Ajali mbaya ya Gari 3 Karagwe Mkoani Kagera, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Ajali mbaya ya Gari 3 Karagwe Mkoani Kagera, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Kalanga Lisser,amedhibitisha kutokea ajali ,katika eneo la Kiyanga wilayani humo.

Dc Kalanga,ameongea na kasibante radio Bukoba,ambapo amesema kuwa kwa sasa hawezi dhibitisha vifo ni vingapi na majeruhi ila ajali ni mbaya.

Amesema kuwa roli likiwa limebeba maparachichi limeigonga kwa nyuma Haice iliyokuwa ikitokea karagwe kwenda bukoba na Haice kugonga Costa iliyokuwa ikitoka Bukoba kwenda Karagwe.

Mmoja wa mashuhuda ameiambia kasibante radio bukoba,kuwa ameweza kusaidia kutoa baadhi ya maiti katika Gari ya haice.

Tutaendelea kuwapatia updates.


Update.
Kwa mjibu WA taarifa ya polisi vifo ni saba na majeruhi ni 9.

Dhibitisha = Thibitisha
Roli = Lori
 
kwenye iyo ice sidhani kama katoka mtu. mwisho wa mwaka huu, makafara kibao sometimes hata madereva sio wa kuwalaumu, wanajikuta imetokea hivyo. tukumbuke kumpa Yesu maisha, tuokoke ili lolote likitokea uwe na pa kwenda.
 
Njaa
Tutaendelea kuwapatia updates.
Njaa za uhamiaji, Polisi na watu wa ushuru wa mazao kuweka barrier kizembe imesababisha watu kufa na kujeruhiwa.

Hivi vitendo vya kuweka vizuizi au barrier bila mamlaka husika kuchukua tahadhari zikemewe kwa sauti kuu.

Inatakiwa waweke koni, alama na kadhalika umbali mrefu ili kukinga ajali au kutengeneza eneo maalum ambapo magari yatachepuka na kufanyiwa ukaguzi wa uhamiaji, mazao au shuku wa wahalifu kwa usalama zaidi.

Lawama zote ziende kwa walioweka barrier kizembe katika mazingira hatarishi.
 
Back
Top Bottom