Ajali tano kubwa zaidi zilizowahi kutokea Tanzania

Kila nikiangalia yanayoendelea Uturuki naogofywa na hii dunia japo yenyewe ni majanga ya asili, watu 16,000 mpaka sasa wamefariki. Nimejifunza pia duniani janga lililoondoka na watu wengi kwa muda mfupi ni mafuriko ya mto Yangtze yaliyoondoka na maisha ya watu milioni 3.7 huku tetemeko lililoondoka na watu wengi zaidi ni lile lililotokea Haiti mwaka 2010 likiondoka na watu 200,000-300,000.

Tukirudi kwenye mada, Tanzania kikubwa kinachoondoka na watu ni ajali kuliko majanga ya asili na hii ni orodha ya ajali zilizoondoka na watu wengi zaidi mpaka sasa.

5: MV Skagit - 2012

Ajali hii ilitokea miezi 10 tu baada ya kutokea kwa ajali ya MV Spice Islander. Ilikuwa Julai 18, 2012 majira ya alasiri meli hii ya MV SKAGIT ilipozama katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.

Wananchi walikumbushwa machungu ya ajali ya MV Spice Islander kwa ajali ya meli ya Skagit iliyoua watu 81, wakiwemo Watanzania 75, Wakenya 3, Waholanzi 2 na Mrundi 1. Aidha, watu 212 walipotea na 154 walinusurika wakiwemo Waholanzi 5, Wajerumani 4, Wabelgiji 2, Wamarekani 2 na Waisraili 2. Kwa mujibu wa ripoti tumwe iliyoundwa kuchunguza ajali hiyo

Chanzo cha Meli hii iliyoundwa nchini Marekani mwaka 1989 na kampuni ya HALTER MARINE kuzama inaelezwa ilikuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa.

4: Ajali ya Treni -Msagali - 2002
Dodoma

Ajali ya treni iliyotkea Msagali Dodoma ni moja ya ajali kubwa za treni Tanzania

Kwenye upande wa ajali mbaya za treni kuwahi kutokea Tanzania hii ni miongoni mwao. Ajali ya treni ya abiria Namba A.12 ilitokea kilomita 388 kati ya stesheni za Igandu na Msagali Juni 24, 2002 saa 2.30 asubuhi.

‘Taifa limekumbwa na msiba mkubwa’ hii ilikuwa sehemu ya taarifa fupi kuhusu ajhali hiyo aliyowasilisha waziri wa uchukuzi wakati huo Profesa Mark Mwandosya, bungeni Dodoma.

Watu 281 walipoteza maisha, maiti 193 zilitambuliwa na kuchukuliwa huku maiti 88 zilizikwa na mamlaka za serikali kwenye mazishi ya halaiki katika makaburi ya Maili Mbili Kata ya Miyuji mjini Dodoma 27 Juni 2002 kutokana na kutotambuliwa.

Inaelezwa treni hi ilikosa nguvu ya kupandisha muinuko na breki kushindwa kufanya kazi kabla ya kuanza kurudi kwa kasi kinyumenyume na kwenda kuvaana na treni nyingine ya mizigo.

3: MV Nyerere - 2018

Kivuko cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba watu 101 lakini siku ya ajali ilielezwa kujaza watu karibu mara mbili ya uwezo wake

Septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Ilikuwa moja ya ajali iliyoleta kumbukumbu ya ajali kubwa zaidi ya MV Bukoba. Iliyotokea katika ziwa hilo hilo.

Mhandisi wa kivuko hicho Alphonce Charahani alikuwa wa mwisho kuokolewa akiwa akiwa hai baada ya kukaa majini kwa saa 48.

Rais wa wakati huo hayati John Magufuli alipozungumza alieleza kuwa kivuko hicho cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 101, lakini kwa takwimu za miili iliyopatikana na pamoja na manusura, ni wazi kwamba chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria wengi kuliko uwezo wake.

2: MV Bukoba - 1996

Hii ni ajali ya kihistoria, pengine ni moja ya ajali iliyoua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuwahi kutokea Tanzania katika miongo ya hivi karibuni. Ilitokea Mei 21, 1996, na hata Serikali iliwahi kukiri kwamba ajali hiyo itaendelea kuwa miongoni mwa kumbukumbu mbaya kutokana na kuangamiza maisha ya mamia ya Watanzania wengi kwa wakati mmoja.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 800 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kilomita chache kutoka bandari ya Mwanza.

Ingawa ni miaka 26 sasa tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba, Bukoba ilipokuwa inakaribia bandari ya Mwanza umbali wa kilometa 56, aliyekuwepo na asiyekuwepo historia yake imeendelea kukaa vichwnai mwa wengi.

