Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

HUWEZI SEMA WATOTO WAKAE SEAT LEVEL..!! hiyo ajali ni kama ajali zingine kwamba tatizo ni brake... ukiona mpaka dereva kafaa jua ilikuwa no way out.. Safari za wanafunzi ni Mungu tuu huwa wanakuwa wengi sana na kelele kibaoo.. !! Mbona wanaocheza vigodoro huwa wanajazana kwenye garii tena huku wakifanya ufuska lakini haijawahi tokea ajali mbaya kama hiyo..??? HAKUNA ANAEPANGA AJALI... AJALI HAINA KINGA... TUJIFUNZE KWA HILI LAKINI SIO KULAUMU.. R. I. P
 
Hili ndilo jibu katika point zote, Traffic jaeakagui mabasi ya Shule. Mabasi yote ya mjini daladala na mabadi ya shule hayana mikanda ya abiria, km ingekuwepo vifo vingepungua, kwani watoto wangebaki kwenye viti, idadi jsingefika hiyo. Mwisho dereva na Basi lenyewe havina uzoefu, mabasi ya mijini vibreki ma vya papo kwa papo, huo Mlima tembo una mwinuko na mteremko mrefu kabla hujafika mteremko mwingine wa ajali ni lazima breki silishakorofisha

Utamaduniwa kufunga mikanda pia upewe umuhimu mkubwa. Kwa mabasi makubwa ya mikoani naona siku hizi makondakta na madereva wanakumbusha abiria kufunga mikanda, inasaidia sana.

Ila kuna madereva na abiria wengine bado hawajaona au kutambua umuhimu wa mkanda, Kuna siku nilipanda taxi ya Uber uwanja wa ndege wa Dar Es salaam nilipokaa tu kwenye kiti nikawa nashusha mkanda ili nifunge, dereva akaniambia "usihangaike na mkanda kaka polisi wa huku wala hawaangalii'', nilishangaa sana maana kama dereva mwenyewe hajui umuhimu wa kufunga mkanda na badala yake anadhani tunafunga mikanda ili kuonyesha polisi au kuwaogopa polisi basi ni hatari.
 
Wananunua magari used,wanapaka rangi tu,kumbe ni mabovu,alafu wanabebea watoto,hapa washtakiwe
Sion kama kununua magari used in shida maana hata lingekuwa jipya Leo, likitumika kesho litakuwa used.
 
Mawazo yako kama ya Mpiga ramli chonganishi hayo uliyoeleza ya uhusiano gani na hii ajali? Maana hata gari ingekuwa Mpya bado ajali inaweza kutokea.

Hapa cha kulaumu ni barabara zetu tu na si kingine
Duhh, kazi kweli kweli. Hivi hiyo bara bara ya mto wa mbu Karatu ilivyo sasa utalinganisha na ilivyokua miaka ya 1990s? Bara bara hiyo ina shida gani mkuu? Umewahi kuona barabara zenye shida? Au unadhani bara bara zote zitakua kama Ubungo - Posta? Uzembe wa dereva na uchakavu wa chombo ndo vinabeba asilimia kubwa sana katika ajali mkuu.
 
Kwanza jambo muhimu dereva anauzoefu wa kuendesha gari za abiria? Na dereva ana umri gani? Tukianzia hapo tutapata majibu mazuri ya ajali
 
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina.

Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo.

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.

Kwanza kabisa nianze kwa kutoa pole kwa Familia zote zilizokumbwa na huu Msiba mzito na mkubwa kabisa, pili nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Wana Arusha wote bila kumsahau Mkuu wao wa Mkoa Comrade Mrisho Gambo na mwisho kwa Watanzania wote kwa janga hilo lililotokea hapa nchini Kwetu Tanzania na tumuombe Mwenyezi Mungu azipokee roho na Watoto wetu wote, Walimu na Dereva wa gari lile la Shule ya Lucky Vicent aziweke mahala pema peponi Amin / Inshaallah.

Kwa mtazamo wangu binafsi naweza nikapingana na Mtoa mada juu ya baadhi ya lawama zake alizoziweka hapo juu japo nikiri wazi pia kuwa kuna mahala pengine amesema mambo ya wazi na ya kweli kabisa ambayo Mamlaka husika zinapaswa kuyachukua na kuyafanyia Kazi.

