Ajali Kimara Mwisho: Lori limezuia njia

Ajali Kimara Mwisho: Lori limezuia njia

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
Wale wazee wa road trip ambao mmepanga kutumia barabara ya Morogoro.

Wale wakazi wa kuanzia Kimara Mwisho kuelekea Mbezi Mwisho.

Kuna ajali ya lori maeneo ya Kimara Mwisho usawa wa kituo cha BRT kiasi kwamba inalazimu magari yanayotoka mjini kutumia Lane ya BRT kuingilia Kimara Korogwe.

Hivyo kama hupendi kugamble unaweza ukatumia barabara mbadala za Goba/Kinyerezi kukufikisha Mbezi Mwisho na ukanyoosha mguu kutafuta Morogoro na kuendelea.

Kimara.JPG
 
Duh... Hakuna madhara yoyote yaliotokana na hiyo ajali? I mean vifo au majeruhi?
 
Duh... Hakuna madhara yoyote yaliotokana na hiyo ajali?

Sina uhakika sana zaidi ya kuona lori lililopinduka ubavu, naamini waliokuwemo hawajapata madhara...

Trafiki wapo maeneo hayo kuongoza magari
 
Wadau poleni majukumu no straight to the point. Nimeona kuna lorry limepinduka maeneo ya Kimara na limeziba njia ya upande wa waendao Mbezi mwisho, sasa ndio nataka kuchomoka mjini na naomba kujua kwa aliyekuwa maeneo hayo vipi wameshalitoa? Ama nitafute njia mbadala.

millardayo-20210823-0001.jpg
millardayo-20210823-0002.jpg
 
sasa ndio nataka kuchomoka mjini na naomba kujua kwa aliyekuwa maeneo hayo vipi wameshalitoa? Ama nitafute njia mbadala
Lile sio la kutolewa leo, labda wataangaika nalo usiku

Hivi kama hapo unapindukaje?

Pale pana kona fulani kali, kabla ya barabara kunyooka kuelekea darajani...

Huenda hiyo kona ndio ilimsumbua dereva wa lori na lilikuwa limebeba kontena...
 
huyo dereva mzembe utapindikaje peupe hapo na gari zinatembea 50 tena malori huwa 30 kwasababu ya mlima
 
Boda washenzi sana..huwa wanapasua katikati ya road na kujichomeka mbele ya magari bila kuangalia
 
Back
Top Bottom