Meli hiyo iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 iliyokuwa tegemeo kubwa la kutoa huduma ya kubeba mizigo na abiria ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bandari za Bukoba na Mwanza. Siku ya ajali inaelezwa kupakia zaidi ya abiria 2,000.

1: MV Spice Islander - 2011

Pengine kumbukumbu ya muda mrefu ya ajali ya MV Bukoba inapunguza machungu ya ajali ya MV Spice Islanders. Kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hapo Septemba 10, 2011 katika eneo la Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, kulileta huzuni kubwa hasa visiwani humo kutokana na idadi kubwa ya watu kufariki.

Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya jopo lililoundwa kuchunguza ajali hiyo chini ya Jaji Abdulhakim Ameir aliyeongoza jopo la watu 10, watu 1370 walipoteza Maisha.

Uchunguzi unaeleza ilibeba abiria karibu mara nne Zaidi ya uwezo wake. Ilikuwa na abiria 2,470 wakati uwezo wake ilikuwa watu 620.

Tume iliyoundwa inasema meli hiyo ilibainika kuwa na hitilafu iliyojulikana miezi miwili kabla ya kuzama kwake kutokana na ukaguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa bahari Sumatra, lakini bado meli hiyo ilipewa leseni.
2010:
Babu wa Loliondo kuwanywesha chai feki viongozi wote wakubwa wa nji ensi hiso.
 
Kwenye tetemeko la uturuki nimeguswa na kuokolewa na kichanga ambacho familia yake yote imeangamia, lakini ni yeye tu yani yeye tu aliyezaliwa katika mazingira ya mama kushtushwa na tetemeko, akapona,, ukuu wa Mungu hausemeki kabisa[emoji22]
Mwenyewe hadi sasa najiuliza kaliwezaje ishi masaa yote ndani ya kifusi, kaliwezaje ishi kwa kulia kwa muda wote huo.

Kuna mwingine nimeona waokozi walitaka shusha sululu, ila mmoja akavuta, kuvuta ni mtoto yuko hai...

Mungu wetu ni mkubwa sana
 
Inastaajabisha yani katika hilo tetemeko habari kuu ya kusisimua ni hiyo,, eneo hilo hilo alipozaliwa ndipo baba, mama na ndugu zake 4 wamepoteza maisha ila yeye tu kichanga cha masaa machache tu akapona, inawezekanaje!!! Acheni aitwe Mungu matendo yake hayachunguziki
 
Yeah mkuu hizi ajali zimetuachia simanzi kubwa sana hapa nchini hasa ukiwa sehemu ya ajali ,umeshuhudia wakati zinatokea au umeingia kwenye ajali muda mfupi baada ya kutokea, binafsi ajali ya wale wanataarabu waliokuwa wanatoka ziarani mbeya na kufika mikumi national park wakapata ajali ile na coaster yao kuungua moto, ilinisikitisha sana maana Nami niliingia eneo la tukio within mins
 
Hizi ajali za majini zina uzembe mkubwa, hebu fikiria chombo kina beba mara nne ya uwezo wake. Na huu ujinga bado unaendelea
 
Kila nikiangalia yanayoendelea Uturuki naogofywa na hii dunia japo yenyewe ni majanga ya asili, watu 16,000 mpaka sasa wamefariki. Nimejifunza pia duniani janga lililoondoka na watu wengi kwa muda mfupi ni mafuriko ya mto Yangtze yaliyoondoka na maisha ya watu milioni 3.7 huku tetemeko lililoondoka na watu wengi zaidi ni lile lililotokea Haiti mwaka 2010 likiondoka na watu 200,000-300,000.

Tukirudi kwenye mada, Tanzania kikubwa kinachoondoka na watu ni ajali kuliko majanga ya asili na hii ni orodha ya ajali zilizoondoka na watu wengi zaidi mpaka sasa.

5: MV Skagit - 2012

Ajali hii ilitokea miezi 10 tu baada ya kutokea kwa ajali ya MV Spice Islander. Ilikuwa Julai 18, 2012 majira ya alasiri meli hii ya MV SKAGIT ilipozama katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.

Wananchi walikumbushwa machungu ya ajali ya MV Spice Islander kwa ajali ya meli ya Skagit iliyoua watu 81, wakiwemo Watanzania 75, Wakenya 3, Waholanzi 2 na Mrundi 1. Aidha, watu 212 walipotea na 154 walinusurika wakiwemo Waholanzi 5, Wajerumani 4, Wabelgiji 2, Wamarekani 2 na Waisraili 2. Kwa mujibu wa ripoti tumwe iliyoundwa kuchunguza ajali hiyo

Chanzo cha Meli hii iliyoundwa nchini Marekani mwaka 1989 na kampuni ya HALTER MARINE kuzama inaelezwa ilikuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa.

