Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Angalia vichwa vya madereva wetu....hapo kuna kibao kabisa kuwa kuna kona kali lakini wanapitana hapo hapo! Ikitokea ajali kuna watu watasema ni kwasababu ya barabara na Mungu kapenda


Huu ni ukichaa, Madereva kama hawa naomba abilia tuungane asimamishe gari sehemu yenye usalama, dereva mwingine aendeshe. Tusikubali madereva wenye matatizo ya akili kuendesha magari.
 

Mkuu naungana na wewe kabisa, Hivi pombe ni chai? Mtu mwenye akili timamu hawezi kuendesha gari akiwa amelewa pombe. Mimi naomba tuanze sisi wenyewe hapa ACHA UPUMBAFU NA UJINGA WA KUENDESHA GARI UKIWA UMELEWA SIO SIFA HIZO.
 

Mkuu naunga mkono mada hii ni muhimu sana; kitu kingine tuanze kuwaambia hawa wamiliki wa mabasi wao hulipa bima, lakini sijasikia watu kulipwa fidia au kulipiwa matibabu kutoka katika bima. lakini wenye mabasi bima zinawalipa fedha nyingi au hata kureplace basi jipya endapo ajali ikitokea. Sasa tuwaambie makampuni ya bima kulipa fidia watu wote waliopate matatizo katika ajali mbalimbali.
 
Asante sana kimsingi ndivyo inavyotakiwa lakini abiria hupata shida kubwa mno kwenye fidia za bima na mwisho wa siku wanachopata hakilingani na madhara waliyopata
 
Asante sana kimsingi ndivyo inavyotakiwa lakini abiria hupata shida kubwa mno kwenye fidia za bima na mwisho wa siku wanachopata hakilingani na madhara waliyopata

Mkuu mimi naamini tukiwakomalia hawa jamaa wa bima kulipa fidia ajali za mabasi zitashuka 70%. I can guarantee that once they start paying, change will come and buses/cars accident will decrease. Mkuu tuhamasishe na watu wengine humu wanye kampuni za Bima "lipeni watu haki zoa msiwalipe wamiliki wa magari tu" Nitamwambie Mheshimiwa Magufuri atumbue jipu!!!
 
Kupitia JF na kupitia uzi huu pengine kelele zetu zinaweza kusikika
 
Abiria wengi wala ndugu zao hawajui kama wanastahili kulipwa bima pindi ajali ikitokea....Na wamiliki wa mabasi wanatumia loophole hio kujitajirisha,ajali ikitokea wanachukua malipo yote na hawawalipi abiria kama inavyotakiwa, katika hili wanashirikia na polisi na watu wa bima.
 
ajali hii imeondoka na roho moja huku ikijeruhi wengine akiwemo mke wa Waziri mkuu mstaafu mama Tunu Pinda
 
hasara kubwa ya roho vitu mali nguvu kazi ya Taifa wataalam na uchumi wa nchi
 
hizi ajari zinatibika sana kwa 60 mpaka 70% ni ajari ambazo zipo ndani ya uwezo wetu kabisaa.sema tuu hatujataka na kuamua.
kwa dunia ya sasa ya kidigital kuna vitu sio vya kuvifanya kabisaaa.tatizo technologia inatukimbiabsanaaa bongo na serikali yetu na vyombo vya usalama hawataki kamwe kuendana na mzingira na hali halisi.

kwa mbaali naona raisi wa sasa anayo nia na mwamko nahisi akipelekewq wazo zuri lakudhibiti haya majanga kamwe hata weza likataa.
sheria kali zitungwe na zisimamiwe kwa ufasaha bila kuwa na uonevu au upendeleo.

funga cctv camera barabarani sheria ikivunjwa adhabu kali itolewe.

ikiambatana na dereva kufungwa au kufungiwa leseni yake ikiwezekana kupumzishwa kwa mda.

leo hii dereva ana gonga mwenda kwa miguu kwenye zebra hachukuliwi hatua yoyote upande wa pili mwenda kwa miguu kapata ukilema wa maisha au kafa kabisaaa.

unashangaa mfano barabara ya mwenge ubungo mtu anapata au anagongwa au magari yanagongana pale mliman city penyewe kwenye geti la kuingilia dereva yupo kwenye speed 80 or 60 hapo unaanza kupata picha maana pale super star kuna mataa ukija mbele kidogo kuna kituo cha kivulini kuna stop zebra mbele yake kuna kituo cha mliman city na zebra mbele kidogo kuna round about sasa hembu pata picha.hapo utaona kabisa huyo dereva kwanza mataa anaweza akawa hakusimama stop zote kapita speed na hiyo round about angezunguka tuu.

polisi na trafic mpo mnabaki kuvizia tuu watu na kupigwa na upepo ofisini ukisubili mshahara kwani mnalipwa pesa ya nn??
na huku ndugu zetu na jamaa wanakufa.
 
