Aishi na risasi 3 mwilini kwa miaka 11 baada Muhimbili na Bugando kutomfanyia upasuaji

Seriously?

Kwa hio ametunga kwamba alienda ila hakwenda? Hii inaingia akilini kweli?
 
Kauli ya Muhimbili, MOI

Alipoulizwa kutaka kufahamu kama Makasi alipokelewa, Msemaji wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema taarifa za mgonjwa huyo hazionekani.

“Nimeangalia kwenye mfumo sijaona kama alitibiwa hapa Muhimbili, nadhani alipofikishwa hapa alielekezwa kwenda MOI,” alisema Aligaesha

Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi naye alisema taarifa za mgonjwa huyo hazioni ingawa suala hilo halizuii mgonjwa kutibiwa.[emoji2827]
 
Em ngoja kwanza..
Ni risasi hizi hizi ambazo Wakina Taylor wanazitoaga na visu afu wanamwagia Whiskey au Hanson's choice ???
Wewe ulidhani zipi?

Na zile za maigizo ya cinema na movie za kivita sio zenyewe maana zile hazina madhara, uwe unachukua muda wako kuangalia behind the scenes za movies utajifunza kitu, kwenye movies wanafanya kitu kinaitwa make-up kinafanya na make-up designers au make-up artist
 
1.) Yaani taarifa hazionekani na mtu amekaa hapo mwaka mmoja?

2.) Ni mashine gani hiyo iliyoharibika na hadi leo haijatengenezwa?
 
Hivi risasi za plastic kama zinazotumika kweny mamuvi hamna jaman...
 
Watumie mitandao ya kijamii kuomba msaada.
Maana hii ni taarifa tu, ni vizuri kama wangeambatanisha na mawasiliano yao watu huenda wakachangia chochote.
 
Hivi risasi za plastic kama zinazotumika kweny mamuvi hamna jaman...
Wewe unazitaka za nini? Ma-toy yapo kwa Mangi nenda kanunue unaweka maji ya pilipili unachezea
 
Ushauri,arudi tena MOI,tutakuwa nyuma yake kumpambania,maana sidhani kwa uongozi wa sasa pale Muhimbili wanaweza kumuacha bila ya kumpatia matibabu,na swala la gharama,iwekwe wazi tu taarifa za matibabu yake,hawezi kukosa wasamaria wema kumchangia...
 
Em ngoja kwanza..
Ni risasi hizi hizi ambazo Wakina Taylor wanazitoaga na visu afu wanamwagia Whiskey au Hanson's choice ???
Inategemea zipo sehemu gani mwilini.
Kaka ndugu yangu anayo mbavuni toka 1998 imefika kwenye uti wa mgongo (spinal column/spinal cord) sasa ikitolewa ata pooza anakuwa kilema hatosimama wala kutembea.
Risasi ikikaa vibaya kwenye fuvu la kichwa (skull) ukiitoa pressure kwenye ubongo inaweza kusababisha ubongo uvuje na mtu anakufa au anapata ulemavu wa kudumu.

Note: Mimi siyo daktari haya ni maoni yangu tu kama mtu wa kawaida.
 
Sidhani kama maelezo aliyoyatoa yana ukweli kitaalamu, eti mashine za hospital 2 kubwa nchini zilikosa umeme hivyo kushindwa kuzitoa hizo risasi! Ninavyofahamu risasi (hasa hizi za shot guns) zina kawaida ya ku lodge mwilini na Maamuzi ya kuzitoa mara nyingi yanategemea na sehemu zilipo Mfano km zipo karibu na mfumo wa fahamu au karibu na mshipa mkubwa wa damu kitendo cha kuzitoa linaweza kuwa na madhala makubwa ikiwemo kifo au ulemavu mkubwa kuliko kuziacha! Rahisi ni zile zinazokwama kwenye misuli maana Kadri muda unavyoenda ndivyo zinapanda juu mwishowe unaweza zitoa kwa urahisi.
 
Kwani Kikwete bado yuko hai maana hii ilikuwa awamu yake!!!
 
UNYAMA HUU.
RAIS AWAMU YA SITA HAPENDI NA WALA HATAKI MAMBO YA NAMNA HII,NADHANI SOON ATASAIDIKA,KATIKA AWAMU HII YA SITA, AMBAYO NI AWAMU YENYE MUNGU NDANI YAKE.
Linapokuja swala la siasa, Mungu muweke mbali.
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu itamsaidia kupata matibabu mungu atakuponya usikate tamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…