Aishi Manula sikia hili

Aishi Manula sikia hili

Kitambi chakufutia tachi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2019
Posts
1,063
Reaction score
2,566
Salaam wakuu,

Binafsi ninaamini Aishi S Manula ndiye mlindalango bora wa kitanzania kwa sasa ila kuna jambo ananikera sana.

HAWEZI KUCHELEWESHA MUDA (nimemuona kwenye michezo mingi ikiwemo wa jana dhidi ya Benin) yani timu yake inaongoza bao moja na imeelemewa muda wote wanashambuliwa wao kisha anadaka mpira dk ya 75+ hata kulala halali wala kusingizia ameumia badala yake anainuka na kuanzisha mpira haraka unakera.

Ile kuchelewesha muda huwaudhi wachezaji wa timu pinzani na kusababisha kutoka mchezoni kwa namna fulani.

MANULA BADILIKA.
 
Mkuu mazingira ya kuchelewesha muda jana hayakuepo.

Hapakua na kugongana gongana na washambuliaji wa timu pinzani, afu wale ball boys walikua sharp sana kurudisha mipira uwanjani (goal kick).

Alijitahidi kutafuta mazingira ya kupoteza muda ila ikawa ngumu sana.

NB: Maoni yangu kulingana na nilivoshuhudia mchezo.
 
Mkuu tambua kuwa kila dakika ya mchezo imewekwa kwa ajili ya kucheza sio kufanya maigizo ya kujifaya umeumia! Binafsi sikualiani kabisa na mtindo huo!

Hivi hukuona kuwa kua kipidi cha dakika hizoizo Samatta alibaki kidogo atupatie goli la pili ? Sasa kujiagusha hovyo kama timu za Mwadui au Meya City huoi kama ni kujiaisha?

Tuwapongeze tu walipambana na kiume aisee!
 
Haa Haa
Ushauri Wako Hautapokelewa Sababu Moja,
 
Mkuu mazingira ya kuchelewesha muda jana hayakuepo.

Hapakua na kugongana gongana na washambuliaji wa timu pinzani, afu wale ball boys walikua sharp sana kurudisha mipira uwanjani (goal kick)...
Haha sure mkuu wale watoto walikua wanarudisha mali chap chap kweli uwanjani, nilikua mpaka nacheka aisee
 
Mkuu mazingira ya kuchelewesha muda jana hayakuepo.

Hapakua na kugongana gongana na washambuliaji wa timu pinzani, afu wale ball boys walikua sharp sana kurudisha mipira uwanjani (goal kick).

Alijitahidi kutafuta mazingira ya kupoteza muda ila ikawa ngumu sana.

NB: Maoni yangu kulingana na nilivoshuhudia mchezo.
wale waokota mipira sijui walikuwa trained yani anamuwekea kabisa mpigaji mpira apige badala ya yule mpigaji kuuweka yeye
 
Kabla ya kipindi Cha pili kuanzia refa aliita magolikipa wore nafikiri alikuwa anawaonya juu ya kupoteza muda
 
Salaam wakuu.

Binafsi ninaamini Aishi S Manula ndiye mlindalango bora wa kitanzania kwa sasa ila kuna jambo ananikera sana.

HAWEZI KUCHELEWESHA MUDA (nimemuona kwenye michezo mingi ikiwemo wa jana dhidi ya Benin) yani timu yake inaongoza bao moja na imeelemewa muda wote wanashambuliwa wao kisha anadaka mpira dk ya 75+ hata kulala halali wala kusingizia ameumia badala yake anainuka na kuanzisha mpira haraka unakera.

Ile kuchelewesha muda huwaudhi wachezaji wa timu pinzani na kusababisha kutoka mchezoni kwa namna fulani.

MANULA BADILIKA.
Kwa hili namtetea Manula, kijana wangu wa kutokea kule Chikago Mkamba morogoro. Kupoteza muda bila sababu ni hatari sana kwa timu yako.

Maana wachezaji wenzako watapunguza kasi ya kucheza na hivyo kuruhusu makosa, na kufungwa dakika za mwisho.
 
Wewe jamaa una muda gani kuufatilia mpira, yaani mtu upo kwenye world qualifications unaanzaje kuchelewesha mpira,

Yaani saving alizofanya Jana bado tu mnamkosoa,kweli Kuna mijitu hairidhiki muwe na shukrani Basi

Ukimtoa Msuva aliyescore,manula ndiyo kacheza vizuri,Mambo unayoyaleta hayana tija kabisa
 
Inawezekana pia ni maelekezo ya benchi la ufundi maana wao ndio waliokuwa uwanjani kwa hiyo ni rahisi zaidi kupeleka maelekezo kwa namna wanavyotaka acheze.
 
Unapoteza muda alafu unakuja kufungwa dakika za nyongeza.Hiyo mbinu niyaovyo sana na ziko timu ilishawagharimu.
 
Back
Top Bottom