Najua kuwa wengi wetu tunaweza kumtupia lawama yule Dereva wa lile Basi ila niseme tu wazi kuwa ile ajali ya jana imetokea kwa BAHATI MBAYA sana na haina cha kumlaumu. Ukiona ajali yoyote ile inayohusisha Mabasi ya Abiria halafu hadi Dereva na zingine Dereva na Utingo / Kondakta wake nao ' wamekufa ' basi jua ya kwamba hiyo Gari hata Yeye ( Dereva ) ilimshinda na siyo ya kawaida.

Inasemekana kwamba sababu kubwa hadi iliyopelekea hiyo ajali ni kwamba Basi lilikuwa katika Spidi kiasi na siyo kubwa kama ambavyo tunaanza kupeana ' Sumu ' mitandaoni na kwamba Gari lilipofika katika huo Mlima kulitokea ' Ukungu ' mkubwa mno wa ghafla hali ambayo ulimchanganya Dereva kiasi cha kutaka kupunguza kidogo Spidi ili aende kwa ' tahadhari ' ndipo Gari lile ( Basi ) likaanza ' kuyumba ' huku likisaidiwa na ' utelezi ' uliokuwepo pale na ambao ulitokana na hali ya ' unyevu unyevu ' hali ambayo ilifanya Gari lile likose mwelekeo na kuanza kuyumba yumba hadi likaingia ' Korongoni ' pale na kusababisha yale ' mauti ' ya kutukuka ya Watoto wetu wapendwa, Walimu wao na Dereva.

Nadhani kwa maoni yangu kama tukisema tutupe lawama mahala fulani basi itapendeza sana kama tukizipeleka hizi lawama zetu kubwa kwa Mamlaka husika hasa Tanroads ya Mkoa wa Arusha na hata Serikali vile vile kwa kuweza ' kuzembea ' kuweka angalau ' Vizuizi ' vya pembeni ( Kingo ) ili kuweza kuepusha ' Ajali ' kama hii kwani hata ukiangalia tu ile sehemu ilipotokea ajali utaona ni barabara nzuri tu ila hapo katika bonde hakuna ' Kingo ' zozote hivyo ni rahisi mno kwa Gari lolote kutumbukia humo pindi pakitokea ' hitilafu ' yoyote.

Mwisho kabisa nimalizie tu kwa kusema kuwa kuanza kuwalaumu Walimu wa Shule au Mmiliki wa Shule au sijui Madereva wa wale Wanafunzi hakutosaidia kitu kwani wao kama wao walitimiza wajibu wao na bahati nzuri ni kwamba kumbe hii siyo mara ya Kwanza hao Watoto wanaenda kufanya hiyo mitihani ya ujirani mwema na kwamba ni mara ya tatu isipokuwa tu sisi kama Wanadamu tutambue kuwa kuna bahati mbaya maishani na siamini kabisa kama Walimu au Mmiliki wa Shule hiyo ya Lucky Vicent alipanga hili kutokea au hata amelifurahia.

Ni ajali tu ya bahati mbaya hivyo kikubwa tu kama Wanadamu kuanzia sasa tunatakiwa tuchukue tahadhari siyo tu hapo Karatu bali hata maeneo mengine ambapo tunajua kuna miundo mbinu mibovu au hali ya barabara siyo nzuri pindi pakiwa na mvua na hata Wahusika hasa TANROADS nao wanapashwa kuhakikisha kuwa sehemu zote hatarishi za barabara Kuu za Mabasi usalama wake hasa wa Kingo za bondeni umezingatiwa ili basi Tanzania isije ikapata tena ' Mkasa ' mkubwa kama huu.

Poleni sana Watanzania wote na GENTAMYCINE nipo nanyi katika ' majonzi ' katika kipindi hiki kigumu kabisa cha huu Msiba kikubwa tuwape ushirikiano mkubwa na wa hali na mali ' Wafiwa ' wote, tuwafariji na tuwaombee Mwenyezi Mungu awape moyo wa ' subira / uvumilivu ' mpaka pale tutakapowapumzisha ' Wapendwa ' wetu katika Nyumba zao za Milele na wala hakuna haja ya kuanza kuichukia Shule ya Lucky Vicent au kumchukia sijui Mwalimu Mkuu au Mmiliki wake kwani hili jambo lingeweza kutokea mahala popote pale na hata kumtokea Mtu yoyote yule.