Mkuu naungana na wewe kabisa, Hivi pombe ni chai? Mtu mwenye akili timamu hawezi kuendesha gari akiwa amelewa pombe. Mimi naomba tuanze sisi wenyewe hapa ACHA UPUMBAFU NA UJINGA WA KUENDESHA GARI UKIWA UMELEWA SIO SIFA HIZO.
mkuu ni bora wangekuwa wanakufa wenyewe na.magari yao lakini kibaya zaidi wanatuulia ndugu zetu wasio kuwa na.hatia.

hivi ina maana polisi wameshindwa kabisaa kudhibiti watu kuendesha magari wakiwa wamelewa??
viletwe vipimo na kwa hili jeshi la polisi ligaramikie tuu linunue kwa wingi sana.na kuvitumia mtu atakaye kutwa anaendesha gari kalewa hata liwe la kwake basi faini kali lazima imhusu.
 
.........funga cctv camera barabarani sheria ikivunjwa adhabu kali itolewe.

ikiambatana na dereva kufungwa au kufungiwa leseni yake ikiwezekana kupumzishwa kwa mda.

leo hii dereva ana gonga mwenda kwa miguu kwenye zebra hachukuliwi hatua yoyote upande wa pili mwenda kwa miguu kapata ukilema wa maisha au kafa kabisaaa.........
[/QUOTE]

LEGE;
Katika mengi uliosema naomba nisemee haya mawili:
Kufunga cctv camera barabarani na adhabu kali; Hizo cctv ni kwa ajili ya nini? Ina maana hizo tochi zoote hazitoshi unaongeza tena gharama ya camera? Hao wanaokimbiza magari ka mashindano wameshindikana kukamatwa kwa hizo tochi?? **** mahali hapako sawa hapo. Hata ungeweka camera ngapi, usipokijua kiini haisaidii.
Kuhusu dereva kugonga waenda kwa miguu. Hivi weye unaendesha gari au chombo chochote cha usafiri? Hata baiskeli tu?? Kama jibu ni ndiyo, utajua wazi kwamba, HAKUNA MWENDESHA CHOMBO CHA USAFIRI mwenye moyo mbaya mpaka amuue mwenda kwa miguu. Wengi wa waenda kwa miguu hudhani kuwa zebra crossing ni breki za kusimamisha magari. Hapana, hapana hapanaaaaa. Utaalam ni kuwa, ukifika kwenye zebra crossing, Fuata hatua zifuatazo: 1. Simama kwanza, Angalia kulia, angalia kushoto, Angalia kulia tena. 2. Kama hakuna gari hatari, Vuka kwa haraka. Usimwamini dereva yeyote.
Moyoni, elewa kwamba, kama ukigongwa ni weye unapata ulemavu au kupoteza maisha yako. Hakuna malipo ya kutosha maisha yako weye. Jitambueeeee.
Nimeona wanaojifanya watoto wa mujini wakijifanya Trafiki na kusimama katikati ya barabara ati wanazuia magari ili watembea kwa miguu wapite. Nasema, sintakaa nifanye hivyo. Nikiumia, hata hao niliowasaidia kuvuka, hawanisaidiiiiii.
Nawasilisha...
 
mshana jr hizi rekodi za wapi? India i guess...za tz ziko wapi?

RRONDO ndio maana nikaweka overall records na breakdown sisi hatuna vitu kama hivi...najitahidi kutafuta vitu vinavyofanana na hii post kwa faida ya wote...our sensitive organs wako busy na siasa they jus Don care about this...the nation is loosing the families are loosing. ..friends n relatives are loosing too...mwisho wa yote sote tunapoteza...
Nguvu kubwa imewekezwa kuhakikisha ccm inashinda visiwani....what a fucked up mind(sorry to say this)
Hata sasa ukienda kwenye mahospitali yetu kuna maiti na majeruhi wa ajali za barabarani wanaongoza! But who cares? Hata mods wa JF they just don't care!unafikiri huu uzi ungewekewa sticky kama nyuzi nyingine si ungekuwa msaada na chachu kwa wengine??? Tunapoteza hata members humu...!yuko wapi Dotto Mzamva n the like??? (RIP THEM ALL)
Tunahangaika kuleta nyuzi si kwa ajili ya sifa la hasha bali kama jukwaa na wanajukwaa tuwe chachu ya mabadiliko kwa mambo muhimu ya kitaifa
 
Post kama hizi zilipaswa ziwe live daily...kuwakumbusha washika dau na kujikumbusha watumiaji... China na wingi wao wameweza kudhibiti ajali kwa kiwango chake.....kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna ninini? ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…