomavu wa demokrasia. Watu uchoma bendera za nchi iwe kitenge chenye picha ya samia. Je ccm inataka rais wawe misukule wake.
 
Hapa ndipo Tanzania ya Nyerere ilipofikishwa na Watukufu aliowaachia ambao wamejipa Uungu Mtu, Ngoja tuone Mwisho wao.
================

Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Aisha Machano, ambaye anadaiwa kutekwa na kuteswa na baadae kuokotwa kwenye pori la Kibiti, akizungumza tukio zima mara baada ya kuachwa porini Kibiti na kisha kujikuta Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo alipatiwa matibabu.

Tukio hilo la kutekwa na kuokotwa kwa kiongozi huyo wa Baraza la Wanawake la Chadema Taifa, lilitokoa jana tarehe 19 Oktoba 2024, Kibiti mkoani Pwani na tayari jeshi la polisi limeshatoa taarifa ya kuanza kwa uchunguzi wa tukio hilo.

Soma Pia: Aisha Machano, Katibu mwenezi BAWACHA Taifa, alitekwa na kupigwa sana, ameokotwa porini akiwa na hali mbaya

Pia soma:Kuelekea 2025 - Aisha Machano, Katibu mwenezi BAWACHA Taifa, alitekwa na kupigwa sana, ameokotwa porini akiwa na hali mbaya
Pole yake ila Hawa Jamaa ndio wale walikuwa wanaimba SSH muuaji na wakachoma vitenge alivyovitoa?

Haya mambo Huwa wanaoyataka wenyewe Kwa Kushindwa kutumia akilalamika na busara
 
Huwa hawataki kushirikiana na Polisi kwa visingizio vya kukosa imani.Najua unajua kwamba ushahidi wa mlalamikaji ni muhimu sana kwenye upelelezi.Kwenye hili tukio la Aisha imebidi Polisi wampekee PF3 baada ya kugoma kuripoti Polisi ili asaidiwe.Sasa unajiuliza umetekwa unaogopa kutoa maelezo Polisi?Au kuna jambo linafichwa?
Hiyo ni jinai na ni kazi ya jamhuri hiyo haihitaji ridhaa ya mtu. Kama kweli hajafanyiwa ubaya huo basi jamhuri imfungulie mashtaka ya kudanganya umma. Aisha ameeleza yaliyomkuta na ameonesha majeraha aliyopata. Je inawezekana mtu mzima mwenye akili timamu apange njama ya kukubali kudhuriwa na wenzake kwa sababu za kisiasa? Ili apate nini hasa? Au una maana gani? Yeye kukataa kutoa ushirikiano kwa polisi hakuhalalishi kwa aliyofanyiwa.

Aisha ameona gari yenye namba ya polisi ikihusika kwenye tukio la yeye kutekwa na kupigwa halafu unataka aende polisi kutoa ushirikiano, huo ni ujuha.

Lissu alipopigwa risasi uliwahi kusikia jamhuri imefungua jalada la uchunguzi na kumhoji Lissu? Mtu hadi anapewa ulemavu watu wanakalia kimya kama hakuna lililotokea unaona ni sahihi? Ingekuwa ni kiongozi wa ccm amefanyiwa hayo wangekaa kimya?Ukandamizaji wa haki dhidi ya upinzani sio suala jipya na ni moja ya sababu ya ccm kuchukiwa na watu waliokuwa neutral kwenye siasa.
 
Duh

Kumrekodi mama wa Kiislam akiwa mtupu ni Dhambi mbaya Mno mbele ya maulana 🐼
Mkuu; Usiwatweze wengine. Kwa Binadamu yoyote yule; Ni dhambi kubwa au mbaya mno (ni kosa) kumrekodi mtu yeyote akiwa mtupu - huo ni Udhalilishaji wa kiwango cha juu na uliovuka mipaka. Hairuhusiwi na Haikubaliki kabisa.
 
Kama ni fitna kwanini Polisi wasichunguze wawashike hao watekaji. Kama ni Chadema wanateka watekaji washikwe tatizo sio chama ni wahalifu washikwe bila kujali chama.
Kama Chadema wana jeshi la kuteka mtu kutoka kwenye basi mchana na kwenda kumuua na Raisi kasema apewe ripoti ambayo kama kaipata kafanya siri!
Huyu Mama wenzake wamteke kwa kuchoma kanga za Samia! Dada yangu kajipime kidogo mapenzi yako na Mama sasa . Yaani uchawa wako umefikia sehemu ya ku suppport haya. Jiulize wadini ni Chadema au wewe!
Samia ni mwenyekiti wa ccm pia. Kama wanawake wa CDM walichoma kanga za Samia kama mwenyekiti wa chama kuna tatizo gani wakati ni sehemu ya siasa ya vyama. Inashangaza kwamba siasa zinawagawa watanzania kwa sababu tu watu fulani wananufaika na madaraka.

Tukio kama hilo hutosikia ccm wala viongozi wa dini wakikemea vikali ila wakisikia kuna maandamano ya amani ya kupinga uovu huo wanajitokeza na kuhubiri amani na kukemea watu wasiandamane.
 
Back
Top Bottom