Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Hawa polisi wetu akili zao wanazijua wenyewe, maneno "Ashok Leyland" aliyoandika manufacturer ni kama hayatoshi wametumia pesa kurudia maandishi yaleyale wakati kuna magari yao mengine yanakosa spare na service

Screenshot_20211117-185830_Samsung Internet.jpg
 
Nimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??

Afande taarifa ya ajali:

KAB/TR/ar/16/2021(×)ajali ya magari manane kugongana na kusababisha majeruhi na uharibifu wa magari (×) mnamo tar 14/11/2021 majira ya saa 18:30 huko katika kijiji cha Kwedilomba kata ya Kwedibomba tarafa ya mzundu wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga barabara kuu ya Segera-Chalinze gari No.T.131 DVU aina ya HOW yenye tela No.T.329 DMR ikiendeshwa na Saimon S/O kristo @Mwanyila, 36yrs, Mbena, mkazi wa Kibaha Pwani akitokea kabuku kuelekea Chalinze alipokuwa akijalibu kulipita gari la mbele yake mahala pasipo ruhusiwa ndipo ghafla mbele yake kukatokea gari nyingine iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea kabuku yenye No.Pt.4036 ashok leyland mali ya jeshi la polisi Tanzania likiendeshwa na H.3637 CPL Juma wa chuo cha Polis CCP Kilimanjalo na ndipo dereva wa gari No.Pt.4036 alisimama ghafla ili kuepuka ajali isitokee na ndipo baada ya gari hiyo kusimama ghafla ikatokea gari nyingine kwa nyuma iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea Kabuku PT.4087 ashok leyland ikiendeshwa na F.7658 CPL John Robert wa makao makuu madogo ya polisi DSM na kugonga kwa nyuma.

Ghafla tena ikaja gari nyingine kwa nyuma No.Pt.4097 ashok leyland ikiendeshwa na F.5889 CPL Kigiri wa Polisi makao makuu madogo ya Polisi DSM na kusimama ghafla PT.4087 ashok leyland na kusababisha gari No. PT.2370 Isuzu bus ikiendeshwa na g.6123 CPL abel wa chuo cha polisi Kidatu na kugonga ubavuni gari no.Pt.4087 ashok leyland pia ikatokea tena gari No.T.573 AYR toyota corolla ikiendeshwa na Amin S/O UR Rasul@Khan, 60yrs, mkazi wa Tanga na kusimama ghafla baada ya kuona ajali na kusababisha gari no.SU 44275 gx v8 mali ya TANESCO DSM ikiendeshwa na Tuma S/O Hassan lean na kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.T.573 AYR Toyota corolla pia ikasababisha gari nyingine yenye no T.773 CND Toyota hilux kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.Su.44275 GXV8 TANESCO na kusababisha majeruhi kwa watu 16 ambao ni 1.D.8420 s/SGT John Mwakipesile 2.Pf.18891 insp sister 3.G.6123 CPL Abel ambao wote watatu wamepelekwa hospitali ya rufaa Bombo kwa matibabu

Na 4.Pf.17534 insp Rashida 5.Pf.18326 insp Nyalugembe 6.Pf.17896 insp Gonga 7.Pf.18202 insp Said 8.Pf.17166 insp Ally juakal 9.Pf.17899 insp Sanya 10.Pf.18445 insp pangane 11.Pf.17691 insp Peter 12.Pf.18719 insp Ohusso 13.Pf.17321 insp Ilomo 14.Pf.18616 insp Anthony 15.Pf.17674 insp Zongho 16.H.1659 pc gift (×) majeruhi wote wameumia sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa kituo cha afya Kabuku na kuruhusiwa (×) chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no.T.131 dvu how yenye tela no.T.329 dmr kujalibu kulipita gari iliyokuwa mbele yake pasipo kuchukuwa tahadhali (×) dereva amekamatwa yupo mahabusu kituo cha polisi Kabuku kwa ajili ya mahojiano (×) eneo la tukio limekaguliwa na acp. Sofia jongo rpc Tanga akisaidiwa na ssp leopord .N. Fungu rto tanga , sp. Elias Rwambano ocs Kabuku, a/insp Rajabu kaimu DTO Handeni pamoja na g.3191 cpl Mussa ambaye ndiye amechora na kupima eneo la tukio (×)///////////