Muinto Obrigado nyote na tupo pamoja.
 
Kwa kuwa we continue to point our fingers towards the wrong direction,tutaendelea kuangamia day in and day out.Very sad.Sijui kwa nini we are so afraid to confront our real enemy,the Devil and his agents who are all around us.
Who is the real enemy!!! The devil??? Serious??? Ndiyo maana nchi hii haiendelei na haitaendelea kwa sababu wapiga kura na wapigiwa kura wote ni wale wale.
 
inasikitisha sana ni sahihi ulichokiandika lakini mkuu kaa ukijua ajari haina kinga gari linaweza kuwa na hayo yote na dreva ni mzoefu wa miaka mingi ninachoweza kusema yawezekana dreva alikuwa mzembe sawa lakini! ! mazingira yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajari yani mvua, ukungu na mahali penyewe yote kwa yote tunapata fuzo kubwa sana sisi tuliobaki Mungu awalaze mahali pema watoto wetu majeruhi awaguse pole kwa kwawalio fikwa na msiba

kinachonipa shida ni mtoto alietoka akiwa hana ana mchubuko zinazunguka picha 2 tofauti za jinsia tofauti sijui ninani kati yao muhusika
napia wanasema aliepona alikuwa kwenye gari la nyuma tofauti na lile lililo pata ajari maana gari zilikuwa wengine wanasema 4 inasikitisha sana kwakweli
Acheni akili za kijima,
Watoto wote wangekuwa wamefunga mikanda wangekufa?
Ajali nyingi ni uzembe,uroho wa kubania pesa, ujinga pamoja na imani hizi za kishirikina.
 
Kuna siku nilisikia clouds wanajadili suala la magari ya shule kuwa mabovu...
Walitoa ushauri trafic wawe wanakagua sana haya mabasi...

Hata kama hii si sababu...lakini jamani shule nyingi magari yao ni reject...
Watoto kwa kuwa ni wadogo hawasemi kwa wazazi ...
Wenye shule kama hamna uwezo wa ku manage magari bora mge outsource tuuu....
 
Hiyo ni ajali msitafute visingizio. Ivi wangeongoza kitaifa mngeleta thredi ya basi kujaza kuliko uwezo wake?
 
Huyu mkuu wa shule mwenyewe alikuwa anajikanganya...eti tuliyafanyia matengenezo hayo magari na tuna mafundi hapa hapa shule...na hayo magari matatu ndio yalikuwa na hali nzuri...
Nimejiuliza yaliyobaki (yenye hali mbaya) hayabebi watoto ...?????Hii issue ichukuliwe kama fundisho...
 
Ndugu umekosea sana bara bara iko sawa haina tatizo ina alama za barabarani zote inasafirisha 90% ya watalii wote wanaokuja kanda ya kasikazini hawapati ajali sababu madereva wameenda shule Na magari siyo mabovu usitetee ujinga kwa imani potofu
Ni vema tukaelezana ukweli kama hivi, maana baadhi ya watu akili zao hazifai kuleta ufumbuzi wa matatizo ya nchi hii. Eti ubovu wa barabara!!!!???
 
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina.

Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo.

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.
Likishaandikwa school,bus hawa wakubwa wa barabara hawana time nalo!!!!!!
 
Acheni akili za kijima,
Watoto wote wangekuwa wamefunga mikanda wangekufa?
Ajali nyingi ni uzembe,uroho wa kubania pesa, ujinga pamoja na imani hizi za kishirikina.
Hii pia point...ukiangalia gari limeharibika kwa mbele tu...ila viti vimechomoka (ubovu) na kama vingekuwa na ubora na kungekuwa na mikanda wasingekufa kwa wingi huo...hili liwe funzo maana wako wengi wanaobeba watoto wetu kwenye magari mabovu...
 
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina.

Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo.

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.
Nawapa pole wazazi waliofikwa na msiba. Nimesikia kuwa hats Rais wa Kenya Mheshimiwa Kenyatta alisimama kwa muda kwenye mikutano take ili kutoa salaamu kwa ajili ya watoto hao. Sisi wahusika tamko letu likoje.
 
Ila kwa abiria 35 kw costa haikuwa overloaded, nadhan kuna matatzo mengne tu
 
Back
Top Bottom