john p gwau
Member
- Jan 21, 2015
- 81
- 25
Askari wa usalama barabArani ndo wanaosababisha ajali kwa uzembe wao, hawakagui gari, wanachofanya, wanasimamisha gari,wanachukua chao, generally siwapendi police, hasa wa usalama barabarani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo wakifutiwa leaeni majeruhi walio poteza viungo watapona na walio fariki watafutuka??
Ninge muelewa angesema kuanzia sasa maaskari wanao wapa madereva leseni kwa hongo, na wakaguzi wa magari wanaopokea hongo na kuruhusu mwendo kasi na magari mabovu kupakia abiria watafutwa kazi nakufungwa jela. Kamanda Mpinga amekuwa mno mwanasiasa kuliko askari.
Akiambiwa vijana wake ni wala rushwa huwa ana watetea wakati sisi ndio tuko nao na tunajua matendo yao. Naona sasa hata kama ni uhome boy, IGP Mangu afumbe macho afanye marekebisho kikosi cha usalama barabarani. Mauaji ya ajali Tanzania yamezidi ya boko haramu na malaria.
hatua muafaka kabisa
hata hivyo hatua hizi hazitoshi.
1. wapelekwe mahakamani na wahukumiwe kama wauwaji
2.wamiliki nao wachukuliwe hatua hizo hizo kwa kupakia abiria katika magari mabovu
3.fidia kwa wafiwa itolewe ya kutosha kulingana na sheria za nchi
Askari wa usalama barabArani ndo wanaosababisha ajali kwa uzembe wao, hawakagui gari, wanachofanya, wanasimamisha gari,wanachukua chao, generally siwapendi police, hasa wa usalama barabarani
Eneo lingine la kuangalia ni kupiga marufuku pome aina ya viroba. Vimeathriri sana madereva na vimechangia sana ajali vikisaidiana na simu za mikononi.
Kwani pombe aina ya viroba ndo ina kilevi tuu? Wakinywa pombe nyingine ruksa?
''Kutokana na ajali za barabarani ambazo watalawa kama vile wameshindwa kusimamia au kuchukua hatua za dharura kunusuru maisha ya watu ambayo yanapotea kila siku; Ningekuwa kiongozi ningesema haya yafuatayo:
''Sitaki kusikia ajali zinatokea, hivyo basi kamanda wa usalaama barabani wa eneo usika (eneo la ajali), mkuu wa wilaya wa eneo n.k , barua zao ziko tayari kufukuzwa kazi kama hayo yatatokea katika eneo lao ikiambatana na kutunga sheria ya kufungwa kwa miaka 3 jela kushindwa kuweka mikakati ya kuzuia ajali''
MATOKEO:Wakuu hao wataweka mitakati ya kudhibiti ajari, hutasikia ajari za hovyo ovyo.
2.Kama wauzaji wa madawa ya kuleya wamewekewa sheria kali,kwa nini madereva na wamiliki wa kampuni ya usafirishaji yasiwekewe sheria kali.
Mfano🙁a)ikithibitika ni uzembe wa dereva;Dereva akisababisha ajari atalipa fidia ya sh TZS 10 billion Na kifungo cha maisha jela
(b) Wamiliki wa mabasi hayo pia watalipa fidia ya TZS 10 billion na kufungiwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa miaka isiopungua 5
3.Serikali kufuta vyuo vya mitaani ambavyo havina sifa za kufundisha udereva.
Je kama haya yakisimamiwa kutakuwa na ajari barabari
e
WADAU TUJADILI
Taifa inabidi liingie katika maombi mazito, hii sio hali ya kawaida.......Mungu tunusuru na haya majanga.
Mungu awatie nguvu wote wanaopoteza wapendwa wao katika hizo ajali.