AJABU: Vyombo vya Habari Tanzania na Watanzania tunavyofuatilia uchaguzi Kenya, tuna maslahi gani haswa?

Umejidharirisha sanaaaa kwa hili bandiko..
 
Uungwana huanzia nyumbani usiwe mwoga wa kufikiri mzembe wewe! rekebisha ya kwako nyumbani kwako kwanza sio kushobokea mambo ya jirani yako!
Wewe hata huelewi kwamba kurekebisha ya nyumbani kutafanikiwa vizuri zaidi kama tukiangalia wenzetu, majirani zetu tunaofanana nao kwa mengi, wameweza vipi pale ambapo sisi bado panatutatiza.

Kenya wana wagombea binafsi, sisi hatuna.

Kenya wana katiba mpya, sisi hatuna.

Kenya wana uwazi mkubwa kwenye kutangaza matokeo, sisi hatuna.

Kenya washapinga matokeo ya uchaguzi wa urais, sisi hatuwezi.

Kenya wamekitoa chama tawala kilichowaongoza tangu uhuru, KANU, sisi hatujaweza.

Kenya wana uraia pacha, sisi hatuna.

Sasa mpaka hapo huoni tu kwamba hata kama tunataka kubadilisha mambo nyumbani tunaweza kujifunza Wakenya wamewezaje kufanya yote hayo ambayo sisi hatujaweza?

Yani unaona nongwa kujifunza kwa jirani yako aliyekuzidi kwa sababu una kiburi cha kutotaka kujifunza kwa wengine tu?
 
Mpuuzi ni Wewe, unaye fikiria kila kitu lazima kiwe na masilahi!
 
Kwani kuna shida kujua kinachoendelea kwa jirani???
 
Hebu tuache ushamba
Wakenya wanasema (nukuu kutoka kwa mtangazaji wa KTN), kati ya Matajiri wakubwa sana 100 hapa Ulimwenguni, 50 kati yao wamewekeza Kenya. Sasa nasubiri maelezo ya watangazaji wetu hapa nyumbani wanaiheshimisha vipi Tanzania .
====
Mleta mada ningekuona umeleta hoja ya maana sana kama ungekuja na hoja ya kuifanya Tanzania sehemu nyeti na muhimu katika kukuza uchumi wake na na kuvutia nchi nyingine kuwa na imani kufanya kazi na Tanzania katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia, kiteknolojia na kadhalika badala ya kuja na hoja za kusimanga watu!!
 
Halafu inawezekana nawewe una watoto wanakuita Baba,au nawewe huwa unatoa ushauri kwenye vikao vya familia/ukoo
 
Wana JF nisaidieni.

Asubuhi mchana usiku taarifa za maendeleo ya Uchaguzi Kenya katika vyombo vya habari hapa Tz hadi kushangaza. Labda niko nyuma ya wengine lakini najiuliza ni lipi hasa la kutufanya...
Zamani nilikuwa nafuatilia kweli kweli ila saizi sina huo mda maana unakuta tv ya Tzn iko busy na uchaguzi wa Kenya as if hakuna vitu vya maana vya coverage hapa Tanzania..

Sijui wananufaika hasa watu wa habari au laa ila mambo ya maendeleo hakuna anaehangaika kuwahabarisha watu..

Vyombo hivyo vinasubiria Yanga na Simba na ajali zitokee, upuuzi mtupu..
 
Tunafurahia jinsi SANNDUKU la kura linavyoheshimiwa.

Katiba mpya tutaidai Hadi tuipate.

Majirani watuambukize Ari ktk kudai na KUSIMAMIA HAKI ktk Nchi.

Ameeeeen
 
Tuna maslahi makubwa sana na nchi yoyote jirani. Kujua kiongozi wao ajaye ni jambo muhimu kwetu kama ilivyo muhimu kwao.
Kenya yenye amani, utulivu na uchumi imara ni faida kwetu.
Jaribu hata kuangalia mapato ya serikali kupitia TRA katika vituo vya mipakani na Kenya kama vile Sirari, Namanga, Holili, Tarakea na Horohoro. Hapo ni makusanyo tu. How about faida kwa wananchi na makampuni ya Tanzania?
Kenya ni soko kubwa kwa bidhaa za Tanzania za Chakula na mboga mboga.
Hata sehemu kubwa ya mifugo inayofugwa kaskazini mwa Tanzania, soko lake kubwa ni Kenya.
Kwa hiyo kinachoendelea Kenya, sio uchaguzi tu, chochote, kinatuhusu.
 
Kwa sababu wewe ni mjinga huwezi ona faida ya kufuatilia uchaguzi wa Kenya.
 
Kwa sababu wewe ni mjinga huwezi ona faida ya kufuatilia uchaguzi wa Kenya.
Safi sana.
 
Tunafuatilia wenye siasa za kistaarabu sio zile za yule kichaa!
 
Uchambuzi ulioenda shule huu.
 
Vy kwenu si mlizuia visitangaze habari yoyote ya Upinzani?

Sasa yako wapi.

Dunia tunapita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…