Wana JF nisaidieni.
Asubuhi mchana usiku taarifa za maendeleo ya Uchaguzi Kenya katika vyombo vya habari hapa Tz hadi kushangaza. Labda niko nyuma ya wengine lakini najiuliza ni lipi hasa la kutufanya tushabikie na kushobokea uchaguzi wa wenzetu kwa kiasi hicho?
Ingelikuwa Marekani ama Uingereza ama China naam maana hawa Wababe wana maslahi kwetu! Misaada, Rushwa, Ulinzi nk.
Kwa uchambuzi wa haraka huenda hii ni dalili ya mnyonge unayetamani hayo ya mwenzako yangeonekena kwako! Ume ya miss mno.. unafurahia na kuburudika anavyofanya mwenzio na mwishowe unashusha pumzi ya nguvu baada ya matokeo ya mwisho na kusema Aaaah! Kweli walichuana.
Sioni labda Wajaluo ama Wamasai walioko Tanzania wenye ndugu zao Kenya ndio wakafaidika vipi
Hebu tuache ushamba na tuache upuuzi huo!