Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Hili ndilo jibu katika point zote, Traffic jaeakagui mabasi ya Shule. Mabasi yote ya mjini daladala na mabadi ya shule hayana mikanda ya abiria, km ingekuwepo vifo vingepungua, kwani watoto wangebaki kwenye viti, idadi jsingefika hiyo. Mwisho dereva na Basi lenyewe havina uzoefu, mabasi ya mijini vibreki ma vya papo kwa papo, huo Mlima tembo una mwinuko na mteremko mrefu kabla hujafika mteremko mwingine wa ajali ni lazima breki silishakorofisha
 
Hamkawii, bongo zikigota kufikiri mnasingizia ulozi.

Gari limejaza, mwendo wa kasi, eneo hatarishi milima na kona kali, hakuna mikanda ya usalama..

Bado tu ...huoni?
Ajali husababishwa na mambo mengi sana na ulozi ukiwepo, tembea uone mkuu, dereva akimbize kwani hapendi uhai wake?
 
Ajali haina kinga sawa na kujikwaa na kuanguka la msingi kuchukua tahathari kwa kuyafanyia matengenezo ya kina magari tunayo yatumia pia ikumbukwe magari haya sisibinadamu ndiyo tunayo yatengeneza haya uwakika wa asilimia mia moja breki zinaweza kufeli muda wowote hatakama gari likiwajipya kinachofanya gari kufunga breki niviraba vya plastiki kwa magari ya aina ya rossa kama hiyo iliyopata ajali au coastar ukionyeshwa ivyo viraba unaweza usipande gari vikitumbuka tu biashara imeisha labda usimamie gia lakini sio breki madereva wanajua tusilaumu sana chamsingi nikumuomba m/mungu kabla ya kuanza safari yoyote ile
 
Waswahili mnapenda conspiracies...
Hiyo gari inabeba abiria 32 watu wazima.
Na kwakua ni school bus tena ya primary na nursery zinakua zinafungwa seats kulingana na size ya abiria wenyewe.
Zinauwezo wa kubeba abiria hadi 50. Kama ni watoto wa dizaini hiyo.
Gari yenyewe ilopata ajali ni Mitsubishi Rosa Fuso engine type ni 4D33 cc4210 tena nyingi hizo bus zinafungwa turbo Kwahiyo nguvu ipo.
Tufanye waliikodi bado kiasi cha abiria kilikua sawa kwa idadi ya watu 38 watoto 34 watu wazima wanne.
Unavyo lalamika kuhusu maintainance na blah blah blah nyingine unasahau kama hizo Shule huwa na mafundi wake na services ni kitu kinacho zingatiwa kwakua Ina beba roho za vijana wetu.
AJALI haina excuse na ni unforeseen circumstance... Karibia wiki mbili zilizo pita basi mpya kabisa kampuni ya Panda imeanguka lakini wibonela na ubovu wake wote ule linadunda tu.
Waacheni vijana wetu walale kwa Amani. Kuna factors nyingi zinaweza sababisha ajali.
Hiyo gari imeanguka ikiwa inashuka mteremko na kwa picha inaonyesha kabisa kulikua na hali ya mvua mvua na kama wewe ni mtu wa magari you must know what happens pale ukijaribu kufunga breki na mvua imenyesha.
Kashata za tairi hazishiki lami.
Muache kua majudge dereva wa hiyo gari ndio ajuaye nini kilicho msibu mpaka ajali ikatokea.
Unadhani madereva hufa kibwege bwege kwenye ajali.
Hii ilimshtukiza na katika harakati za kujaribu kuokoa hao watoto na yeye ame perish pamoja nao.
 
Tatizo la haya yote ni uongozi usio zingatia sheria na haki za binadamu,
Kila kipindi unaona wanafurahia kusanyo la faini barabarani zinapanda kwa kasi badala ya kufanya bidii za kupunguza ili makosa yapungue wenyewe wanafurahia faini
 
Hii ni kweli kabisa. Vile vile wanaposafiri magari yao yawe yanakaguliwa na kuangalia kama yanakidhi matakwa ya usalama barabarani hasa idadi yao kwa kulinganisha siti zilizopo ndani ya basi. Kuna siku niliwaona walikuwa katika ziara ya kutembelea mbuga za wanyama, idadi yao ilikuwa ni kubwa sana ukilinganisha na uwezo wa basi!
 
Mkuu unasema mazingira kuchangia, yaani mvua, ukungu na mahali penyewe.

Hivi mfano wewe unaendesha gari say sehemu kubwa ya safari yako unakwenda 120 au 100 kph na umefika sehemu ina mvua tuseme imechanganyika na ukungu na sehemu hiyo tuseme ina kona kali, miteremko au milima mikali, nadhani utabadilika na kuendesha kulingana na hali hizo zitakavyokuruhusu. Madereva wengi hawana hizi ABC za kwenda na mazingira, hili ni tatizo.

Kiufupi, asilimia kubwa ya ajali duniani kote, huwa ni uzembe wa wanadamu. Hiyo ajali imeua sana kutokana na pia watoto hawakufunga mikanda hivyo baada ya gari kukita kwenye korongo kwa mbele, watoto wote wa nyuma, walitupwa mbele kwa kasi ya mwanguko.

Haya yote ni uzembe, kwa gari ya abiria tena watoto kutofunga mikanda.

Mtu ukiwa na gari yako private tena labda uko peke yako ukikutwa hujafunga mkanda, fine 30,000/- sasa hapo liko wapi. Tubadilike watanzania, tukizidi kutoa hizi excuses hatutajifunza kwa makosa.
 
hiz poit zingetolewa kabla ingesaidia ila sasa it is useless
 
Kuna hili la matumizi ya simu dereva anapoendesha gari. Madereva wengi sana hufanya kazi hizi mbili kwa wakati moja. Kama sio hitilafu ya gari, basi nadhani alikuwa anaongea na simu au anaangalia sms wakati akiendesha. Nitaunga mkono iwapo faini kubwa itatozwa kwa dereva yeyote atakaepatikana kuongea na simu huku akiendesha gari isipokuwa kama gari lina radio call.
 
Mkuu, bus kama hili shule ngapi zinaweza nunua? kumbuka tangu ndalichako aseme waliosoma english medium wakifika chuo kikuu hawapati mkopo watoto hawapelekwi tena shule hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…