Taarifa kwa maandishi inafuata //////////


Toka rto tanga ///////////

Tatizo hawa wenzetu wa PT wanajifanyaga wapo Juu ya sheria
 
Ukisoma maelezo ambayo kimsingi yameandikwa na kupitishwa na mtu mwenye cheo kikubwa ni lazima ukubaliane na hoja ya Prof. Assad juu ya ile hoja yake ya 60% ya wafanyakazi wa umma.

Pia inatoa picha ya upande wa pili ambayo ni mbaya zaidi kuwa ndugu zetu wengi walioko magerezani makosa yao yanahukumiwa kwenye tukio (kama dereva wa lori) kutegemea utashi wa ofisa aliyepo hata kama ushahidi unasupport kiasi gani uko wazi kama hizi picha zilivyo.

God have mercy on us
 
Ukisoma maelezo ambayo kimsingi yameandikwa na kupitishwa na mtu mwenye cheo kikubwa ni lazima ukubaliane na hoja ya Prof. Assad juu ya ile hoja yake ya 60% ya wafanyakazi wa umma.
Naomba nikumbushe tafadhali
 
kwa maelezo tajwa, dereva na lori lilihusishwa kuovertake halipo hapo..ukisoma tela no according to hiyo report na ukiangalia trailer iliyopo pichani haziwiani usajili.. huyo aliyehama na kwenda kubusanisha vyuma alitanua kulia badala ya kushoto baada ya gari ya mbele yake kusimama ghafla.. ishu kubwa hapo ni mwendo waliokuwa nao walinda usalama wa raia na mali zao, walikuwa mwendo wa msafara bila kisafisha njia wala strobes ..yaani mtaani tunasema walikuwa wanamwaga moto bila king'ora wala vimulimuli. hivyo basi, huyo deree aliyeacha zahma huko nyuma (inasemekana aliosha yaani chap kwa haraka )asibebeshwe zigo lote ..makosa ya kibinadamu yalitokea pande zote ..situation awareness and defensive driving haikukamilika kotekote.
 
Peleka upumbavu wako huko,kusoma hujui hata picha ?

Gari lenye tela ambalo liko kwenye njia yake siyo lililotajwa kwenye ripoti ya polisi kwa mjibu wa namba za tela hilo.

Je unafikiaje mwafaka hapo?
Kuwa makini na majibu yako na kuwa mtulivu unaposoma maelezo ya wenzio.

Usipende uwezo wako wa kufikiri uwe ndo wa wengine. Toa maoni yaki kwa kadri ya uwezo wako inatosha.

Huyu unaemwona hapo amegonga lori inawezekana siyo chanzo cha ajali yenyewe, yeye kwa spidi aliyokuwanayo ametoka nyuma ya leyland/bus akaingia kulia ili kuepusha kuingia nyuma ya basi mwenzake na kukutana na lori.

Hizi ni static pictures, tuwe makini.

Kama unaweza tafuta namba ya tela tajwa kwenye ripoti kama utaipata hapo. Hivyo, kuna vitu haviko sawa kama ukisoma ripoti vs picha.

Ni kweli kuwa ukiingia/kugonga nyuma ya gari la mbele yako bado makosa ni yako kwa kuhusisha umbali vs spidi yako.
 
Ila huyo dereva wa howo ni muhuni sana kawaachia mapoti waseme na tela [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]jamaaa naona aliona wanakuja kwa mbwebwe akawaachia tela
 
Hiyo HOWO ikowapi kwani naona kila mtu dereva wa HOWO mara hivi mara vile kwenye hizo picha mi nimeona kichwa cha lorry ni FAW
 
Back
Top Bottom