Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Naungana Na wewe kaka sababu baadhi ya wazazi wanaosomesha shule hiyo wanadai wanalipa nauri ya team lakini school basi zao zinaharibiki zaidi ya Mara sita(6)kw a mwezi
 
Sawa Tuache mambo ya magari. KULIKUWA NA UMUHIMU GANI KWA WANAFUNZI KUSAFIRI KWA AJILI YA KWENDA KUFANYA JOINT EXAMS. WANGEWEZA KUTUNGA MTIHANI WAPAMOJA NA WATOTO WAKAFANYA BILA KUSAFIRI.
 
Watanzania tungekuwa wamoja tuhakikishe wahusika wa shule hii wanawajibishwa kwa vifo hivi Na ukizingatia hata RPC anatoa taarifa za uongo kuwa ni wanafunzi 30 wakati ni zaidi ya 33
Wanafunz waliofarik ni 29 na walimu wawil na dereva 1 jumla 33. Sasa wahusika wanahusika vip na wewe wakat ajal ni ajal tu
 
Kusafiri siyo tatizo tatizo kutoa ruhusa ya watoto kupanda gari bovu Na kwenda kuwa ua
 
Acha kutetea ujinga jumla ya waliofariki ni 36 hadi Jana saa moja jioni wanafunzi 33 dereva 1 walimu 2
 
Hilo gari limepita sehemu hatarishi kuliko hata sehemu ya ajali...


Kama kingekuwa bovu kama unavyotaka tuamini basi lisingeweza kutoboa eneo linaitwa Kilima Tembo.
Mkuu hii siyo hoja, kitu kinapokuwa kibovu kwa kadri kinavyopita kwenye sehemu korofi ndipo ubovu huongezeka na hata kuibua ubovu mwingine ambao haukuwepo jambo ambalo huweza kupelekea gari kubuma hata sehemu usiyotegemea ingebuma, kwa hiyo inawezekana ni kweli gari haikuwa imara na kwa kupitishwa kwenye hizo sehemu unazoziita hatarishi zaidi zikaongeza ubovu wa gari na hatima yake imekuwa hapo unapopaona wewe kuwa siyo hatarishi.
 
inasikitisha sana ni sahihi ulichokiandika lakini mkuu kaa ukijua ajari haina kinga gari linaweza kuwa na hayo yote na dreva ni mzoefu wa miaka mingi ninachoweza kusema yawezekana dreva alikuwa mzembe sawa lakini! ! mazingira yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajari yani mvua, ukungu na mahali penyewe yote kwa yote tunapata fuzo kubwa sana sisi tuliobaki Mungu awalaze mahali pema watoto wetu majeruhi awaguse pole kwa kwawalio fikwa na msiba

kinachonipa shida ni mtoto alietoka akiwa hana ana mchubuko zinazunguka picha 2 tofauti za jinsia tofauti sijui ninani kati yao muhusika
napia wanasema aliepona alikuwa kwenye gari la nyuma tofauti na lile lililo pata ajari maana gari zilikuwa wengine wanasema 4 inasikitisha sana kwakweli

Mkuu, mimi kuna siku nilipata ajali mbaya sana, ingawa sikuumia ila gari iliharibika mno. Ulikuwa ni uzembe mdogo tu wa sekunde kadhaa. Toka siku ile nilianza kuamini kuwa kama kila mtu akiwa anafuata sheria zote za barabarani pamoja na kuwa na nidhamu na chombo chako cha usafiri, basi kupata ajali ni kitu kigumu saaaaaana, amini usiamini. Ajali ni kitu kigumu kutokea kama tu utakuwa na nidhamu barabarani wakati huo uki-ensure chombo chako kinafanyiwa services kila inapobidi.

Kwa maoni yangu Ajali ina Kinga tena kubwa sana. Just let's play our part and let's the rest into God's hands.
 
Acha kutetea ujinga jumla ya waliofariki ni 36 hadi Jana saa moja jioni wanafunzi 33 dereva 1 walimu 2

Taarifa ya habari ni kwamba mwenye shule amesema basi

Ilibeba watu 38
Wanafunzi 29 walikufa papo hapo pamoja na walimu 2 na dereva.

Mwanafunzi mmoja amefariki hospitali.

Hivyo wamejeruhiwa wanafunzi 5.

Hivi hilo basi linatakiwa kubeba abiria wangapi?
 
Ingawa gari iliyopata ajali haikuwa "school bus" bali gari ya kukodi,bado kuna umuhimu wa wizara ya elimu kwa kushirikiana na kitengo cha usalama barabarani kuwa na program maalum (mfano kila mwezi) ya kukagua hizi school bus ili kuhakikisha usalama wa watoto,na zisizo na sifa kuwekwa pembeni,na pale gari inapokodiwa kwa kusafirisha wanafunzi ipate kibali cha traffic police baada ya ukaguzi wa kina.
 
Ngoja polisi wafanye kazi yao ya uchunguzi.....mzembe akibainika lazima awajibishwe....wanaumiza sana hawa wadogo zangu ......wote wameondoka kwa siku moja tu .....
 
Back
Top Bottom