Vivax
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 520
- 184
Kwanza naunga mkono hoja kwamba ajali nyinga sana hapa nchini zinasababishwa na mwendo kasi uliozidi. Hili halina ubishi hata kidogo. Lakini niulize: Hivi unafikiria polisi wanashindwa kuzuia mwendo kasi uliozidi kwa sababu hawana ushahidi kuwa magari yanakimbia sana? Bila hata kutumia hiyo application unayosema ziko njia luluki za kujua kama basi inakimbia. Na zaidi niseme polisi wanajua kabisa magari yanayokimbia. Kitu kinachofanya haya mabo yasiishe ni rushwa! Nakuhakikishia kama kusingekuwa na rushwa iliyokithiri madereva wote wangeshika adabu na wangekuwa na mwendo unaokubalika. Ni kama wanaosema adhabu ya kifo itumike kwa mafisadi! Mimi huwa nasema kuwa tatizo si adhabu bali wanakamatika? Pamoja na changamoto hii lkn wazo lako bado ni zuri sana sana = ku-monitor speed ya mabasi!
Halfu njia ulipendekeza ya kutegemea applicatin ya simu sio realiable! Kuna navigation system nyingi tu tena za uhakika zinaweza kutumiwa na polisi kujua mwendo wa mabasi. Ukiwa sehemu kama Ulaya na unasubiri basi kuna sehemu zenye screen yenye ramani inakuonyesha basi linavyotembea, liko wapi na muda litakaofika na mwendo wake. Hivi ni vitu affodable kabisa kununulika. Mwisho niseme sikupinga wazo wako ila nimeonyesha changamoto zake nyingi na mwisho nikiri una wazo zuri lakini naomba tutumie navigation systems zilizo reliable na sio application za simu.
Nilimalizia kwa kuruhsu kama kuna mwenye wazo bora zaidi ...
naamini we ni moja wao .
her I mngekuwa wengi,
swali gumu toka kwako ni , kwani polisi hawabaini mwendo kasi?
wanabaini kazi ni kwako
RUSHWWWWWA