4: Ajali ya Treni -Msagali - 2002
Dodoma

Ajali ya treni iliyotkea Msagali Dodoma ni moja ya ajali kubwa za treni Tanzania

Kwenye upande wa ajali mbaya za treni kuwahi kutokea Tanzania hii ni miongoni mwao. Ajali ya treni ya abiria Namba A.12 ilitokea kilomita 388 kati ya stesheni za Igandu na Msagali Juni 24, 2002 saa 2.30 asubuhi.

‘Taifa limekumbwa na msiba mkubwa’ hii ilikuwa sehemu ya taarifa fupi kuhusu ajhali hiyo aliyowasilisha waziri wa uchukuzi wakati huo Profesa Mark Mwandosya, bungeni Dodoma.

Watu 281 walipoteza maisha, maiti 193 zilitambuliwa na kuchukuliwa huku maiti 88 zilizikwa na mamlaka za serikali kwenye mazishi ya halaiki katika makaburi ya Maili Mbili Kata ya Miyuji mjini Dodoma 27 Juni 2002 kutokana na kutotambuliwa.

Inaelezwa treni hi ilikosa nguvu ya kupandisha muinuko na breki kushindwa kufanya kazi kabla ya kuanza kurudi kwa kasi kinyumenyume na kwenda kuvaana na treni nyingine ya mizigo.

3: MV Nyerere - 2018

Kivuko cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba watu 101 lakini siku ya ajali ilielezwa kujaza watu karibu mara mbili ya uwezo wake

Septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Ilikuwa moja ya ajali iliyoleta kumbukumbu ya ajali kubwa zaidi ya MV Bukoba. Iliyotokea katika ziwa hilo hilo.

Mhandisi wa kivuko hicho Alphonce Charahani alikuwa wa mwisho kuokolewa akiwa akiwa hai baada ya kukaa majini kwa saa 48.

Rais wa wakati huo hayati John Magufuli alipozungumza alieleza kuwa kivuko hicho cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 101, lakini kwa takwimu za miili iliyopatikana na pamoja na manusura, ni wazi kwamba chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria wengi kuliko uwezo wake.

2: MV Bukoba - 1996

Hii ni ajali ya kihistoria, pengine ni moja ya ajali iliyoua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuwahi kutokea Tanzania katika miongo ya hivi karibuni. Ilitokea Mei 21, 1996, na hata Serikali iliwahi kukiri kwamba ajali hiyo itaendelea kuwa miongoni mwa kumbukumbu mbaya kutokana na kuangamiza maisha ya mamia ya Watanzania wengi kwa wakati mmoja.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 800 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kilomita chache kutoka bandari ya Mwanza.

Ingawa ni miaka 26 sasa tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba, Bukoba ilipokuwa inakaribia bandari ya Mwanza umbali wa kilometa 56, aliyekuwepo na asiyekuwepo historia yake imeendelea kukaa vichwnai mwa wengi.

Meli hiyo iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 iliyokuwa tegemeo kubwa la kutoa huduma ya kubeba mizigo na abiria ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bandari za Bukoba na Mwanza. Siku ya ajali inaelezwa kupakia zaidi ya abiria 2,000.

1: MV Spice Islander - 2011

Pengine kumbukumbu ya muda mrefu ya ajali ya MV Bukoba inapunguza machungu ya ajali ya MV Spice Islanders. Kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hapo Septemba 10, 2011 katika eneo la Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, kulileta huzuni kubwa hasa visiwani humo kutokana na idadi kubwa ya watu kufariki.

Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya jopo lililoundwa kuchunguza ajali hiyo chini ya Jaji Abdulhakim Ameir aliyeongoza jopo la watu 10, watu 1370 walipoteza Maisha.

Uchunguzi unaeleza ilibeba abiria karibu mara nne Zaidi ya uwezo wake. Ilikuwa na abiria 2,470 wakati uwezo wake ilikuwa watu 620.

Tume iliyoundwa inasema meli hiyo ilibainika kuwa na hitilafu iliyojulikana miezi miwili kabla ya kuzama kwake kutokana na ukaguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa bahari Sumatra, lakini bado meli hiyo ilipewa leseni.
Ajali mbaya ya mabasi ya abiria

Majinjah

11/03/2015

Hii iliwaacha watu chini ya watano tu kati ya 60+

Zaid ya 50 walifariki
 
Back
Top Bottom