Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Kwanza naunga mkono hoja kwamba ajali nyinga sana hapa nchini zinasababishwa na mwendo kasi uliozidi. Hili halina ubishi hata kidogo. Lakini niulize: Hivi unafikiria polisi wanashindwa kuzuia mwendo kasi uliozidi kwa sababu hawana ushahidi kuwa magari yanakimbia sana? Bila hata kutumia hiyo application unayosema ziko njia luluki za kujua kama basi inakimbia. Na zaidi niseme polisi wanajua kabisa magari yanayokimbia. Kitu kinachofanya haya mabo yasiishe ni rushwa! Nakuhakikishia kama kusingekuwa na rushwa iliyokithiri madereva wote wangeshika adabu na wangekuwa na mwendo unaokubalika. Ni kama wanaosema adhabu ya kifo itumike kwa mafisadi! Mimi huwa nasema kuwa tatizo si adhabu bali wanakamatika? Pamoja na changamoto hii lkn wazo lako bado ni zuri sana sana = ku-monitor speed ya mabasi!

Halfu njia ulipendekeza ya kutegemea applicatin ya simu sio realiable! Kuna navigation system nyingi tu tena za uhakika zinaweza kutumiwa na polisi kujua mwendo wa mabasi. Ukiwa sehemu kama Ulaya na unasubiri basi kuna sehemu zenye screen yenye ramani inakuonyesha basi linavyotembea, liko wapi na muda litakaofika na mwendo wake. Hivi ni vitu affodable kabisa kununulika. Mwisho niseme sikupinga wazo wako ila nimeonyesha changamoto zake nyingi na mwisho nikiri una wazo zuri lakini naomba tutumie navigation systems zilizo reliable na sio application za simu.

Nilimalizia kwa kuruhsu kama kuna mwenye wazo bora zaidi ...
naamini we ni moja wao .
her I mngekuwa wengi,

swali gumu toka kwako ni , kwani polisi hawabaini mwendo kasi?
wanabaini kazi ni kwako

RUSHWWWWWA
 


Vivax usife moyo kuanzisha mada zenye tija.

Kukosoa ni kazi nyepesi sana. Mnapokosoa, fikirieni pia kupendekeza suluhu mbadala ya hoja au pendekezo lililoko kwenye mada. Wachache wameonesha mfano hapa.

Mimi nitaongezea kwa kushauri kila gari lifungwe dashboard camera. Kama ambavyo ni lazima gari kuwa na insurance, iwe lazima kufunga dashcam. Iwepo adhabu kwa watakaokiuka utaratibu huu.

hoja yako nimeipenda kuliko.yangu thanks nx
 
Jawabu ni Smart phone

Huawei Ascend Y530,download application iitwayo "My tracks"- controller akae siti yoyote ya BASI,safari ianze.
Speed,umbali, vyoote vitaonyeshwa na muda uliotumika kituo hadi kituo!

Mahitaji:-
1)smartphone kama iliyotajwa hapo juu au iliyo bora zaidi.

2)mtu(operator) wa simu hiyo
3)power bank(chargers)

4)My track(application) haihitaji mtandao wa simu ila smartphone iwe na line ya sim(sim card)


Utaratibu

Smartphone ikaguliwe na RTO au wakala wake!
Dereva asini kuwa smartphone yenye IMME 12345678... Ndiyo itakayo record mwendo wa basi lake kwa siku hiyo!

Kama una mawazo bora zaidi changia

Utakwama kwa sababu ya mtandao . Hadi sasa hatuna kampuni ya simu yenye mtandao njia nzima.
 
Unaweza kuovertake magari yaliyo kwenye mwendo kasi mkubwa bila ya wewe kuwa kwenye mwendo kasi mkubwa?

Hujaelewa point yangu vizuri.. labda usome tena mkuu

By the way kama wewe ni dereva utaelewa nilichoongea
 
I am not surekama wahusika wakoa serious hizi ajali! Na hii huenda athari ya muda mrefu.Ningelikua Rais, Ningeikujua hasa ambia taasisi ya elimu ya juu ifanyeunchunguzi bayana kuja na data/ information , kuanalyse mzizi wa hizi ajalikwasasa . Ajali kwa sasa ni janga! it is not safe anymore kusafiri kwabasi n ndio usafiri a wengi.
 
I am not surekama wahusika wakoa serious kuh. hizi ajali! Na hii huenda athari ya muda mrefu.Ningelikua Rais, Ningeiambia taasisi ya elimu ya juu ifanyeunchunguzi bayana kuja na data/ information , kuanalyse mzizi wa hizi ajalikwasasa . Ajali kwa sasa ni janga! it is not safe anymore kusafiri kwabasi na ndio usafiri wa wengi.

