Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,206
- 18,549
Naona lengo lako ni kuendelea kupoteza maisha ya watuUnaweza kutusaidia takwimu za haya mabasi ili tusione kama kauli yako ni kuharibu biashara za watu??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona lengo lako ni kuendelea kupoteza maisha ya watuUnaweza kutusaidia takwimu za haya mabasi ili tusione kama kauli yako ni kuharibu biashara za watu??
kwani hayo mabasi yanabeba mbuzi mpaka yasindikizwe!? Wanaopanda humo ni ni watu na akili zao na jeshi la polisi na SUMATRA wanatoa maelezo kila wakati toeni taarifa kama unaona mambo yanayofanywa na dereva safarini sio ya kawaida, matrafiki siku hizi wako wengi sana barabarani na wametoa namba za mawasiliano, hamtaki kuwasiliana nao mnataka msindikizwe na askari kwenye mabasi kuwa control madereva!Serikali ije na sheria inayolitaka jeshi la polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa mabasi kuajiri traffic na askali wanaosindikiza mabasi yote yaendayo mikoani. Hii itasaidia sana kupunguza ajali zitokanazo na uzembe na mizaha kama ilivyotokea kwa city boys.
Kwanza askali wa barabarani watakuwa namerahisishiwa kazi ya kusimamisha mabasi bila sababu za msingi. Pili madereva watendesha gari kwa kuzingatia taaluma yao. Tatu Abiria watajihisi wako salama muda wote. Nne itakuwa rahisi kugundua magendo yanayofanyika huko barabarani. Tano itarahisisha kuchukua hatua sitahiki kwa makosa yatokanayo na uzembe barabarani, kwa dereva abiria na askali wenyewe wasindikizaji. Sita tutakuwa tumepunguza rushwa za barabarani.
Mwisho Askali hawa lazama wapewe mafunzo maalumu na wawe committed kwa kazi yao, walipwe pesa ya kutosha na ili wasinunuliwe wawapo kwenye chombo. Wajibu wa abiria ni kuripoti mienendo ya Askali ndani ya gari mwisho wa safari na wajibu wa Askali itakuwa kuripoti usalama wa abiria na gari kila wanapofika standi kuu kwa mkuu wa usalama barabarani wa mkoa
Mara nyingi kinacho washinda abiria kutoa taarifa ni suala la usalama wao. Ukiwa ndani ya gari ni vigumu kumpigia trafiki simu ukizingatia wapo wengi watakao kupinga wakiona kama unawakwaza na wengine watakutishia kukushusha njiani.kwani hayo mabasi yanabeba mbuzi mpaka yasindikizwe!? Wanaopanda humo ni ni watu na akili zao na jeshi la polisi na SUMATRA wanatoa maelezo kila wakati toeni taarifa kama unaona mambo yanayofanywa na dereva safarini sio ya kawaida, matrafiki siku hizi wako wengi sana barabarani na wametoa namba za mawasiliano, hamtaki kuwasiliana nao mnataka msindikizwe na askari kwenye mabasi kuwa control madereva!
Sio kweli kwamba ajali haina kinga kinga unayo wewe abiria na dereva wako. Huwezi ona shimo mbele ya barabara na kwa vile umezoea kupita hapo siku zote bila shimo hilo kuwepo ukadharau kwa kuhisi umeona vibaya ukaamua tu upite. Mazoea waliokuwa nayo City boys ni mfano tosha kuthibitisha hili.Ajari aina kinga
Kwa haliwahusu? Au hawana ndugu?Duh. Kweli keyboard mnajua kuzitumia tatizo wenye mamlaka viziwiiiii