Tuna maslahi makubwa sana na nchi yoyote jirani. Kujua kiongozi wao ajaye ni jambo muhimu kwetu kama ilivyo muhimu kwao.
Kenya yenye amani, utulivu na uchumi imara ni faida kwetu.
Jaribu hata kuangalia mapato ya serikali kupitia TRA katika vituo vya mipakani na Kenya kama vile Sirari, Namanga, Holili, Tarakea na Horohoro. Hapo ni makusanyo tu. How about faida kwa wananchi na makampuni ya Tanzania?
Kenya ni soko kubwa kwa bidhaa za Tanzania za Chakula na mboga mboga.
Hata sehemu kubwa ya mifugo inayofugwa kaskazini mwa Tanzania, soko lake kubwa ni Kenya.
Kwa hiyo kinachoendelea Kenya, sio uchaguzi tu, chochote, kinatuhusu.