 
Hata abiria wenyewe tuwe kiini cha upunguzaji wa hizi ajali, watu wakihojiwa baada ya ajali utasikia wanasema 'huyu dreva tulimuona mda kuwa anaendesha na kuovertake bila mpangilio', ifike mahali tuwalazimishe madreva waendeshe kwa ustaarabu. Lakini hata abiria wengine ni wa ajabu sana, siku moja nimepanda daladala kutoka tabata kwenda kariakoo, mama mmoja amekaaa karibu na dreva akapokea simu anamweleza jamaa yake kuwa 'ningeshafika lakini hili gari linaendeshwa kama tunaenda harusini' ikabidi watu wote tumcharukie huyo mama'
 
Utakwama kwa sababu ya mtandao . Hadi sasa hatuna kampuni ya simu yenye mtandao njia nzima.

tracking device haihitaji mtandao was sim ,inahitaji GPS (global positioning system) tu, soma tens mada
 
Tatizo la ajali Tanzania ni wingi wa magari barabarani huku barabara zikiwa finyu, ubovu wa barabara, ubovu wa magari yenyewe na uzembe wa Dereva.

Ndio maana asilimia kubwa ya ajali ni kugongana yenyewe kwa yenyewe.

Tanzania mnaua Reli huku mkitegemea kusafirisha mizigo yote kwa barabara wakati huo barabara zenyewewe za toka enzi za mwalimu.

Uamuzi mgumu ni kufuta usafirishaji wa mizigo ya kwenda nje ya nchi kwa kutumia magari.
 
miye naitumia sana kwenye "route march" zangu ni za uhakika!
Ni rahisi tu ukiwa na smartphone ukadownload hiyo application kwenye Google play,halafu inakupa maelekezo
mwisho wa mwezi/mwaka itakupa jumla ya kilometres ulixokimbia kcls(ugali) ulotumika

Nashukuru sana mkuu....nitaifanyia kazi. Nia yangu hasa ni kufuatilia improvement yangu katika time ninayotumia kwa umbali fulani.
 
Mpinga-15April2015.jpg
images


KIKOSI cha Usalama Barabarani nchini, kimesema madereva wote waliosababisha ajali kwa uzembe zikiwemo za hivi karibuni, watafutiwa leseni zao.

Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ajali jeshi hilo limeazimia kufuta leseni za madereva hao.

Alisema ajali za hivi karibuni, zimesababishwa na uzembe wa madereva; hivyo ni lazima wafutiwe leseni na hawapaswi kufanya kazi ya udereva nchini na taarifa zao zitawekwa kwenye tovuti ili waajiri wengine wasiwachukue.

"Kuanzia sasa, mabasi yote yaendayo mikoani tutakuwa tunaangalia yametoka kituoni saa ngapi kwenye maeneo mbalimbali hadi linapomaliza safari yake...likiwa mbele ya muda hatua stahiki zitachukuliwa," alisema.

Kamanda Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali za hivi karibuni.


Chanzo: Majira
 
Kwa hiyo wakifutiwa leaeni majeruhi walio poteza viungo watapona na walio fariki watafutuka??
Ninge muelewa angesema kuanzia sasa maaskari wanao wapa madereva leseni kwa hongo, na wakaguzi wa magari wanaopokea hongo na kuruhusu mwendo kasi na magari mabovu kupakia abiria watafutwa kazi nakufungwa jela. Kamanda Mpinga amekuwa mno mwanasiasa kuliko askari.

Akiambiwa vijana wake ni wala rushwa huwa ana watetea wakati sisi ndio tuko nao na tunajua matendo yao. Naona sasa hata kama ni uhome boy, IGP Mangu afumbe macho afanye marekebisho kikosi cha usalama barabarani. Mauaji ya ajali Tanzania yamezidi ya boko haramu na malaria.
 
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, kimesema madereva wote waliosababisha ajali kwa uzembe zikiwemo za hivi karibuni, watafutiwa leseni zao. Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ajali jeshi hilo limeazimia kufuta leseni za madereva hao.

Alisema ajali za hivi karibuni, zimesababishwa na uzembe wa madereva; hivyo ni lazima wafutiwe leseni na hawapaswi kufanya kazi ya udereva nchini na taarifa zao zitawekwa kwenye tovuti ili waajiri wengine wasiwachukue. "Kuanzia sasa, mabasi yote yaendayo mikoani tutakuwa tunaangalia yametoka kituoni saa ngapi kwenye maeneo mbalimbali hadi linapomaliza safari yake...likiwa mbele ya muda hatua stahiki zitachukuliwa," alisema.

Alitoa wito kwa wamiliki wa mabasi kuwahamasisha madereva kupunguza mwendo kasi na kuajiri madereva wawili katika safari ndefu ili kupunguza ajali za barabarani. Watu 103 wamepoteza maisha na wengine 138 kujeruhiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Machi 11 hadi Aprili 12 mwaka huu, kutokana na ajali za barabarani. Kamanda Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali za hivi karibuni.[/QUOTE]
hata hivyo hatua hizi hazitoshi.

1. wapelekwe mahakamani na wahukumiwe kama wauwaji
2.wamiliki nao wachukuliwe hatua hizo hizo kwa kupakia abiria katika magari mabovu
3.fidia kwa wafiwa itolewe ya kutosha kulingana na sheria za nchi
 
Hata kama mkiwafutiabwote haisaidii, maana watu wenyewe hawajasoma, pili vileseni vyenu hivyo vinapatikana kiraisi sana kuliko hata sarafu ya sh. Kumi,

Mnacheza tuu kila siku mnakuja na mikakati isiyo na plan wala implimentaion itakuwaje,.

Mmmhhhjhsshhh
 
Back
Top Bottom