View attachment 320681
Tunahitaji mjadala wa kitaifa katika hili kila mmoja wetu na kwa umoja wetu liwe ni jukumu letu sote.
Jamii Forum ilete msukumo chanya kwenye hili. Nchi imapoteza nguvu kazi wataalam na wazazi wa kesho.
Makaburi yanaongezeka kila uchao, yatima, wajane na wategemezi wanazidi kuongezeka! Ndoto nyingi zinazimika...mapato ya nchi yanazidi kutumika kununulia madawa na vifaa tiba
Walemavu wanaozeka!Taifa lina rudi nyuma nchi inahujumiwa na mamlaka zake yenyewe
.Kitengo cha polisi wa barabarani -kunatakiwa mabadiliko makubwa sana hasa idara ya leseni, zinatolewa kama njugu pesa ndio I naongea
.Shule za udereva-je zina wakufunzi wanaokidhi vigezo? Je wanafundisha umuhimu wa kukilinda na kukitunza chombo kisilete madhara kwa mtumiaji na wengine? Je wana elimu ya uchumi?
.wazazi walezi ndugu na jamaa-wanatimiza wajibu kuhusu usalama barabarani? Je hawashiriki kusaidia kupata leseni kwa njia za mkato na kufahamiana?
.vyombo vya habari-je jukumu Lao ni kuishia kutangaza kwa mbwembwe matukio ya ajali ? Hawa wana jukumu zito sana.
.TRA-walipa kodi wanazidi kuteketea, pokea pesa ya leseni lakini hakikisha huyo mtu ni mjuzi ili isije ikawa ndio pesa yake ya mwisho kupokea!unahitaji mapato una jukumu kubwa hapa.
.mitandao ya simu hili pia ni lenu mnahitajika sana kwakuwa ajali nyingi hutokana na kuongeza na simu
.wazalishaji wauzaji na wamiliki wa mabar na vileo-mnawahitaji hawa wateja muwaone tena na tena mnahusika moja kwa moja
Makundi mengine katika jamii sijayataja, madaktari wetu tuwapunguzie mzigo wa kutibu majeruhi ili nguvu zielekezwe kwingineko
Misiba siku hizi ni gharama kubwa familia zinaingia umaskini na kupoteza muda mwingi
Ajali za Tanzania ni mjadala wa kitaifa tuna jukumu kuhakikisha tunafanya kitu kwenye hili