Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Angekuwa Magufuli haya yasingetokea trust me uzembe umekuwa mkubwa sana ofisini siku hizi:

Nipo natazama ITV super brand mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na wananchi walijitokeza wakati wa ajali mbaya iliyouwa Watanzania 20 watatu wakifua hospitalini wanathibitisha kuwa madaktari walipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Korogwe wakaitikia na kusema wao walishapata taarifa mapema kabla hawajapigiwa simu muda wa saa nne na nusu usiku ila cha ajabu wakatokea saa kumi na moja asubuhi.

Baadhi ya madaktari waliopigiwa simu wanaishi jirani na hospitalini kwa kuwa waziri wa afya ni mtu wa Tanga na yupo Tanga ni vema atolee maelezo haraka maana wananchi wanajazba sana juu ya hili.

Wananchi wenye hasira walikuwa wakitaka hatua kali zaidi maana huo ni uzembe na uuwaji kabisa kwa kuwa kama wagonjwa wangepata huduma wasingekufa wengi hasa walipelekwa usiku hospitalini.

"Uzembe kazini ilikuwa ni kutumbua papo kwa hapo kipindi cha jemedari Magufuli"

USSR
 
Ni upuuzi tu!! Kwani masaa ya kazi hayajulikani? Hata uwapigie simu siyo lazima waje muda huo, kwani hawana shughuli nyingine waliyokuwa wanafanya? Eti asingekuwa Magufuli wasingefanya hivyo? UJINGA MTUPU.

Mbona yeye mwenyewe KAFA akiwa Rais? Kwa nini watu hawakumuogopa kuwa atakufa.
 
Mkuu,

Madaktari hawahusiki kufika eneo la tukio, kikosi cha uokozi na zimamoto ndio kazi yao, kazi ya DMO na timu yake ni kuweka sawa mazingira ya kupokea wagonjwa emergency na casuality unit, kufanya triage, kuandaa vyumba vya upasuaji wa dharura, kuandaa dawa, madaktari n.k

Wamewaonea tu, daktari aende huko kufanya nini? Atatundika damu au NS kwenye nini? Anavifaa vya kuvunja nondo, ana vifaa vya kuinulia gani iliyopinduka?

Miongozo ya tiba haipo hivyo. Kama wangetelekeza wagonjwa waliofikishwa hospitalini ingekuwa msala wao, hapo mkuu wa mkoa anafanya siasa tu.
 
Angekuwa Magufuli haya yasingetokea trust me uzembe umekuwa mkubwa sana ofisini siku hizi:

Nipo natazama ITV super brand mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya na wananchi wa lijitokeza wakati wa ajari mbaya iliyouwa watanzania 20 watatu wakifua hospitalini wanathibitisha kuwa madaktari walipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya korogwe wakaitikia na kusema wao walishapata taarifa mapema kabla hawajapigiwa simu muda wa saa nne na nusu usiku ila cha ajabu wakatokea saa kumi na moja asubuhi.

Wananchi wenye hasira walikuwa wakitaka hatua kali zaidi maana huo ni uzembe na uuwaji kabisa kwa kuwa kama wagonjwa wangepata huduma wasingekufa wengi zazi hasa walipelekwa usiku hospitalini.

"Uzembe kazini ilikuwa ni kutumbua papo kwa hapo kipindi cha jemedari Magufuli"

USSR
Mkuu Hujui Masaa ya kazi wewe? Working hours ni 8 tu,sasa uzembe wao uko wapi!?
 
Angekuwa Magufuli haya yasingetokea trust me uzembe umekuwa mkubwa sana ofisini siku hizi:

Nipo natazama ITV super brand mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na wananchi wa lijitokeza wakati wa ajari mbaya iliyouwa Watanzania 20 watatu wakifua hospitalini wanathibitisha kuwa madaktari walipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya korogwe wakaitikia na kusema wao walishapata taarifa mapema kabla hawajapigiwa simu muda wa saa nne na nusu usiku ila cha ajabu wakatokea saa kumi na moja asubuhi.

Wananchi wenye hasira walikuwa wakitaka hatua kali zaidi maana huo ni uzembe na uuwaji kabisa kwa kuwa kama wagonjwa wangepata huduma wasingekufa wengi zazi hasa walipelekwa usiku hospitalini.

"Uzembe kazini ilikuwa ni kutumbua papo kwa hapo kipindi cha jemedari Magufuli"

USSR
Yaani Madaktari waende eneo la tukio? Au ulitaka kusema fire na Polisi?
 
Back
Top Bottom