Mkuu,
Madaktari hawahusiki kufika eneo la tukio, kikosi cha uokozi na zimamoto ndio kazi yao, kazi ya DMO na timu yake ni kuweka sawa mazingira ya kupokea wagonjwa emergency na casuality unit, kufanya triage, kuandaa vyumba vya upasuaji wa dharura, kuandaa dawa, madaktari n.k
Wamewaonea tu, daktari aende huko kufanya nini? Atatundika damu au NS kwenye nini? Anavifaa vya kuvunja nondo, ana vifaa vya kuinulia gani iliyopinduka?
Miongozo ya tiba haipo hivyo. Kama wangetelekeza wagonjwa waliofikishwa hospitalini ingekuwa msala wao, hapo mkuu wa mkoa anafanya siasa tu.